SBL Yapeleka Uzinduzi wa Tuzo za Ubora wa Thamani Kwa Wakazi wa Mwanza na Moshi



Mkazi wa Kona ya Bwiru jijini Mwanza Bw. Godfrey Urio akionyesha zawadi ya fedha taslim alizopokea mara baada ya kuibuka mshindi wa shindano la “Serengeti Masta” wakati wa kusherekea uzinduzi kampeni ya tuzo ya dhahabu ya ubora wa thamani ya Monde Selection ambapo kwa mwaka huu bia ya Serengeti Premium Lager toka SBL imejinyakulia medali tatu za dhahabu kutokana na ubora wake. (Kushoto) ni Meneja Masoko kwa wateja wa Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya Mwanza Bw. Denis Tairo na kulia ni mshereheshaji wa tukio hilo aliyefahamika kwa jina la MC Bebe. Hafla hiyo ambayo ilikua mahususi kwa wakazi wa kanda ya ziwa, ilifanyika katika baa ya “The dreams” iliyopo Kona ya Bwiru jijini Mwanza. Shindano la “Serengeti Masta” litafanyika Tanzania nzima na kuibua Mshindi mmoja kwa kila kanda na mwisho kumuibua wa taifa. Kauli mbiu ya kampeni hii ikiwa ni “TUNAIJUA BIA NA SERENGETI PREMIUM LAGER NDIO YENYEWE”.

Mdau wa bia ya Serengeti Premium Lager Ben Rockman akijaribu kuitambua bia ya Serengeti Premium Lager ,aliposhiriki kwenye shindano la kumtafuta “Serengeti Masta” wa baa ya “The dreams” ya jijini Mwanza wakati wa kusherekea uzinduzi kampeni ya tuzo ya dhahabu ya ubora wa thamani ya Monde Selection ambapo kwa mwaka huu bia ya Serengeti Premium Lager toka SBL imejinyakulia medali tatu za dhahabu kutokana na ubora wake. Kauli mbiu ya kampeni hii ikiwa ni “SERENGETI PREMIUM LAGER. TUNAIJUA BIA NA HII NDIO YENYEWE”.

 Wakazi wa Majengo mjini Moshi wakiburudika kushangilia Tuzo ya Dhahabu ya Monde waliyoipata kwa Bia ya Serengeti Premium Lager mwaka 2015 kutambua ubora wa kiwango cha juu wa iliyopata Bia ya Serengeti Premium Lager ambayo iliambatana na mashindano ya kutambua bia ya Serengeti Premium Lager mwishoni mwa wiki katika Baa ya Oriental.

Wafanyakazi wa kampuni ya Serengeti Brewieries Limited wakiwa na Mabalozi wa kinywaji hicho wakati wa kutambulisha Tuzo ya Dhahabu ya Monde inayotambulika kimataifa baada ya bia ya Serengeti Premium Lager kukidhi viwango vya juu vya ubora katika hafla iliyofanyika katika Baa ya Oriental ,Majengo mjini Moshi mwishoni mwa wiki.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad