Serikali Yakanusha Mabasi Yaendayo kasi DART ni ya KICHINA: Ni kiwanda kilicho Assemble Mabasi

Kuna upotoshaji wa Makusudi uliozagaa kwenye Mitandao ya Kijamii kuwa Mabasi Yaliyozinduliwa Tarehe 17/08/2015 kuwa.

1. Ati ni ya Kichina

2. Milango ya kushukia na kupandia Abiria Iko kushoto hivyo hayaendani na Miundombinu iliyojengwa.

HUO NI UZUSHI WENYE LENGO LA KUWAPOTOSHA WATANZANI WALIOCHOSHWA NA MSONGAMANO UNAOONGEZEKA SIKU HADI SIKU

TAARIFA SAHIHI KUTOKA KWENYE MAMLAKA HUSIKA HII HAPA:

1. Kiwanda Kilicho Assemble (Kuunganisha) Mabasi haya kinaitwa Golden Dragon cha China.

2. Aina ya Injini ni CUMMINS ya Marekani (USA)

3. Aina ya Giaboksi ni VOITH ya Ujerumani.

4. Mfumo wa Stelingi ni ZF ya Ujerumani.

5. Mgumo wa Difu ni kutoka Marekani (USA).

6. Aina ya Suspension (Za upepo) Air Suspension kutoka Marekani (USA).

7. Mfumo wa Breki ni WABCO

8. Aina za Mabasi ziko mbili. Articulated Mita kumi na nane almaarufu (Ikarusi) Kutoka Hungary zitakazopita kwenye barabara Maalumu za zege zilizojengwa na Mabaai ya mita kumi na mbili yanayoitwa (Feeder) Mabasi Mlisho yatakayotumia vituo vilivyoko nje ya mfumo Mfano Kituo cha Shekilango, Moroco Hotel, Mwanamboka na Magomeni Mapipa kuwapeleka na kuwaleta kwenye Mfumo.

9. Milango ya kupanda na kushukia Abiria ipo kulia na kushoto ili kukidhi mahitaji ndani na nje ya mfumo ambayo idadi yake ni Minne kila upande ila itatumika mitatu na mmoja niwa dharula kila upande.

10. Urefu kutoka ardhini kwa milango ya kushoto ya Basi ni Sentimita thelathini (30) ambayo hata mtoto anaweza kushuka bila msaada wa mtu mzima.

11. Urefu wa Milango ya kulia ni Sentimita tisini (90) sawa na urefu wa Platform za kila kituo cha DART unaomuwezesha hata mtu mwenye mahitaji maalum Kuingia na kutoka ndani ya basi bila msaada wa mtu.

12. Ndani ya basi kuna eneo la kukaa watu wenye Mahitaji maalum.
Walemavu, Wazee na Mama wajawazito.

13. Mfumo wa ulipaji nauli unafanyika vituoni kama ilivyo kwenye kivuko pale Kivukoni hivyo basi hili halina Kondokta. Makondakta wapo vituoni.

14. Muda wa Safari kutoka Kivukoni hadi kimara ni wastani wa dakika thelathini (30) ikihusisha muda wa kushusha na kupakia kwenye Vituo vya DART.

15. Ni marufuku kwa chombo ama mwananchi kutumia barabara maalum za Mabasi. Wananchi watumie maeneo yaliyotengwa maalum kulingana na mahitaji. Watumiaji wa Bodaboda wanatakiwa kupita kwenye barabara zinazotumiwa na magari ya Kawaida na siyo eneo lililotengwa kwa ajili ya Watembea kwa Miguu.

HIZI NDIZO TAARIFA MUBIMU NA RASMI KWA WATANZANIA

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Japokuwa sihipendi ccm imejaa wanga nampenda rais kikwete hongera sana baba kwa kutuachia dar IPO kama Londan rais mwingine abadili na mikoa mingine kwa miundo mbinu ya kisasa pia muheshimiwa rais ingekuwa serekali yako haijatuibia mapesa yetu bilashaka tanzania ingefanana na dubai lakini kwakuwa mnajali matumbo yenu na yawanenu kujilimbukizia mali ndani na nje ya nchi taifa linabaki la kizamani madini gesi.mafuta ciment samaki mbuga vinafanya nini miji isibadilike kiuzuri? Japokuwa mme tunyima maisha bora basi wekeni mazingira ya miji yetu ikae kisasa tafadhali es p

    ReplyDelete
  2. Serekali ya ccm huwa mna majabu sana nyie viumbe sijui mmezaliwa kuzimu ivi huwa mnasumbuliwa na utindio Wa ubongo au mmekuwa mkifanya mabadiliko mawili matatu ili tuone mmefanya kitu mlijenga uwanja mmoja Wa taifa mkaishia hapo vipi viwanja vingine Leo Barbara ya mwendokasi sawa Nzuri BT vipi baranara za mikoa mingine at a kiwango kizuri kabisa cha lami vipi viwanja vya ndege mikoa ya shinyanga na mingine yenye navyo na havina ubora mnampango gani wa kuwa na hosipital za kisasa mashule ya serekali ya kisasa ofisi za serekali nzur za kisasa nyumba nzuri xà polisi na walimu vipi Barabara za vijijini vipi umeme vijijini na kwenye mikoa lini mgao utaisha vipi ulinzi Wa tembo zetu vipi maboresho ya mbuga zetu zinazo pitiwa na magari makubwa vipi wazee lini mtawakumbuka vipi watoto Wa mitaani lini mtawatafutia vituo vya kuwatunza na kuwapa mafunzo ya elimu ya ufundi walau sikumoja wajiongoze wenyewe na kuinua uchumi Wa taifa lini kodi zitapungua ili watanzania wafurahie kufanya biashara na kuingiza kipato stahiki lini wakulima hawa talia lini wajasiriamali wadogo watafunguliwa njia za kushiriki kibiashara na mataifa mengine mnawaza kula tuu na kujipendekeza kwa tuvijimiundombinu viwili tu usoninpa dar wajinga sana nyinyi lini wapiga madebe stand watqpungua na kubaki watu wanao stahili hapo tu lini shirika la reli litaboreshwa na kuwa na teen za kisasa ziendazo.mikoani kupunguza maajali ya barabarani link njia zile za tren zitafukuliwa na vyuma chakavu kutolewa na kujengwa njia mpya nzuri na zakisasa nyie nikula tu nasi tunapenda sikumoja tuishi kama wenzutu wa ulaya miji mizuri nchi zinapendeza inatia hamasa kwakweli nyie miaka yote mnataka watu wabaki vilevile ndio mana watanzania wakienda kusoma ulaya wanazamia uko rekebisheni taifa muone kama kunamsomi atazamia ulaya tutabaki nyumbani na kuwekeza nyumbani kwani uzuri wa mazingira ya taifa ndio chanzo cha kuwa na wasomi wengi na wawekezaji wa ndani na hats wasio soma wstapata hajira zozote zitakazo endana na kipaji chake katika usanifu haohao waliowekeza ulaya watarudi kuwekeza nyumbani vijana badala ya kukaa stand watabeba hata mabox kwenye viwanda vya watanzania wenzao na watapata kiinua mgongo na hamtasikia mslalamiko hayo ndio maisha bora watanxania tunayataka tumechokakuishi kwenye nchi iliyojaa madimbwi ya Maji machafu Barbara za mashimo viwanja vya vibovu vya michezo basi ya kuanguka kila kukicha umeme Wa manati madawa ya kuunga mstari hosipitalini watukufa kisa ukosefu wa huduma nzuri ukosefu wa vitendea kazi mashuleni elimu mbovu polisi Wa kichama ambao mustakabali Wamtanzania wawo kurusha mabomu wanavyojisikia tu nchi isiyokuwa nahaki mahakamani mpaka rushwa ndio upewe haki nchi iliyo has rushes mpaka kwenye unyayo Wa miguu nchi iliyojaa umasikiniwa kutisha kisa kubananishwa kukatwa makodi katika kila kitu eti kulipa madeni ya taifa ukupesa wale ccm watanzania ndio tuwajibishwe kwa uwovu wenu tumechoka na tanzania ya leo tunataka taiga jipya linalo jitambua tunahitaji viongozi wanao kwrnda namabadiliko ya dunia ya leo sio ya nyerere tunahitaji taifa lenylenyi mainjinia madaktari walimu polisi safi jeshi safi tunahitaji taiga LA wachapakazi sio wazururaji aka ombaomba mitaani hatutaki taifalwacheza uchi taifa la madàwa ya kulevya tunahitaji taifa jipya

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad