TCRA yatoa onyo kali kwa TBC1 kwa kuzikwepa habari za UKAWA na Kupendelea CCM

MAMLAKA ya mawasiliano nchini (TCRA) imekipa onyo kali  kituo TBC1 kwa kosa  la  kubagua kusoma taarifa zinazohusiana na UKAWA.

Hukumu hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na kamati ya maudhui ya utangazaji, katika ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati hiyo Walter Bugoya wakati wa mkutano na waandishi wa habari.

Bugoya alisema kamati hiyo imebaini TBC one imekiuka sheria ya utangazaji ya mwaka 2005  pamoja na sheria ya uchaguzi ya mwaka 2015 kwa kufanya upendeleo wa vyama katika taarifa zake kwenye kipindi.

Alidai katika kipindi cha Jambo Tanzania kilichorushwa tarehe 15 mwezi huu majira ya saa 12 asubuhi hadi saa tatu, katika kipingele cha uchambuzi wa magazeti mtangazaji wa kipindi hicho alikuwa anayasoma magazeti huku akiruka kusoma habari kuu husika.

Alisema Mtangazaji huyo alipokuwa anachambua gazeti la Majira na Nipashe alidanganya umma jambo ambalo amedai ni kosa.

Bugoya alitaja makosa hayo  kuwa ni wakati  mtangazaji huyo alipokuwa anasoma Gazati la Majira  ukurasa wake wa mbele alisema habari kubwa ni “CCM yazidi kuwaumbua wanaomfuata lowassa” wakati habari  kubwa ilikuwa inasomeka hapo ni ile inayosema “Mbeya kwafurika”, huku picha ya gazeti hilo likionyesha picha ya umati watu pamoja na mgombea wa Urais wa chadema Edward lowassa akihutubia.

Alisema mtangazaji huyo pia alifanya kosa lingine kama hilo pia wakati akisoma Gazeti la Nipashe ambapo alisema Habari iliyopewa uzito wa kipekee ni  “Mbalawa atoa sheria ya mitandao”  ambapo habari iliyopewa uzito ilikuwa ni ile “Mafuriko Mbeya” na sio aliyokuwa anaisoma yeye.

Alisema baada ya Kamati yake kubaini makosa hayo waliwasiliana na mkurugenzi wa TBC one Bwana Mshana.

Mkurugenzi huyo alitoa utetezi wake kwenye kamati hiyo akisema mtangazaji huyo hakufanya kosa kwakuwa alikuwa hajaridhika na taarifa zilizokuwa zimeandikwa kwenye magazeti hayo.

Sanjari na hayo Mshana alizidi kujitetea akidai kuwa hata mtangazaji huyo  asingesoma habari ile lakini picha iliyokuwa inaonekana kwenye magazeti hayo tayari mtazamaji alikuwa ashajua kwahiyo amedai haikuwa na ulazima wa kusomwa.

Bugoya alisema baada ya kusikiliza upande wa TBC one ndio wakabaini kituo hicho kilikiuka sheria ya utangazaji ya Mwaka 2005 ambayo inavitaka vituo vyote vya utangazaji nchini kuripoti taarifa kwa kutokuwa na upendeleo wowote.

Alisema Kamati imefikia uamuzi wa kuipa onyo kali TBC one na endapo wataendelea basi Mamlaka hiyo haitasita kuwachukulia hatua kali zaidi.
Tags

Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. TCRA ANGALAU KWA HILO TUKIO LA TAREHE 15 AUGUST 2015 MMELIONA NA KULIFANYIA KAZI LAKINI CHA AJABU YA MUNGU MAKUSUDI YA KUPINDUA HABARI KUPOTOSHA UMMA WA WATANZANIA YAMEKUWA TAKITEKELEZWA KILA SIKU YA MUNGU KWA KILA AINA YA TAARIFA INAYOHUSU MWELEKEO WA UCHAGUZI MKUU WA MWAKA HUU KWA UCHACHE TUMEGUNDUA UPOTOSHAJI WA TAARIFA UPENDELEO WA WAZI WAZI KWA MGOMBEA WA CCM MARA 956.MAANA YAKE NINI?MAANA YAKE TBC INAPASWA KUFUNGIWA KURUSHA MATANGAZO MARA MOJA IT IS LONG OVERDUE.NAWAULIZA TCRA JEE WALI MONITER COVERAGE ZA TBC ONE KWA TAREHE 18,19,20,21,NA 22 AUGUST HII? KUHUSU KAULI ZA UONGO NA UZANDIKI ZA MKURUGENZI WA TBC AKITUMIA NGAO YA KIBURI CHA KIKWETE MAMLAKA INAPASWA IMHUKUMU ILI UNAFIKI WAKE UTUMIKE KAMA ONYO SAHIHI KWA WALE WOTE WANAOLEWA MADARAKA YAO TUNASUBIRI TUONE HILI NI SUALA LA UAMUZI WA LEO NA SIO KESHO

    ReplyDelete
  2. ni kituo cha tv cha hovyoooo kabisa, ndiyo maana binafsi taarifa za habari za bongo sizifuatiliagi

    ReplyDelete
  3. huo ndiyo msimamo wetu sisi raia watanzania tuliopotoshw sana sana na TBC One leo hii tbc anglikuwepo tido mhando upuuzi huu wa kitoto unaopewa maelekezo binafsi na kikwete usingalikuwepo.mnajua huyu mkurugenzi wao mshana hakuitegemea zawadi hiyo ya cheo aliyopewa na kikwete mwaka huu sisi na waosahani moja bakuli moja.

    ReplyDelete
  4. Tafuteni Radio nyingine jamani si ndio maendeleo tunayotaka kama kwa Obama vile kuna FOX NA NBCA Moja Republicans na nyingine Democrats, unauamuzi wa kusikiliza wapi mna lalamika. I don't care hata ukija na matusi yeni tusha yazoea.

    ReplyDelete
  5. Kitambo Sana hiyo tv nilisha acha kuangalia

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad