Mwenyekiti wa Wenyeviti CCM Taifa, Mgana Msindai Ahamia CHADEMA

Mhe Mgana Msinda  akiwasalimia  wajumbe  wa  Baraza  Kuu CHADEMA
****
Mwenyekiti wa wenyeviti wa CCM, Mgana Msindai jana alijiunga na Chadema na kutambulishwa katika mkutano wa Baraza Kuu la Chadema.

Mgana, ambaye aliwahi kuwa mbunge wa Iramba Mashariki (2000-2010) alitambulishwa pamoja na Mbunge wa Arumeru Magharibi (CCM), Goodluck Ole Medeye na ofisa mwandamizi wa chama hicho, Matson Chizii.

Makada hao wa CCM jana usiku waliambatana katika kikao hicho na aliyewahi kuwa waziri mkuu Edward Lowassa.
 
Habari zinasema kuna makada zaidi wa CCM watakaotambulishwa katika mkutano mkuu wa Chadema leo.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Imekuwa fashion kutafuta umaarufu wataingia waliomo na wasiokuwemo ili mradi vurugu mechi

    ReplyDelete
  2. Na bado mpaka watanyooka tu mwaka huu.

    ReplyDelete
  3. Huyo Msinda si juzi juzi kashika nafasi ya pili ktk kura za maoni CCM wajameni hata haya hawana alikuwa wapi kutafuta haki kabla ya kushindwa tamaa ya fisi itawatoa roho na mnaudanganya umma wa wa watanzania huruma hawana lini hawa wanasiasa njaa wataerevuka achilia mbali Magufuli jembe hata Iziraili mtoa roho za watu akitutawala hatutazibuka masikio kusoma sio hoja tatizo letu ni nafsi zimejaa kutu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad