Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Kailima Ramadhan (kushoto), akimkabidhi Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Benedict Wakulyamba orodha ya majina 52,078 ya watu waliojiandika katika daftari la kudumu la wapiga kura kwa mfumo wa BVR zaidi ya mara mbili Dar es Salaam jana, kwa ajili ya uchunguzi na baadae hatua za kisheria zichukuliwe kwa wahusika.
Picha hii ni baadhi ya watu waliojiandikisha zaidi ya mara mbili katika daftari hilo.
Picha hii ni baadhi ya watu waliojiandikisha zaidi ya mara mbili katika daftari hilo.
TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imelikabidhi jeshi la polisi orodha ya majina ya watu zaidi ya 52,000 ambao wamebainika kujiandikisha zaidi ya mara moja kwenye daftari la kupigia kura kwa mfumo wa Biometric Voters Registration (BVR), akiwemo Diwani wa Kata ya Kimara, Pascal Manota (Chadema).
Idadi hiyo ilibainishwa Dar es Salaam jana na Mkurugenzi wa NEC, Ramadhan Kailima wakati wa ziara na waandishi wa habari katika bohari ya utayarishaji wa vitambulisho vya kupigia kura kwa mfumo wa BVR
Wabongo walivyokuwa walivyozoea maisha ya RUSHWA na MAZABE wanafikiria hizo machine mtu anaweza ku cheat kumbe wanajipiga vitanzi wao wenyewe na hiyo bado mtawakamata wapiga kura wote safari hii hapo hakuna kugushi kura hii ni dunia ya technology sio kuandika katika madaftari kama mlivyozoea ili ugushi kiurahisi kazi mnayo watu wa kugushi mmeukwaa mnanaa
ReplyDeletembona wa ccm hawawaoneshi walio cheat?
ReplyDelete