Napata shida sana kujua dhamira ya Mh Lowassa kwa Taifa la Tanzania na katika Siasa za Tanzania

1: Aliangaika sana kwa hali na mali kwa kutumia Pesa nyingi sana ndani ya CCM ili siku moja aweze kuwa Rais.

2: Kama angefanikiwa ndani ya CCM angetawala nchi kwa kufuata Sera za CCM na kudumisha Muungano wa Tanzania.

3: Leo hii amewakana CCM kwa kusema 'CCM si baba yangu wala mama yangu' kwa kutumia Pesa nyingi saana na kuhamia CHADEMA. Kama leo hii CCM imekanwa basi na wewe ukiwa kama mwanachama wa CHADEMA/UKAWA au Mwananchi wa kawaida wa Tanzania basi na wewe jiandae kukanwa wakati wowote.

4: Ametumia Pesa nyingi sana kuwashawishi CHADEMA na wengine (kuwanunua) ili awe mgombea pekee wa Urais kupitia UKAWA. Hii inaonesha wazi wazi ni jinsi gani Mh Lowassa hasivyopenda Demokrasia ya kweli na kupenda Uditekta kwa chochote atakacho.

5: Hivi Sasa amehamia CHADEMA kwa matumaini kwamba atashinda Urais na kama akifanikiwa basi atakuja kutawala nchi kwa kutumia sera za CHADEMA/UKAWA na kuvunja Muungano wa Tanzania na kuweka Serikali tatu.

Nikiwa kama Mwananchi nisiye na Chama chochote cha Siasa hapa Tanzania, napata shida saana kujua dhamira ya Mh Lowassa katika Siasa za Tanzania, napata shida sana kujua dhamira yake ndani ya Tanzania kitu ambacho kinanifanya KAMWE siwezi kumuamini chochote asemacho kuhusu swala lolote ndani ya Tanzania, kitu ambacho kinanifanya kutoamini chochote wasemacho CHADEMA/UKAWA maana kama wanaweza kununuliwa kwa mabilioni machache basi ata rasilimali za nchi na Serikali yao siku wakishika madaraka inaweza kununuliwa na Mataifa ya nje kwa pesa ndogo sana.

Kwa kutumia uzoefu wangu wa kutambua watu, Vitu vyote afanyavyo na matendo yake nayaona ni kama mchezo wa kuigiza and its too Good to be true haswa haswa sura yake ukiiangalia kwa makini sana you will see theres something fishy going on.

Kama kweli anauchukia Umasikini na anauchukia umasikini wa Watanzania basi katika mabilioni aliyoyapoteza kwenye Kampeni za kutaka kuwa Rais kupitia tiketi ya CCM na mpaka sasa CHADEMA/UKAWA basi kwanini asingetoa kiasi kidogo kwa Wananchi wa Tanzania na kuwasaidia??!

Je Mh Lowassa una dhamira gani ndani ya Tanzania, Je ni nani anayekutumia kuusaka Urais kwa namna hiyo?? Kwa malengo gani haswa??!

Watanzania, CHADEMA/UKAWA na vyama vyote vingine vya Siasa nchini muogopeni Mh Lowassa zaidi ya Ukoma, CCM wameona basi nanyi kuweni makini sana.

Asanteni.

Maoni Binafsi Toka Kwa Infinite wa JF

Post a Comment

18 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Subir achaguliwe mtakiona cha mtema kuni na hiyo amani muko nayo mutajuta badae. Neno ningelijua huja wakat kila kitu kilisha haribik na nyiny mutasem hivyo baada ya kumchagua huyo eti Ngoyai.

    ReplyDelete
  2. Ni kweli kabisa. Huu uraisi wa kinguvu sijui ana nia gani na sisi Watanzania. Hata mi sipati jibu. Mbona analazimisha sana kuwa raisi wetu? Kuna nini nyuma ya pazia?

    ReplyDelete
  3. Inashangaza sana CHADEMA kupokea mbuzi ndani ya gunia,kwa lengo la kuingia Ikulu.
    Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  4. Francis pongezi haya ndo maneno yanapashwa kumuingia mtu akilini kufafanua na kuuweka wazi ukweli sio ushabiki wa kupenda mtu chake hata kama kinanuka uvundo atakwambia laa kinanukia marashi tena kwa shari na ugomvi

    ReplyDelete
  5. Hayo ni maoni yako na wana ccm wenzako so hatubaiswi na wanafiki mnaonganagania kuendelea kuwanyo wanyonge!

    ReplyDelete
  6. Weeeee utakua n kibaraka wa ccm na hata ufanyeje huewz kumchafua mh.Lowassa atashnda tuu ht mkimpaka matope lowassa is the best na ww tuseme umepewa mamilion na ccm kumchafua Mh Lowasa p***Mb weee

    ReplyDelete
  7. Karudisha kadi ya CCM?

    ReplyDelete
  8. Hata mimi binasfi najiuliza swali kama hilo, kama dhamira yake yake kweli

    ReplyDelete
  9. Ukweli Edo anatamani kuingia ikulu tuuuuuuuuuuuuuuuuuu,hata kama ni kwa siku moja ili mradi aonje Ikulu akiwa Rais.
    IKULU NI MAHALI PATAKATIFU,PAOGOPENI KAMA HAMNA DHAMIRA NZURI.

    ReplyDelete
  10. wewe nimnafiki sana,tena jibwa Koko.Unaweza kuthibitisha kuwa ametumia hela?
    Acha unafiki .huwezi kuwa mtanzania huku huna chama.unaongea nini.CCM imepoteza dira.Miaka 50 yakushika dola wanatuambia watatatua matatizo ya mamalishe na wamachinga.dah wewe mshamba.vyema usitujazie upumbavu.Huna data hunalakuongea.

    ReplyDelete
  11. we acha kunibania.comment zangu upost.we mshamba nini.au ccm wasio na dira

    ReplyDelete
  12. sawa tu ukisema huna chama chochote si maoni yako huru? wala hatuhitaji hotuba za kutuambia tumwogope el.. kama ukoma ! uwe mtafiti kidogo kwani si lazima ujiulize maswali ambayo yanakidhana na uwezo wako wa kuchambua mambo!. ukisema el ametumia fedha kuhonga kwanini msimkamate na TAKUKURU ipo?. wewe kwani unajua yaliyo moyoni mwake? kuna siku yoyote walikushirikisha yeye na Mh kabisa walichokuwa wamenia siku zote za maisha yao?. acha siasa chafu na taka .....Jana mlisema makapi.... sasa Makamu.... Mtoto wa mkulima..... mzee wa kiluvya, mwenye ng'ombe wengi wa kisasa; wote nao ni makapi? unachotakiwa kufanya ni kuwa mpole, ukiendelea kuomba Mungu nchi iwe na amani.... kama kura za maoni tu wizi mtupu ! Je wakati wa uchaguzi mkuu octoba si ndio kabisa? mimi nasema hadanganyiki mtu....na mtu yeyote asitufundishe tunakotaka kwenda na kufika....wengi wataamua wenyewe wanakotaka kuelekea... maana mwenye macho haambiwi tazama....!

    ReplyDelete
  13. Hata mimi ile sura yake sijaielewa bado, analoliongea mdomoni halifanani na sura yake, yaani amekaa kikatili au kisasi sijui nisemeje, lakini HANA FURAHA wala AMANI ya moyo hata kidogo, labda mpaka awe rais!!

    ReplyDelete
  14. Katika watu wanao nishangaza ni Prof. Lipumba, pamoja na elimu yako yote anazidiwa kete na DJ Mbowe..... kawaingiza chaka bovu CUF, afadhali NCCR wao chama chao sio kikubwa sana. DJ Mbowe ni mjanja mno, kaona Zanzibar hawana wafuasi ndio akabanisha kwa CUF, na wao bila kufikiria wakaingia mkenge......amakweli WAJINGA NDIO WALIWAO!!

    ReplyDelete
  15. Na lazima huyo mbowe aingie ikulu na UKAWA wote wewe unamuita mbowe dj lazima utakutakwa mototo wa mjumbe wa kumi kumi au akili zako zipo unapotolea haja kubwa.

    ReplyDelete
  16. Rais wetu awe na moyo wa kuingoza nchi yetu katika haki,kuondokana na kero za afya,barabara,usalama uwepo usiku na mchana,mali ghafi za nchi zisaidie wananchi ,ajira,,maji,elimu,na kuwa na viwanda vyetu sio kutegemea kila kitu kutoka nje haswa nguo,kuongeza uzalishaji,tupate Rais mzalendo mimi sijali chama najali maslahi ya nchi ,ya Tanzania na watu wake,nchi yetu isiwe kama shamba la babu,nchi yetu itasimama baada ya marais 3 kuanzia sasa,bado sasa tupo kwenye mpito ,na watu wengi hawajui wanacho taka kifanyike katika taifa letu,Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  17. Rais wetu awe na moyo wa kuingoza nchi yetu katika haki,kuondokana na kero za afya,barabara,usalama uwepo usiku na mchana,mali ghafi za nchi zisaidie wananchi ,ajira,,maji,elimu,na kuwa na viwanda vyetu sio kutegemea kila kitu kutoka nje haswa nguo,kuongeza uzalishaji,tupate Rais mzalendo mimi sijali chama najali maslahi ya nchi ,ya Tanzania na watu wake,nchi yetu isiwe kama shamba la babu,nchi yetu itasimama baada ya marais 3 kuanzia sasa,bado sasa tupo kwenye mpito ,na watu wengi hawajui wanacho taka kifanyike katika taifa letu,Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete
  18. Rais wetu awe na moyo wa kuingoza nchi yetu katika haki,kuondokana na kero za afya,barabara,usalama uwepo usiku na mchana,mali ghafi za nchi zisaidie wananchi ,ajira,,maji,elimu,na kuwa na viwanda vyetu sio kutegemea kila kitu kutoka nje haswa nguo,kuongeza uzalishaji,tupate Rais mzalendo mimi sijali chama najali maslahi ya nchi ,ya Tanzania na watu wake,nchi yetu isiwe kama shamba la babu,nchi yetu itasimama baada ya marais 3 kuanzia sasa,bado sasa tupo kwenye mpito ,na watu wengi hawajui wanacho taka kifanyike katika taifa letu,Mungu ibariki Tanzania.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad