Maalim Seif Amlipua Profesa Lipumba........Asema Wanachama Waliojiunga CUF Kwa Sababu ya Lipumba Wanaweza KUONDOKA Pia

Wafuasi  wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) na pia mwenyekiti mwenza wa muungano wa wapinzani wanaounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Profesa Ibrahim Lipumba, wameanza kushughulikiwa na kutakiwa kuchagua moja; kuendelea kuwa ndani ya chama hicho au kutoka.

Ingawa Profesa Lipumba alipojiuzulu uenyekiti, alisema ataendelea kuwa mwanachama wa CUF, lakini Katibu Mkuu wa chama hicho, Maalim Seif Sharif Hamad amewataka wanachama waliokuwa wakimuunga mkono, kuamua moja, kubaki ndani ya chama hicho kama alivyoamua mchumi huyo mashuhuri duniani, au kutoka.

“Profesa Lipumba kajiuzulu CUF, wale waliojiunga CUF kwa sababu ya Profesa, wanayo fursa ya kuamua kubaki CUF au kutoka,” alisema Hamad juzi usiku.

Mbali na kuwataka wanaomuunga mkono Profesa Lipumba kuamua kutoka ndani ya chama hicho au kubaki, wakati kiongozi wao akiwa ameweka wazi kuwa hana nia ya kutoka katika chama hicho, Maalim Seif alitoa kauli zingine kuashiria kutohitaji hata uanachama wa Lipumba ndani ya CUF.

“Kama ni treni inayokwenda Mwanza, ikifika Morogoro abiria watashuka, lakini wengine watapanda, ikifika Kaliua watashuka abiria lakini wengine watapanda,” alisema Maalim Seif alipofanya ziara ya ghafla katika Makao Makuu ya CUF, Buguruni jijini Dar es Salaam juzi usiku.

Hamad amewahakikishia wanachama wa chama hicho waliokuwa wamezingira ofisi hiyo, kuwa uamuzi wa Profesa Lipumba kujiuzulu wadhifa wake hautausambaratisha Ukawa na CUF, ambayo kwa sasa haina Mwenyekiti wala Makamu Mwenyekiti, lakini akasema imeendelea kubaki katika mikono salama.

Alisema akiwa Katibu Mkuu na viongozi wenzake waliobaki, watahakikisha kwamba chama hicho kinafikia malengo ya kuanzishwa kwake, ambayo ni kuhakikisha kinakamata dola.

Alisema mwishoni mwa wiki hii, chama hicho kitaanza vikao vyake kuzingatia hatua iliyotokea, ili wachukue uamuzi thabiti wa kukiongoza chama hicho na kuhakikisha kinabaki katika mikono salama, hadi hapo uchaguzi wa kumtafuta Mwenyekiti utakapofanyika.

Akizungumzia Ukawa, Hamad alisema baada ya hatua hiyo ya Profesa Lipumba, alizungumza na viongozi wakuu wa umoja huo, akiwemo Freeman Mbowe (Mwenyekiti wa Chadema), James Mbatia (Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi) na Emmanuel Makaidi (Mwenyekiti wa NLD) pamoja na mgombea urais wa umoja huo, Edward Lowassa na wamehakikishiana kuwa hawatarudi nyuma.

“Tumehakikishiana kwamba Ukawa upo na umeimarika zaidi na hatutarudi nyuma… Tumeona kwa namna unavyoungwa mkono na wananchi walio wengi, Magufuli (mgombea urais wa CCM) Ikulu ya Magogoni hataiona,” alidai Maalim Seif.
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Maalimu laghai hicho chama ni mali yako binafsi au ni chama cha wananchi nini unatishia watu huku unawachamba kabla ya haja tafadhali kuwa muungwana usichambe wanachama wa kawaida kwa kuwaingiza ktk sokomoko lenu la viongozi hivi vyama vya kisultani ni taaabu sana eti CCM imeparaganyika tutachukua dola ni nani huyo wa kukupa Dola umtawale labda kichaa wa milembe

    ReplyDelete
  2. jidanyanye baba, lipumba ni tofauti na wewe, wewe ni mpemba na lipumba ni mbara acha kupayuka hovyo tuko cuf kwa ajili ya lipumba na siyo wewe na hatutoki ng'oo

    ReplyDelete
  3. Hayo sio maneno ya kutuambia wanachama wako tatizo vyama vya upinzani mnajaziba sana mtu akiamua kutoka maneno ya jeuri ya nini mshavurugwa nyie vyama vya upinzani na ikulu hatutaingia wee Zanzibar washakufunga mdomo kwa kukupa uongozi CUF bara bila lipumba tutaona.

    ReplyDelete
  4. Kwani huyo Lipumba alikuwa mkeo mpaka uwe na jaziba wanachama wa CUF ni wanao mama yao hakutaki watoto fukuzilia mbali wamfate mama yao hizi ni dalili vyama vya UKAWA ni vya kibabe kuliko Hitler mtatunyonga nyie kama mabadiliko tumesamehe baada ya nguzo za wanyoge kugive up Slaa na Lipumba hakuna mwingine wa kuleta mapinduzi ya uhakika tusubiri kina Slaa na Lipumba wengine labda watazaliwa baada ya miaka hamsini

    ReplyDelete
  5. wewe anaonymous wa 8/8 saa 4.06 pm: kwani ccm hawana maneno ya JEURI? Mbona haya maneno yametoka kwa kwa viongozi wa ccm: a) Watakiona cha mtema kuni b) makapi c) goli la mkono d) watasoma namba n.k. Nyie ccm ndio wenye haki na nchi ya TANZANIA? Mna dhamana ya kuongoza watu milioni 58 kwa miaka 70? Ondoka na upumbavu wako - pumbfu wee

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wacha CCM Itutawale mpaka kiama kwa ujinga wenu kama huo mmekosana CUF sasa unaingiza CCM unaitakia nini kama sio hulka ya mkosaji na uhasidi mpaka mna hasidi nafsi zenu kwani nchi ya wajinga ya kutawaliwa kwa zamu kama ni zamu mnae wa kuwawakilisha zaidi ya Kina Edo fisadi, Maalim Sefu anayefukuza wanachama kama vile chama ni mali yake sababu Lipumba je akishaka dola kuna kupona kweli wote tutakuwa wakimbizi, Mbowe mnataka rungu apewe kichaa

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad