Mwenzenu sikuwahi kuwa na mazoea ya kuangalia movie zetu za hapa nyumbani kwa maana mara nyingi huwa actors wana overdo hadi nikawa naboreka. sasa last weekend kwa kufuata ushabiki wa watoto nikakaa kuangalia, kwa kweli nilikuwa shocked na nikawa nashindwa kuelewa. Kwani ni nani anayewaandikia zile subtitles za kiingereza, halafu it seems ni myu mmoja ndiye huwa anapelekewa kwa jinsi zilivyo.
Ni aibu jamani, kama bado hamjafikia level hiyo ya lugha, acheni tu, wekezeni zaidi kwenye kiswahili basi ieleweke tu kwamba movie ni ya kiswahili. Au kama mnataka mpate soko la kimataifa, hebu mu-invest sana mpate professionals wanaoweza kuwaandikia lugha ya kueleweka, otherwise mnajiabisha na kuiabisha nchi hii, can you imagine unaeangalia movie ndo unaona aibu kwa niaba yao. Maana ile lugha inayoandikwa pale si english, bali direct translation from kiswahili inaishia kuwa pigini, au mnajaribu kutengeneza lugha ingine? Mi sijaelewa jamani.
Kama vipi muwe mnaniletea japo nina uelewa mdogo wa hii lugha naamini i can do better than that. Ni ushauri tu, najua kina Kanumba sijui Ray huwa mnapita humu, next time kwenye baraza lenu la wasanii hebu wekeni hii kama agenda, naamini wapo watu kibao ambao hata kwa kuvolunteer wanaweza ku edit na kusaidia kutoa lugha inayoeleweka.
By Carmel on Jamiiforums
MAONI: Nani Anaandikaga ‘Subtitles’ za Movies za Bongo?
2
August 08, 2015
Tags
Dstv ninewapigia wanioe kazi ya kutafsiri kwa kiingereza maana ni aibu
ReplyDeleteusemacho ni kweli. wahusika walifanyie kazi swala hili. ila nawe mleta mada, kanumba yupi unayesema anapita humu? ina maana hujui kuwa kanumba is late? RIP Kanumba
ReplyDelete