Ray C amedaiwa kuzua timbwili Jumapili hii katika hospitali ya Mwananyamala jijini Dat es Salaam baada ya kukosa huduma ya methadone.
Akizungumza na 255 ya XXL leo, mratibu mkuu wa hospitali ya Mwananyamala amethibitisha kutokea kwa tukio hilo huku akidai suala hilo tayari limeshafika polisi.
“Kuna muda maalum wa kugawa dawa, sasa ule muda unapoisha wanafunga,” amesema. “Sasa yule amekuja wakati muda umeshaisha sasa baada ya hapo akaamua kufanya fujo kwa huyo famasia ambaye anagawa dawa na kutoa lugha ambazo hazikuwa nzuri sana kwa huyo famasia. Hakuna mtu aliyeumia ila walisukuma geti la mlango ndio likagonga mlango,” aliongeza.
Hata hivyo Ray C ameiambia Bongo5 kuwa wahusika wa hospitali hiyo wanamfanyia makusudi.
“Mimi nimetoka kwenye madawa ya kulevya, ina maana nilipata matatizo na nilipoteza kila kitu, kwahiyo mimi nikipata mafuta ya elfu 30,000 ya kuweka kwenye gari yangu, elfu 30,000 kila siku ni pesa nyingi. Mimi sina kazi sasa ninavyofika mpaka hapa na nimetumia elfu 20,000 yangu halafu unaninyima dawa na nimemkuta famasia yupo ndani sio nimekuta kumefungwa, yupo ndani anatuona, ‘tunamuomba dada hatujakunywa dawa jana naomba utupatie,” amesema muimbaji huyo.
“Ni kweli wamenipeleka Oysterbay wananiambia mimi sijui nimefanya fujo, lakini sisi tulinyimwa dawa juzi Jumamosi na Jumapili ndio tukawa tunalalamikia tunataka dawa hawajui sisi tunaumia, wao wanacheka tu. Sasa na sisi ni binadamu na tulikuwa wengi na tuna hasira kwa sababu tunaumia, ndio akatoka kwa fujo na gari yake kwa kutuogopa sisi ndo akajikwaruza yeye mwenyewe. Sasa nashangaa polisi amenipeleka mimi. Halafu leo nimeenda pale sijui walitaka niende Segerea, ukiongea nao kidogo wanapaniki mtu katoka Mbagala na shilingi 1,000 ya nauli anakuja mpaka hapa jasho limamtoka mnaanza kumwambia hatukupi dawa?” amehoji.
Bongo5
MPUMBAFU ZENU SI MUWAPE DAWA SASA KM PALIKUWA WAZI SHIDA NINI?
ReplyDeleteWashenzi mwananyamala, hivi wangekua ndugu zenu mngewanyima,? Muyaone kwanza uuaji huo, watu wA hospital wana roho mbaya Sana.
ReplyDeleteJamanj someni tena. Kuna muda maalum wa kutoa dawa. Sasa alikiwa halijui hilo. Kama hafuati muda kwanini alalamikie penalti?
ReplyDelete