Polisi Wazuia Msafara wa LOWASSA Kushiriki Mazishi ya Mzee Kisumo

Polisi  wakiwa  tayari  kwa  lolote  baada  ya  kuzuia  msafara  wa  LOWASSA
Polisi mjini Mwanga, mkoani Kilimanjaro umezuia msafara wa mgombea urais kupitia Chadema, Edward Lowassa uliokuwa unaelekea Usangi kuhudhuria mazishi ya kada wa CCM, Peter Kisumo.

Vyanzo vya kuaminika toka mjini Mwanga vinasema, polisi walizuia msafara huo kutokana na kujumuisha idadi kubwa ya magari ya viongozi waandamizi wa Ukawa na wabunge wanaounda umoja huo jambo ambalo polisi hawakuafiki.

Taarifa zinasema, tukio hilo lililotokea katikati ya Mwanga na Usangi lilizusha mjadala wa zaidi ya dakika 30, polisi wakitaka Lowassa aende mazishini peke yake huku magari mengine yaliyoambatana naye yarejee yalikotoka jambo ambalo halikuafikiwa na mwanasiasa huyo.

Baada ya polisi kusisitiza kutoruhusu msafara mzima uende mazishini mgombea huyo aliamua yeye na maofisa wengine alioambatana nao kurudi Mwanga akisisitiza asingeweza kwenda peke yake akiwaacha watu aliambatana nao.


Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. moto chini!!!!hawapendi attention unayoipata edo ,lazima watakaa its matter of time.

    ReplyDelete
  2. Huko Lindi kwa nini hawakumzuia makufuli? Lakini yote ngoja uone kwamba wananchi wote wana imani na Lowassa: - ccm wote, hUENDA HATA MAKUFULI ANA IMANI NA LOWASSA
    https://youtu.be/f83rfPiPHgA

    ReplyDelete
  3. DAWA NI HIYO TU WASIANDAMANE, WATATUPIGA BAO LA ASUBUHI BURE.... BAO LETU LA MKONO HALITAFUA DAFU....ZUIAAAA MAANDAMANOOOOOOOO

    ReplyDelete
  4. kuweni na akili hajazuiwa kwenda msibani amezuiwa kuwa na msafara wa maandamano penye ukweli semeni ukweli jamani kama alikua na nia ya kwenda msibani angewambia hao wa boda warudi yeye aende asijikweze asubi kukweza ajikwezae hushushwa ajishushaye hukwezwa hiymani ni msiba hafu nyakati hizi nizauchaguz watanzania tuwe makini sio kila kitu ushabiki

    ReplyDelete
  5. Hao ukawa wanapenda sifa tu, kwani kabla hajajiunga nao alikuwa haendi mazikoni, mpaka waende msafara mzima magari madogo 40 na pikipiki 300!! inahusu.........PIGENI TU!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad