Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC) imeagiza kurudiwa kwa uchaguzi katika majimbo matano yaliyopo Tanzania Bara kutokana na dosari mbalimbali zilizojitokeza katika mchakato wa kura ya maoni.
Majimbo yanayotakiwa kurudia uchaguzi wa kura ya maoni ni pamoja na Makete, Busega, Ukonga, Rufiji na jimbo la Kilolo.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Dodoma Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye amesema mchakato huo utarudiwa siku ya Alhamisi Agosti 13 mwaka huu.
Amesema baada ya uchaguzi huo matokeo yatapelekwa katika vikao vinavyoendelea kwa ajili ya uamuzi.
Akizungumzia kuhusu vikao vinavyoendelea katika ukumbi wa NEC mjini Dodoma amesema vikao hivyo vinaendelea vizuri ambapo jana kikao cha kamati ya maadili kiliendelea mpaka usiku.
Amesema leo wanatarajia kumaliza kikao cha Kamati Kuu ambapo kesho na kesho kutwa watamaliza na kikao cha halmashauri kuu ya chama hicho (NEC) kama ilivyopangwa.
hizo gharama wanaotumia kutengenezea uniform za ccm , zinatosha kuwalipa waliostafu na mambo mengine kwa wananchi.
ReplyDeletena hizo za ukawa zimetengenezwa na jiwe???????????? acha ujinga uliopitiliza
ReplyDeleteNAPE.....HIZI RASHA TUU, JE, MVUA ZIKINYESHA UTAKUWA WAPI? Anagalu sasa umeekaa kimya. Kinywa chako kilikuponza. Utakuwa MPINZANI SI SIKU NYINGI ZIJAZO. AU LABDA CHAMA CHAKO CHA MIJIZI KITAPOROMOKA POROMOKA. ANGALIA KANU AU UNIP ZAMBIA NA KADHALIAKA. NA.. MBAAAADOOOOO
ReplyDeletehuna jipya tuliza boli
Delete