STAA wa uchekeshaji na filamu Bongo, Steve Mengere ‘Steve Nyerere’ amefungukia madai ya kujiondoa Chama Cha Mapinduzi na kujiunga na umoja wa UKAWA akisema kushindwa kwake katika kura za maoni hakuwezi kuondoa heshima yake kwa Mwenyekiti wake, Jakaya Kikwete.
Akizungumza na gazeti hili juzi, Steve alisema Rais Kikwete amefanya mambo mengi sana kwa wasanii, kiasi kwamba ni mtu asiye na hisani pekee anaweza kuhama CCM kwa sababu ya kushindwa katika kura za maoni au ushawishi wa namna yoyote.
“Kikwete na CCM wamefanya mambo makubwa sana kwa wasanii, leo unaniambia mimi nihamie Ukawa, hivi wakati Lowassa (Edward, mgombea wa Ukawa) alipokuwa waziri mkuu aliwafanyia nini wasanii? Mimi kushika nafasi ya tano kwenye kura za maoni ni ushindi kwangu, kama ilivyo kwa Wema (Sepetu) kushika nafasi ya tano ni ushindi, kwa nini tuhame?” alisema msanii huyo.
Steve alitoa kauli hiyo kufuatia swali aliloulizwa kutokana na uvumi kuwa yeye na wenzake walikuwa mbioni kujiunga na Ukawa baada ya kushindwa kwenye kura za maoni za CCM hivi karibuni.
Chanzo: GPL
Really??nani anataka huyu kauzu wa kujipendekeza,subirini mabwana zenu wa ccm waondelewe ndio mtajua kwamba wanaume wameamua
ReplyDeleteHivi ana sifa gani?
ReplyDeleteKashapewa pesa huyu! si mlimuona Ikulu ya dodoma au siyo huyu!! atuondolee utumbo hapa.
ReplyDelete