Meneja Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti Bi. Anitha Msangi (Kushoto) pamoja na Meneja Mauzo wa bia ya Serengeti kanda ya Dar es salaam Bw. Godson Tezura wakizindua rasmi tuzo ya ubora wa thamani ya Monde Selection kwa wateja ambapo bia ya Serengeti Premium Lager toka SBL imetuzwa medali tatu za dhahabu mwaka huu kutoka viwanda vyake vyote vitatu; cha Dar es salaam, Mwanza na Moshi kwa 2015. Sherehe ya kuzinduaushindihuoilifanyikakatika baa ya Toroka Uje iliyopo Kimara jijini Dar es salaam.
Wafanyakazi wa Kampuni ya bia ya Serengeti wakiwa kwenye picha ya pamoja wakati wa kusherekea uzinduzi rasmi wa tuzo ya uborawathamaniya Monde Selection kwa wateja ambapo bia ya Serengeti Premium Lager imetuzwa medali ya dhahabu tatu kila moja kutoka katika viwanda vyake mwaka huu wa 2015. Sherehe ya kuzindua ushindi huo kwa wateja ilifanyika katika baa ya Toroka Uje iliyopo Kimara jijini Dar es salaam.
Meneja Masoko wa Kampuni ya bia ya Serengeti Bi. Anitha Msangi akifafanua jambo kwa waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa tuzo ya ubora wa thamani ya Monde Selection ambapo bia ya Serengeti Premium imetuzwa medali ya dhahabu tatu kutoka katika viwanda vyake kwa mwaka huu wa 2015 pamoja na kufafanua zaidi kuhusu shindano jipya la Serengeti Masta lilioanza kutimua vumbi katika baa ya Toroka Uje iliyopo Kimara jijini Dar.
Meneja Mauzo wa bia ya Serengeti Premium kanda ya Dar es salaam Bw. Godson Tezura akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ubora wa bia hiyo ambao ana amini ndio uliopelekea ushindi wa tuzo ya kimataifa ya Monde Selection ambapo kwa mwaka huu bia hiyo imetuzwa medali tatu za dhahabu katika viwanda vyake vyote vitatu. Bw. Tezura alisisitiza jinsi gani wateja wa wakubwa na wadogo watafaidika na kampeni hii ya Serengeti Masta.
Msimamizi wa Mauzo wa Kampuni ya bia ya Serengeti kanda ya Ubungo Bw. Victor Mhindi akikabidhi zawadi ya polo shirt pamoja na fedha taslim Tsh 50,000/= kwa mkazi wa Kimara mwisho Bi. Sharifa Shaaban mara baada ya mkazi huyo kuibuka mshindi wa shindano la “Serengeti Masta wa baa ya Toroka Uje” linaloendeshwa na SBL kupitia kinywaji chake cha Serengeti Premium wakati wa kusherekea uzinduzi wa tuzo ya ubora wa thamani ya Monde Selection ambapo bia ya hiyo imetuzwa medali tatu za dhahabu kwa mwaka huu wa 2015. Sherehe hiyo ilifanyika katika baa ya Toroka Uje iliyopo Kimara jijini Dar essalaam. Shindano hili litafanyika Tanzania nzima na kuibua Serengeti Masta wa kanda na mwisho wa taifa. Kauli mbiu ya kampeni ni TUNAIJUA BIA NA SERENGETI PREMIUMLAGER NDIO YENYEWE