Nisha Akana Kukamatwa na Madawa ya Kulevya

Msanii wa tasnia ya Bongo movie nchini Salama Jabu alimaarufu kama Nisha ameibuka na kuwatoa hofu watanzania pamoja na mashabiki wake kuwa hajakamatwa na madawa ya kulevya kama ambavyo taarifa zinavyosambaza katika mitandano ya kijamii.

Nisha kwa sasa yupo nchini China amekanusha taarifa hizo kupitia ukurasa wake wa Instagram baaada ya kuona akiulizwa sana na kupewa pole na watu wake wa karibu. Nisha amesema huwa si kawaida yake kujibu au kutolea ufafanuzi mambo ambayo huwa ni uzushi lakini kutokana na uzito wa uzushi huu wa kukamatwa na madawa ya kulevya ilibidi atoe ufafanuzi huu.


"Naomba leo niweke wazi hili suala lililoandikwa na kusambaa kuwa nimekamatwa China na madawa, huwa napenda kupuuzia vitu ila wacha niongee leo ili nisiwape watu presha na maswali mengi na kuwaweka njia panda, mimi sijakamatwa, sijawahi kukamatwa na wala sitaweza kukamatwa kwa ajili ya ujinga kama huo wa madawa ya kulevya kwanza siyapendi lakini pili hata niwe masikini vipi siwezi kujiingiza kwenye janga hilo," alisema Nisha.


Mbali na hilo Nisha ameeleza jambo ambalo limemtokea alipofika nchini China katika uwanja wa ndege na kusema kuwa kutokana na nchini za Afrika hususani Nigeria na Tanzania kuhusishwa sana na biashara za madawa ya kulevya hivyo kumekuwa na ulinzi mkali jambo ambalo lilimfanya akagulie kwa zaidi ya saa tatu.

"Kilichotokea ni hiki kutokana na Watanzania kuharibu sana na scandals za kukamatwa na madawa ya kulevya, (wengi mnalijua hilo) ukiwa unavuka border ukionekana tu passport yako ni ya Tanzania basi unasachiwa sana. Ni kweli walinisachi kwa zaidi ya masaa matatu. Hilo kwa Watanzania wanaovuka kwenda Hong Kong nadhani mmenielewa, si mimi tu yoyote Mtanzania au Wanigeria au taifa lolote lenye historia ya nchi yao kukamatwa na unga lazima shughuli ikupate lakini hawajanikuta na kitu I'm ok," aliongeza Nisha.

Nisha amewataka baadhi ya waandishi wa mitandao ya kijamii zikiwepo website pamoja na blogs mbalimbali kuwa na uhakika na taarifa mbalimbali wanazoziweka ili kuepusha kusambaza uzushi ambao unaweza kuleta mshtuko kwa watu wengine na kusababisha matatizo.

EATV.TV
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad