Kamanda Kova |
Sambamba na kukamatwa watu hao, polisi pia imekamata bunduki 10, risasi 300 na bomu moja la mkono.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna, Suleiman Kova ametangaza leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.
Kova aliongeza kuwa watuhumiwa hao pia wanajihusisha na kutoa mafunzo ya kigaidi.
‘’ Hawa tumefanikiwa kuwakamata, tunawaita majambazi au magaidi kwa kuwa licha ya kufanya ujambazi pia wanajihusisha na kutoa mafunzo ya kigaidi katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Lindi,’’ alisema Kamanda Kova.
Amesema kuwa polisi wamefanikiwa kuwanasa watu hao ikiwa ni operesheni endelevu ya kuwasaka wahalifu wote wanaovunja amani hapa nchini.
Ameeleza kuwa baadhi ya silaha zilikamatwa zikiwa zimefichwa maeneo ya Mkuranga mkoani Pwani ambapo baadhi ya silaha hizo tayari zilikuwa zimeshapata kutu.
Kamanda Kova amesisitiza kuwa polisi wanaendelea na upelelezi na ukishakamilika watuhumiwa hao watachukuliwa hatua za kisheria ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.