UKAWA Kutumia Viwanja wa Jangwani Jumamosi

Malalamiko ya vyama vinavyounda UKAWA ya kakatazwa kutumia uwanja wa jangwani kuzindua kampeni yameanza kufanyiwa kazi na tume ya taifa ya uchaguzi na taarifa zilizotolewa na mkuu wa idara ya mawasiliano ya CHADEMA Bw.Tumaini Makene imesema kuwa

Ghafla hiyo itafanyika kwenye uwanja huo kama ilivyokuwa imepangwa.
Bw.Makene ametoa taarifa hiyo kwenye mkutano wa baraza la vijana la vyama vinavyounda UKAWA na waandishi wa habari ambao pia viongozi hao wametumia nafasi hiyo kuiomba tume ya uchaguzi kuwakemea viongozi na watendaji wa serikali kufanya kazi za siasa kwa lengo la kukibeba chama tawala.

Viongozi hao wa vijana wamesema hatua ya viongozi na watendaji wa serikali ya kujihusisha moja kwa moja na kampeni za CCM huku wengine wakitumia rasilimali za umma na vyombo vya dola kukandamiza vyama vya upinzani inathibitisha ukweli wa malalamiko yao.
Tags

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hongereni makamanda!! UKAWA oyeeeeee!!!

    ReplyDelete
  2. UKAWA Pumu imepata mkohozi hebu wapeni uwanja tuwaone watuondolee kelele wamepata sababu za kuzoza kama hawakupasuka msamba kuiga kunya kwa tembo ukubwa wote wa nchi kama tanzania wamekosa uwanja isipokuwa pale pale ilipofanyia CCM na wao lazima ni kutafuta shari na lawama na umaarufu usio na tija tunasubiri sera zenu mwageni hata kwenye redio za mbao tutawaeleweni halafu mtuachie sisi wapiga kura tutoe hukumu October 25 tulizeni munkari

    ReplyDelete
  3. CCM MNAOGOPA NINI??

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad