Mwana FA anaamini kuwa nchi zinazotumia lugha ya Kiswahili zikiweza kutengeneza soko moja la muziki wa wasanii wanaoimba kwa Kiswahili, zitatengeneza himaya yenye nguvu kuwazidi Wanaijeria.
Akiongea na Global TV, FA amesema wingi wa watu nchini Nigeria ni sababu kubwa ya kuwa na kiwanda kikubwa cha muziki barani Afrika.
“Wanajeria population yao ni watu milioni 180,” amesema FA. “Hata wakiamua kuimbia watu wao peke yao bado wana uwezo mkubwa wa kutengeneza pesa kuliko sisi ambao tuko milioni 48. Ndio maana nikasema kama tungeconcentrate kuwafanya swahili speakers wakawa soko letu, Kenya tukalifanya soko letu, Uganda soko letu, Burundi soko letu, sehemu ya Congo wanakozungumza Kiswahili, Rwanda, Burundi sehemu hiyo yote, tukafanya soko moja, tungekuwa na population kubwa kuliko Wanijeria, pengine tungeweza kuanzia hapo,” ameongeza rapper huyo.
“Sarkodie ni bonge la rapper, lakini anachanganya lugha, wakati mwingine namsikiliza lakini simuelewi hata anasema nini, lakini mimi naona raha tu kumsikiliza. Lakini kuna Kiingereza ndani yake na lugha za kwao. Hapa ukitaka ugombane na Watanzania, anza kuimba Kiingereza, hamna mtu atasikiliza wimbo wako.”
Mwana FA Apendekeza Njia ya Kutengeneza soko imara la Muziki Kuwazidi Wanaijeria
0
August 09, 2015
Tags