TCRA Watoa ADHABU Kwa Kituo cha Televisheni cha ITV

Mamlaka ya Mawasiliano nchini (TCRA) imetoa  adhabu ya onyo  kali  na  kukitaka  kituo cha  ITV kuomba radhi mara mbili mfululizo kwenye taariifa zake za habari baada ya kukiuka sheria ya utangazaji nchini ya Mwaka 2005.

Hukumu hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na kamati ya maudhui ya utangazaji, katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Margaret Munyagi (pichani) wakati wa Mkutano na Waandishi wa Habari ambapo  Muyangi  alisema kamati hiyo imebaini kituo cha  ITV kulikiuka sheria hiyo ya utangazaji nchini kwa kurusha taarifa ambayo ingeweza kuleta machafuko nchini.

Alidai katika kipindi cha Habari zilizotufikia muda huu kilichorushwa siku ya Jumatatu ya tarehe 10 mwezi huu majira ya saa 2.22 asubuhi , ITV  Walitangaza  “Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepiga marufuku maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo Chadema wakati wa kumsindikiza Lowassa kwenda kuchukua fomu ya Urais."

Alisema katika kipindi hicho Mtangazaji wake alisikika akisema Jeshi hilo limezuia maandamano hayo baada ya kubaini yanauvunjifu wa amani huku Mtangazaji huyo akimnukuu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam Suleiman Kova akidai ndo amesema hivyo,Wakati taarifa hiyo ilikuwa ya upotoshaji kwani jeshi hilo halikuwa limetoa taarifa hizo..

Bi Muyangi  alisema baada ya ITV kurusha taarifa hiyo ya kwanza juu kuzuiliwa  huko kwa maandamano, ndipo siku hiyo hiyo  tena katika kipindi hicho cha Habari zilizotufikia mda huu majira ya saa tatu asubuhi kilirushwa taarifa inayosema Jeshi la Polisi limeruhushu maandamo ya Chadema kutoka Makao makuu wa Chama cha Wananchi CUF Buguruni Jijini Dar es Salaam kwenda Ofisi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi NEC.

Muyangi alidai katika taarifa hiyo ilisikika sauti ya Kamanda Kova juu ya kuruhusu maandamono hayo,tofauti na taarifa ya kwanza ambayo haikuweka uthibitisho wa Kamanda Kova.

Alisema baada ya Mamlaka hiyo kubaini makosa hayo,Kamati hiyo iliwasiliana na Mkurugenzi wa ITV Bi Mhavile na mkurugenzi wa Redio one Deogratus Rweyunga pamoja na Mhariri wa ITV Steven Chuwa ili kutaka  ufafanuzi ambapo wote kwa pamoja walikiri kosa hilo huku wakisema Mtangazaji huyu alitoa taarifa kwenye Mitandao ya Kijamii ambayo ilikuwa inakataza maandamano hayo ambapo alishindwa  kuithibitisha kama taarifa hiyo  ni ya kweli au la.

Aidha, Bi Muyangi alisema baada ya Kamati hiyo kusikiliza pande zote,ndipo wakatoa hukumu kwa kupitia sheria ya Utangazaji ya mwaka 2005 ambayo inakataza kituo chohote cha Utangazaji kurusha taarifa zinazoleta mchanganyiko katika jamii,
Tags

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. wafungieni TV imekuwa na habari za udaku kama yale magazeti ya global what a shame.

    ReplyDelete
  2. kaatika kipindi hiki tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu mamlaka hii hususani viongozi wake wakatae kutumika vibaya kwani mwenye macho haambiwi tazama.jee tangazo la kamanda kova halikuonwa na mamlaka?.wafuatiliaji makini tunatunza rekodi.acheni vitisho vya chuki kwa kukubali kutumiwa.angalieni mwisho wa siku.

    ReplyDelete
  3. Wafungieni TBC kama mna hiyo jeuri. Watu mna eliminate yenu, lakini matumizi na chama Tabata m nakubaliana hivyo hivyo tu. Freedom of speech iko wapi hapa.

    ReplyDelete
    Replies
    1. ACHA UJINGA WAKO FREEDOM OF SPEECH NI KUSEMA KITU AMBACHO HAKIPO? AU NI KUTUKANA HOVYO? DARASANI WALIKWENDA KUJIFUNZA NINI KAMA SIYO KUFUATA WEREDI? INAVYOONYESHA HATA DARASA HUKWENDA KAZI KUVUTA ONGA, HOVYOOOOOOOOOOOOO

      Delete
  4. Wafungieni hao TBC na UHURU na mzalendo basi. Watu mna elimu yenu lakini mnatumiwa na chama tawala bila kujijua....mwisho wa ccm umefika

    ReplyDelete
  5. sijawahi kuona wala kushuhudia hasira za kiwendawazimu kama zilivyoonyeshwa na viongozi wa mamlaka hii.wangelipima kwanza agizo shinikizo walilolipokea toka kwa mwajiri mkuu.wamesoma,wasome nyakati.mfa maji haishi kutapatapa,ndio wanaondoka hivyo bye-bye.

    ReplyDelete
  6. ITV HAINA MFANO KWA UBORA

    ReplyDelete
  7. Acheni ubwege,watu lazima wafuate maadili ya uandishi wa habari na si kusikiliza maneno ya kwenye kahawa na kutangaza kama taarifa ya habari.Tumieni elimu yenu kwa weredi msifuate maneno ya wanywa viroba.BIG UP TCRA fanyeni kazi yenu.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad