MTABIRI maarufu Bongo, Maalim Hassan Yahya ameibuka na kusema kwamba utabiri aliowahi kuutoa kwamba kuna mgombea urais atafariki, bado upo palepale.
Maalim Hassan alisema kuugua ghafla kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ni dalili tu za ukamilifu wa utabiri wake lakini suala la mgombea urais kudondoka na kufa akiwa jukwaani akifanya kampeni linakuja.
“Kuugua kwa Mbowe hakujatimiza utabiri kama ulivyosema ila hizo ni dalili tu lakini kuna mgombea atadondoka jukwaani akifanya kampeni na atakufa lakini haioneshi ni wa chama gani na hii ni kutokana tu na mwaka huu ulivyoanza kinyota,” alisema mtabiri huyo.
Mwaka huu mwanzoni mtabiri huyo alitoa utabiri uliyoonyesha kwamba kutakuwa na kifo cha mgombea urais pamoja na mambo mengine ikiwemo kuibuka kwa magonjwa ya kushangaza
wewe sasa umeamua kwa makusudi kuingilia mipango ya mwenyezi mungu.angalia unapotumiwa pia uwe na tahadhali.iepuke adhabu aawali ya mwenyezi mungu.tunakujua wewe ni ccm kama mimi,lakini uwe muoga kwa muumba wetu.adhabu aawali kutoka kwake inakusubiri.tubu.acha hizo kaka.waaleko.
ReplyDeletemaalim hassan yahya,nimekusoma.kwa heshima na taadhma, tunaomba ujitabirie mwenyewe,mwenzetu unaondoka lini?tunakusikitikia kwa kukubali kutumwa kwa visenti kidogo ukamchokoza muumba wetu.ikutangulie adhabu uliyojitakia.acha,acha,acha,epuka laana.muache mungu aitwe Mungu.MUWEZA WA YOOOTE EEEMIIN.
ReplyDeleteHivi huyu mtabiri sio mtoto wa yule Yahya ambaye alitabiri 2010, kuwa mpinzani wa Kikwete atakufa? Halafu cha ajabu akafa mwenyewe?... MUNGU tuhurumie...
ReplyDeleteJamani Mwehu huyu Si tuu anayo sasa, Laana kamili ya Mwenyezi Mungu Bali pia ni mkono mrefu Toka MSOGA.Mnaikumbuka siku ya kwanza ya Kampeni ya Urais pale Jangwani 2005 na maneno yaliyofuatia toka kwa Baba yake huyu Bw Hayaat?baada ya dhahma ile?RAIS MHE.LOWASSA JIANDAE KUAPISHWA.
ReplyDeleteHahahaa. Furaha Henry umetisha
ReplyDeleteUtabiri sio sahihi maana hakuna kifo kilicho tokea kwa mgombea kuanguka jukwaani akiomba kura.Kifo cha Mh.Mtikila kimesababishwa na ajali ya gari kila mtanzania anafahamu.
ReplyDelete"Utabiri ulisema mgombea urais ataanguka jukwaani na kufariki njiani anapokimbizwa hospitalini".
Hicho kitu hakikuonekana mpaka uchaguzi umemalizika.