Mtoto wa Zari Amliza Mwanamuziki Diamond Platnumz

HII ni kali! Muda mchache baada ya mwandani wake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ kujifungua salama, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, amejifungia chemba kisha kuangua kilio akisema Mungu ni mwema huku akiwataja waliowahi kuwa wapenzi wake, Penniel Mungilwa ‘Penny’ na Jokate Mwegelo kwa maneno yao ya shombo.

TUJIUNGE AGA KHAN
Tukio la kujifungua mchumba wa Diamond, Zari lilijiri Agosti 6, mwaka huu mishale ya saa 10:40 alfajiri katika Hospitali ya Aga Khan jijini Dar  ambapo alipelekwa usiku huo baada ya kujisikia uchungu ambapo alijifungua mtoto huyo wa kike.
Chanzo cha habari kilieleza kwamba, siku hiyo, wakiwa hospitalini hapo, muda mfupi tu baada ya Diamond kuambiwa kuwa tayari Zari amejifungua, jamaa huyo alilipuka kwa shangwe na baadaye akajifungia chemba na kuanza kulia.

Kilipenyeza kuwa baadhi ya watu walioshuhudia walijiuliza kisa cha kulia ambapo baadaye alisema kuwa watu walikuwa wamemsema mengi juu yake na ishu kupata mtoto.
AANGUA KILIO
“Diamond alijikuta akiangua kilio, suala ambalo mwenyewe lilianza kunitia hofu maana kabla hajaanza kulia alikuwa akichekelea na hatukujua aliingiwa na nini hadi akaanza kulia huku akimshukuru Mungu kwa kumletea mtoto.
“Ila nilipomuuliza zaidi kinachomliza alisema kuwa amejikuta akifurahia hadi kulia kwani kabla Zari hajajifungua, alikuwa akiwaza sana kutokana na maneno ya watu ambao wengine walikuwa wakimwandikia meseji na kumtishia kuwa hawezi kuzaa salama,” kilitiririka chanzo hicho na kuongeza:

“Eti alisema kwamba, kuna siku alikuwa hapati kabisa usingizi kufuatia ishu ya kutopata mtoto hasa anapowaza maneno ya watu na mara nyingine alipokuwa akikumbuka maneno ya Penny na Jokate ambao walikuwa wakisema hana kizazi hivyo Mungu alikuwa amewajibu bila kinyongo yote waliyokuwa wakimuombea mabaya.

HUYU HAPA DIAMOND
Baada ya kupenyezewa ‘ubuyu’ huo, gazeti hili lilimtafuta Diamond ili kumdadisi zaidi juu ya kilio hicho ambapo alipopatikana alisema kuwa anamshukuru sana Mungu kwa kutimiza ndoto yake na kwamba sasa milango ya heri imefunguliwa hivyo hana sababu ya kueleza machungu yote aliyokuwa nayo zaidi ya kumshukuru  Mungu kwa kuwa yeye ndiye mweza wa yote.
“Siwezi kuweka wazi hilo ila kikubwa ninachoweza kusema kwa sasa namshukuru Mungu kwa kunianzishia historia mpya hivyo namuomba aendelee kumlinda mke wangu na familia yangu,” alisema Diamond.

Hadi gazeti hili linakwenda mitamboni, bado Zari alikuwa hospitalini huku mama Diamond, Sanura Kassim ‘Sandra’ akimhudumia mtori huku mtoto huyo akipewa jina la Latifah a.k.a Princes Tifah au Queen Latifah.
GPL

Post a Comment

15 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. labda ameona au ameng'amua kwamba mtoto si wake. Hata hivyo wahenga walisema kitanda haikizai haramu

    ReplyDelete
  2. Dai anasahau anapowatuka maa x wake anapopata demu mwingine, akijibiwa inakuwa nongwa kwake. alee tuu mengine yatajitokeza baadae. kwani lisemalo lipo!

    ReplyDelete
  3. yeye anapowadharau kwa maneno ya kejeli wanawake alotembea nao ni sawa, wakimjibu analia lia kama kuchu. akafanye dna kwanza ndo atakapolia zaidi majibu yakitoka.

    ReplyDelete
  4. ATAILA ZAIDI MAJIBU YA DNA YAKITOKA. AACHE KIKI ZA TANDALE.

    ReplyDelete
  5. mkeo? na Ivan asemeje?? by tha way ushamuadhinia mtoto au ndo mambo ya kutiwa maji kanisani, maana ulizini na bi kizee na dini kila mtu na yake.

    ReplyDelete
  6. Domo huna mke hapo usijidanganye, ulikuwa unazini tuu, kapime dna kwanza wacha ujinga majnuni.

    ReplyDelete
  7. Nyie watu acheni kuuliza mtoto wake mtoto wake..kwani Dai na familia yao wote ndo wenye shauku ya kujuwa mtoto wake au laa..mtoto anapimwa kabla hajazaliwa kama ni damu ya Dai..mpaka Dai analia inamaana mtoto MaanshaAllah ni wake..hata hivyo Zari si mjinga kiasi hicho hawezi kumpachikia Dai mtoto aso kuwa wake kwani anajuwa atapimwa na kugundulika na kuwa aibu..She could tell her boyfriend before hand kuwa mtoto si wa kwako ili isiwe aibu...Mabrouk Naseeb..Nimefurahi kusikia Zari ni mkeo kwa hiyo ni mtoto wa halali..Allah Akukuzieni salama salimin na Awakinge na kila la shari..Don't listen to wa roho za kwa nin..ni mi sis wako London

    ReplyDelete
  8. Angekuwa President kweli angezalia Trauma Centre.
    Akome kupakazia wenzake name yeye
    Ovyooooo. We ndo was mwanzo! Ulicheat toka uko wema kama kweli mtoto wako

    ReplyDelete
  9. wabongo acheni wivuwaki toto

    ReplyDelete
  10. mkewe alimuoa kanisani au xxxx. acha kumzidishia dhambi wewe Anony 1.10. Nyie ndo wale wale msomjua baba yenu mzazi.

    ReplyDelete
  11. sijawahi ona watu kuwa na chuki za kijinga kama hapa bongo, sasa mtoto awe wake asiwe wake nyie inawahusu nn

    ReplyDelete
  12. DNA please Chibuje unajua kwamba mwanamke akitembea na wanaume ndani ya masaa 72 kujua baba wa mtoto ni kazi. Je Halima kimwana hamu kuta Zari na Ivan chumbani hadi ikawa ugomvi mkubwa Zari Ali yoyos siri Zari alimchukia kufa. So DNA ni mhimu Sana

    ReplyDelete
  13. Siyo swala la wivu Chibu kapatikana hahahaha Zari mjanja sana

    ReplyDelete
    Replies
    1. mama ndio ajuaye mtoto ni wa nani...

      Delete
  14. DNA nyie mna uhakika na baba zenu mwacheni Dai afurahe wake mwana hahaaaa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad