Rais Kikwete Amjibu Lowassa 'Kimtindo'.

Rais Jakaya Kikwete, amefunguka na kusema hatishwi wala hashtushwi na maneno ya watu wanaosema serikali yake kwa miaka 10 haijafanya kitu.

Badala yake amesema kitakachomshtusha ni taarifa zozote za uchochezi kwa kutumia kivuli cha dini ama ukabila kwa kuwa vitu hivyo ni hatari na vinaweza kuliingiza Taifa katika machafuko.

Rais Kikwete aliyasema hayo jijini Dar es Salaam jana alipotembelea Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora  (THBUB) na kuzungumza na watumishi wake ambao walitumia nafasi hiyo kumuaga.

Alisema watu wanaobeza mafanikio ya serikali yake hawezi kuhangaika nao kwa kuwa anajua kuna mafanikio mengi yamepatikana katika kipindi cha miaka 10 mpaka sasa na wanao uhuru na kusema chochote wanachotaka.

“Kuna watu wanasema sana serikali yangu haijafanya chochote, lakini hawa sitahangaika nao kwa kuwa najua kuna mafanikio mengi yamefanyika katika uongozi wangu,” alisema  Rais Kikwete.

Alisema mtu atakayehangaika naye ni yule atakayetoa kauli za kuashiria uchochezi kwa kutumia dini na ukabila kwa kuwa vitu hivi ni hatari kwa amani ya nchi na kwamba kwa hilo atakuwa mkali.

“Kuna uhuru wa kutoa maoni na kama kuna mtu anataka kusema au kukosoa serikali yangu, mimi sina tatizo na yeye aende hata pale Jangwani aseme siku nzima sina tatizo naye, lakini atakayejaribu kuleta uchochezi kwa kutumia dini na ukabila, huyo tutashughulika naye," alisema.

Ingawa Rais Kikwete hakumtaja mtu yeyote, Julai 29, mwaka huu, Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, anayegombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), alisema kuwa Serikali ya Rais Kikwete imeshindwa kuwapatia wananchi maendeleo.

Lowassa baada ya kuchukua fomu za kuwania urais, akiwahutubia wafuasi wa Chadema na wananchi katika ofisi za chama hicho mtaa wa Ufipa, Kinondoni, Dar es Salaam pamoja na mambo mengine, alisema Serikali ya Rais Kikwete imeshindwa kusimamia uchumi kiasi cha bei za vitu kupanda kila uchao vikiwamo vibiriti, mafuta na vyakula.

Katika ziara zake za kutafuta wadhamini kwenye mikoa ya Mwanza, Arusha, Mbeya na Zamzibar, Lowassa alirudia kauli hiyo na kusema kuwa Serikali ya Awamu ya Tatu chini ya Rais Benjamin Mkapa, ilisimamia vizuri uchumi kuliko Serikali ya Awamu ya Nne.

Post a Comment

12 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. HAWA WASHIKAJI BAADA YA KUTOSANA SASA WANAANZA KUPONDANA

    ReplyDelete
  2. MHESHIMIWA RAIS WETU KWA UTAWALA WAKO WA MIAKA 10 UMECHUKUA FEDHA TRILLION NGAPI ZA KODI ZETU KUFANYIA KAZI ZETU ULIZOPASWA KUFANYA HIZI PESA HAZIKUA ZAKO UMETUANGUSHA SANA UMETUIBIA SANA HEBU NJOO MUHIMBILI USHUHUDIE WAGONJWA WANALALA MZUNGU WA NNE TWENDE MIKOANI UONE WATOTO WANASOMA CHINI YA MITI WAMEKALIA MAWE YAANI

    ReplyDelete
  3. Yani kwa hilo Ni kweli kabisa,uchumi umeanguka ukilinganisha na mkapa awamu yake. It's a shame, viongozi aliowachagua km SI mtoto WA best yake basi shemeji, au ndugu WA ndugu yake, madawa ya kulevya kila kona ya jiji

    ReplyDelete
  4. Usisahau katika uteuzi wake mwingi Ridhwani naye aliteua Mama salma naye aliteua kwa ujumla Yeye mama salma aliteua MABALOZI NA WAKUU WA MIKOA Na Ridhwani Mawaziri na Manaibu.Eeee Mungu wetu tumedhalilika sana.OOO MHE LOWASSA TUNAONA KAMA UNACHELEWA VILE

    ReplyDelete
  5. Umekwiba sana sisi hatutokubali ooh eti ana kinga hashitakiwi.ukisha achia tuu ngazi sheria itaanza`kuchukua mkondo wake.ni jela ni jela ni rumande ni rumande ``````````````````

    ReplyDelete
  6. Tunaomba ukae kimya kikwete maana kwa sasa kila neno lako ukisema lina hila ndani,uongo,ulaghai,upotoshaji,mbinu mkakati zisizo na mashiko tena.panga kujifunza kukaa kimya umebakiza muda mfupi sana.una miezi miwili ya kukanyaga zuria jekundu,ya kupigiwa saluti kisha urudi Msoga ukapambane na panya buku kule ni wengi sana.

    ReplyDelete
  7. kwli tumeona mheshimiwa rais watu wana njaa na umasikini hospitali mbovu wwe ukiwa ndani ya ndegw special unazunguka dunia leo canada kesho australia,ukiwaacha wananchi wako wakiwa ktk hali ngumu wanakufa kutokana hakuna dawa za dola ishirini wwe ukiwa angani unaunguza mafuta ya milioni 50 kweli ur best abuser of tanzanian economy..

    ReplyDelete
  8. kwli tumeona mheshimiwa rais watu wana njaa na umasikini hospitali mbovu wwe ukiwa ndani ya ndegw special unazunguka dunia leo canada kesho australia,ukiwaacha wananchi wako wakiwa ktk hali ngumu wanakufa kutokana hakuna dawa za dola ishirini wwe ukiwa angani unaunguza mafuta ya milioni 50 kweli ur best abuser of tanzanian economy..

    ReplyDelete
  9. kwli tumeona mheshimiwa rais watu wana njaa na umasikini hospitali mbovu wwe ukiwa ndani ya ndegw special unazunguka dunia leo canada kesho australia,ukiwaacha wananchi wako wakiwa ktk hali ngumu wanakufa kutokana hakuna dawa za dola ishirini wwe ukiwa angani unaunguza mafuta ya milioni 50 kweli ur best abuser of tanzanian economy..

    ReplyDelete
  10. Kweli raisi wambie hao wanao kuponda jinsi miaka kumi ya uwongozi wako ulivyo let's uchumi mkubwa sana Wa taiga na ukafanya mambo mazuri makubwa sana kweli ccm tutashinda kwa kishindo kikuu man's tumefanya Hays hakika tutapita kwanza tumehimarisha umasikini vyakutosha wajinga wamefurahia I'll kuwa masikini Pili tumeboresha mastaa wetu kucheza uchi tatu tumeboresha sektaya afya kukosa dawa NNE tumeboresha kupata ajali nyingi sana za barabarani tank tumeboresha majambazi Wa kutosha kupora kwenye mabank sita tumeboresha kwa wing I mgao Wa umeme saba tumeboresha na kuwanenepesha watanzania halali kupata pesa za reachmund nane tuka waboresha tena kuwapatia pesa za eppa ili wazidi kujenga magorofa yao Tisa na zuri tumeboresha sekta ya kuua tembo na kuuza pembe za ndovu ulaya na kuwekeza mahela ya wajinga nje kumi na tamu linatia hamasa kabisa ccm kuchukua urais no uboreshaji mzuri na wakisasa nabwakuwaimarisha watanzania halali kabisa nikuwazawadia mapesa ya escrow kuminamoja naongezea katika pongezi zangu za miaka kumi nikupitisha sheria mbovu na kuwalipa wabunge mamilion ya asante Wa muda wawo hongera sana rais wangu na serekali yetu Nzuri ya ccm kutupa mambo hayo kuminamoja katika uwongozi wako ni mambo mazuri sana uliyo yafanya baba raid hakika magofuli utazidisha zaidi ukichaguliwa na wenye akili zilizo jaa vinyesi na wabagua makabila lakini sisi wajinga ngooo hatukupi iyo nafasi

    ReplyDelete
  11. Ukiiangalia sura yake tu machale yanakucheza kuwa huyo jamaa ni bomu mtu wa kutaka sana sifa kujiona kuwa amesoma sana mjanja sana mjuaji sana na kajilimbikizia mali nyingi sana ndani na nje ya nchi bila ya huruma kuwa watanzania wenzake wengi ni masikini mkatili wa kisirisiri I pray and hope that this'll be once and for all the end of CCM's era on power over humbleTanzanians

    ReplyDelete
  12. sisi na yeye safari hii baada ya octoba 25 ajue wazi kuwa tunampeleka kwanza katika mahakama zetu za ndani kwa matumizi mabaya ya ofisi,wizi mkubwa,ubadhirifu,unyanyasaji wa kijinsia,mauaji na utesaji wa waandishi wa habari,wizi wa nyala za serikali,ulanguzi wa madawa ya kulevya,rushwa ya ngono,uporaji wa mali za umma na,na,orodha bado inaendelea

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad