Ushauri: Mumewe ana Maumbile Makubwa, Mkewe Anaumia Wakati wa Tendo la Ndoa

Habarini wadau,

Nitakuwa wazi sana na kwa anayeweza kunisaidia anisaidie ila kama mtu hajui/ hawezi kutoa msaada basi ni bora akaacha kuchangia kuliko kutusi/ kudhihaki.

Nina kaka yangu kabisa ambaye kiukweli alizaliwa na uume mkubwa kupita kiasi, namaanisha sote tuna maumbile makubwa lakini wa kwake umekuwa na matokeo mabaya kwa mkewe.

-Mke wake (shemeji yangu) amekuwa akilalamika mara kwa mara wakati wa tendo la ndoa, na kiasi kwamba kaka anasema huwa haridhiki afanyapo tendo hilo na mkewe kwani hamalizi hamu na anaishia njiani.

Ilifikia mahali kama kaka akirudi kutoka safari naye mkewe anaondoka kwenda kwao kwa sababu isiyo ya msingi, ila kuna siku alimtumia bro meseji kuwa "sina kizazi cha kuharibiwa hapo kitandani" ila sasa wana mtoto mmoja.

Mkewe anasema alikuwa anapata nafuu akifanya wakati akiwa mjamzito ila baada ya kujifungua akifanya anaumia sana kama zamani. Mwaka 2010 kaka alienda hospitali akapewa vi rubberband vya kuvalisha kwenye uume na alivileta home

Ila anasema akivaa na uume ukasimama haswa anaumia sana. Hata hivyo kuna daktari mwingine alimwambia asiivae kwani inazuia flowing ya damu vizuri katika uume.

Huyu shemeji siku hizi hata akienda harusini au katika shughuli yoyote basi ataunganisha mpaka kwao na anamkwepa mumewe mara kwa mara ila kwa bahati nzuri hasemi kwa watu wa nje.

Ila sasa nafikiri mama yake pamoja na dada zake wanajua,na kiukweli ni kama hana hata wivu akisikia mumewe ana mwanamke wa nje.

Naombeni mtusaidie katika hili wadau

Natanguliza shukrani

By Awsom-JF
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mpishe Wema kashazoea size mbalimbali.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad