Hali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mwanza si shwali baada ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mkuyuni, Charles Lugo (Fashion), na wanachama zaidi ya 100 kujiunga na Chama cha Wananchi (CUF).
Tukio hilo linakuja ikiwa ni mwendelezo wa wimbi la wanachama wa CCM kuhamia upinzani hususani Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).
Diwani na wanachama hao kutoka matawi mbalimbali ya CCM, walieleza chanzo na sababu za kutimkia CUF, kuwa chama hicho kimetawaliwa na vitendo vya rushwa, chuki na undugu kitendo kinachosababisha kukosekana kwa demokrasia ya kweli.
Wamesema viongozi wa CCM kuanzia ngazi ya chini hadi Taifa, wamekuwa wakitumia rushwa kushika madaraka na kusababisha watu ambao ni wazalendo wenye nia dhabiti ya kuwatumikia wananchi kukosa haki hiyo.
Wanachama hao wakiongozwa na diwani huyo, wamepokelewa na Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa CUF, Karume Jeremiah, wakati wa mkutano wa hadhara uliofanyika eneo la Chakechake, Nyamagana.
Akizungumzia tamko la wao kujiengua CCM na kujiunga CUF, Fashion amesema wamefikia hatua hiyo kutokana na kuchoshwa na vitendo alivyodai vya rushwa kwenye uchaguzi, uonevu na hila na kukosekana kwa demokrasia.
“Tumetoka CCM kwa sababu ya wizi wa waziwazi katika uchaguzi, wanafunga magori ya mkono watu wakiwa wanaona, sasa tumekuja huku upinzani. Lazima tuwashughulikea mpaka waachane na wizi wao." Amesema Fashion.
Arusha Hali ni Mbaya Zaidi
Habari kutoka jijini Arusha zinaarifu kuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha, Mh Onesmo Nangole na Katibu Mwenezi wa CCM mkoa wa Arusha,Mh. Isack Joseph wamejiuzulu nafasi zao zote leo na kujiunga na chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA).
Wakiongea na waandishi wa habari leo, viongozi hao wamemtaka Katibu Mkuu wa CCM, Mh Kinana kuacha mara moja siasa za matusi za kuwaita Makapi wanachama ambao wamekuwa wakijiunga na vyama vya upinzani.
Ikumbukwe kuwa,zaidi ya wanachama mia 300 waliokuwa chama cha CCM kutoka jamii ya kifugaji katika kata ya Engaruka wilaya ya Monduli juzi walizichoma kadi zao za CCM na kujiunga na CHADEMA .
Mbona bado sana lazima wanyoke mwaka huu!!!
ReplyDeleteWaende tu kikubwa kura ni siri ya mtu hao wote walio hamia cuf na chadema wakipiga kura wanaipigia ccm mtawajua si wanataka kuwafurahisha tu muone mnawafuasi kilakitu OCTEBER 26 MSIC WA MAGUFULI MTAUWEZA,,,,,,mtampa kashfa ya ufisadi kwasababu ya chama chake ila kiukweli kashfa hanaaaa,,,,,,
ReplyDeleteNi uongee utaisoma namba. We kataa jambo la ukweli.
ReplyDeleteKwa hiyo rushwa ipo ccm au huko wanaponunuliwa?
ReplyDeletePumbavu kabisa
Kwahiyo rushwa ipo ccm au huko wanaponunuliwa!!?
ReplyDeletePumbavu kabisa.