Ushindi wa Urais Kwa John Magufuli Utaletwa na Ukawa Wenyewe

Kwa muda mrefu nimekua nikifuatilia pilika pilika za vyama vya siasa kuelekea October ambapo utafanyika uchaguzi mkuu, na kupata rais wa awamu ya tano. Kwa mtazamo wangu ukawa watashindwa vibaya na Mh. John Pombe Magufuli. Sababu kubwa ninazoziona ni hizi hapa.

1. Ukawa ikiongozwa na chama kikuu cha upinzani kimekosa sura ya kitaifa
Kwa kiasi kikubwa viongozi wa ukawa hususani chadema kilichotoa mgombea urais kimekosa sura ya kitaifa. Viongozi wengi wa chadema wanatoka kaskazini, hii ni weakness kubwa sana kisiasa,, chama cha siasa kwa mazingira ya Tanzania kama kinataka kuchukua dola ni sharti kiwe chama cha siasa chenye sura ya kitaifa ili kipate support kutoka sehemu mbalimbali ya jamhuri ya muungano.

2. Dhana mfu ya mabadiliko
Kwa mtu mwenye civic competence kubwa na anauwezo mkubwa wa kuchambua mambo atakubaliana na mimi hakuna uhusiano wowote wa maana kati ya kubadili chama ili upate mabadiliko, nakubali kabisa kua na upinzani wenye nguvu ni kitu bora katika kujenga utawala bora lakini uhusiano na mabadiliko ni mdogo au hakuna kabisa. Nitatoa mfano: Japani toka mwaka 1955 kimeongozwa na chama kimoja cha siasa LDP TOKA mwaka 1955 mpaka 1993 kikatolewa madarakani kwa mda wa miezi 11 kikarudi tena madarakani mwaka 1994 mpaka 2009 kikatoka tena madarakani, mwaka 2012 kikarudi tena mpaka leo. LPD ndio chama kilicholeta mabadiliko makubwa ya kiuchumi kutokana na sera nzuri za kujenga uchumi. Chama cha kikomunisti cha China kimekaa mda mrefu sana na CHINA ipo hapo ilipo leo.

Tatizo kubwa la UKAWA ni kudai mabadiliko kwa kuwaaminisha wananchi kwamba CCM ikitoka madarakani maisha yatakua mazuri. Kuna tofauti kubwa ya ahadi, kwa maana ya kuleta mabadiliko na kuja na mikakati mizuri ya kiuchumi na kijamiii ili waaminiwe kuongoza nchi, sera zao hazieleweki na wanatumia matatizo ya vijana kwa kuwadanganya kua maisha yatabadilika CCM ikitoka madarakani.

3. Udhaifu wa Mgombea wa UKAWA
Ukawa nawamgombea urais dhaifu, hana uwezo wa kujenga hoja na haelezi vitu vya msingi ili kujenga uchumi na taifa hili na kuleta hayo “MABADILIKO” Lowassa kwa mda mrefu jukwaani ameshindwa kujieleza vizuri, amekua haelezi nini atafanya zaidi ya kuhamasisha vijana wadai mabadiliko, LOWASSA NI DHAIFU SANA KUJENGA HOJA UKILINGANISHA NA JOHN MAGUFULI, hili litawaletea matatizo makubwa mbele ya safari kampeni zikipamba moto c z magufuli anauwezo mkubwa wa kujenga hoja na kuitetea vizuri.

Naomba kuwasilisha.

Maoni Huru Kutoka Kwa Manelezu

TEMBELEA WEBSITE YA SIASA >>WWW.WAZOHURU.COM

Post a Comment

16 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hana lolote uloandika wanaotaka mabadiliko ni wanachi sio viongozi,mabadiliko ya kiuchumi na kisiasa kwa hapa tulipofika CCM haitaweza tena, na hawatakuja waweze milele na milele zaida ya kujilimbikizia mali na familia zao,wameshatuona watanzania wajinga na hatujitambui

    ReplyDelete
    Replies
    1. ZITAJE SERA AMBAZO ZA CCM UNAZO ZIJUA AMBAZO HAZIKUTEKELEZEKA.MAANA USIONGEA KITU USICHO KIJUA KWASABABU YA MIKUMBO HATA ILANI YA CCM HUJAWAHI KUIONA,LAKINI MANENO MENGIIII !!

      Delete
  2. Ohhh umetafuta utukanwe na wakereketwa wa UKAWA hata ingawa hoja zako zina mshiko kwa asilimia 200 hawa watu ni sikio la kufa

    ReplyDelete
  3. analysis yako mbovu. wakati wa nyerere viongozi wengi walitoka kwenye kanda ya ziwa, kwani hilo lilikuwa tatizo?

    ReplyDelete
  4. Sasa inaoneka wazi kabisa pengo aliloacha Dr. Slaa hakuna wa kuliziba meli UKAWA yakosa nahodha yaenda mrama tizama hata kampeni zao hazina kichwa wala miguu mchoko Edo anapandishwa daladala ili iweje mzee kachooka Mbowe, Lisu, mmeishiwa mbona mnatuletea uhuni au ndo moto wa mabua hakuna jipya

    ReplyDelete
  5. BIG UP ! Alikuwa anaangalia tatizo la usafiri ambalo CCM Kwa miaka 54 wameshindwa
    Magufuri nae kawa msanii kama JK ahadi 32 sina mbavu mie,dada yake nae kaniacha mdomo wazi 50 million kwa kila kijiji piga hesabu vijiji zaidi ya 20,000,shule za kata tu zimeshinda watoto wetu mpaka leo wanalala chini HAPA DAWA KUWAODOA CCM NA SERIKALI YAO TUUUNDE TIMU, MPYA,KILA SIKU NAMUOMBA MUNGU KWA HILO

    ReplyDelete
  6. POLE SANA MKUU UKAWA NI TAASISI, IPO IMARA NA ITAEDELEA KUWA IMARA , ENDELEENI NA MIPASHO YENU KWANI TUMEWAZOEA NA TAARABU ZENU KAMA ILINYO MWENYEKITI WENU,TUNAWAFAHAMU.

    ReplyDelete
  7. Katika tafti yangu niliyoifanya ndani ya mwezi huu, nilijaribu kuzunguka baadhi ya mikoa hapa tanzania ambaopo nimefika Tanga, Pwani, Morogoro, na Singida. Nikajaribu kufanya tafti na kugundua kwamba kitu kinacho wakwaza wananchi wengi kwa sasa ni desturi ya chama tawala kuwa na sera feki (zisizo tekelezwa) kwa makusudi au bahati mbaya hivyo wengi wakiwa na hasira ya kurudia matapishi yale yale na wengine kufika mbali na kulinganisha wagombea na nguo kwamba uivaapo kwa muda mrefu hupoteza mng'ao, ubora na mvuto na kuiweka pembeni na kununua nyingine hivyo ndgu zangu tuweni makini sana katika kuchangua mtu sahihi atakaye lipeleka mbali taifa letu katika misingi ya haki kwa wotee bila kujali makundi, dini, kabila ili mladi awe mwenye kutii mamlaka zilizo weka kisheria. MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU BARIKI VYAMA VYETU.

    ReplyDelete
  8. Thanks for the most profound analysis. I keep telling people that Ukawa has failed to disclose their plan in governance. They have made this election as a mere we against them with no substance..

    ReplyDelete
  9. GREEN n YELLOW TU,
    HAPA KAZI TUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUUU.

    ReplyDelete
  10. NAJIBU KWA HOJA.
    1. Huwezi kusema Chadema imekosa sura ya kitaifa wakati imeenea nchi nzima mpaka sasa. Hao wanaipokea hawakuona ukaskazini????

    2. Huwezi kulinganisha MFUMO wa CCM na vyama vya Japan na China kwa kuwa KAMA TUNATAKA MABADILIKO YA KWELI, HATUWEZI KUYAPATA KWA MFUMO MBOVU WA CCM. Hilo unalijua.

    3. Lowassa ana maneno machache ya msingi na sio kuwa hawezi kujenga hoja.... Umegubikwa na mawazo ya chama chako sana ndiyo maana huwezi kuona HOJA ZA LOWASSA katika maneno yake machache....

    FIKIRI VIZURI UJE NA HOJA

    ReplyDelete
    Replies
    1. yaaani katika watu mburura ni wewe wa kwanza katika dunia hii maana hata mtoto mdogo anakuzidi kujibu hoja na kuandika vitu vya msingi. huna hata ushawishi ni upumbavu uliouandika. kuwa makini maana hata kichaa ni afadhali kuliko wewe

      Delete
  11. MTOA MADA YUPO SAHIHI KABISA, HUU UBISHI WENU NDIO UNAOWASABABISHIA moto wa mabua, MNGEMSIKILIZA DR MAMBO YOTE HAYA SAHIZI TUNGEKUA TUNAYASIKIA UPANDE WA PILI, UKAWA hamna jipya kwa hili mkubali udhaifu wenu ili mjinasue vinginevyo ikulu mtaendelea kuisoma kwenye NIPASHE, WEREVU MWINGI MBELE GIZA

    ReplyDelete
  12. Tatozo la wtz wengi wanapenda kufuata mkumbo lkn ukweli kwa mtu aliye na akili timamu yafaa ajiulize kwnn viongozi wa chadema wote wanatokea upande mmoja hayopo anaetoka Mtwara, Ruvuma, Mbeya, Kigoma, Kagera, Mara na mikoa mingi hawapo hii haipendezi ht kidogo wakamuona zito co wa moshi wala k/njaro wakamkataa wkisahau kua zito ni miongoni wa watu walioifanya chadema kua pale ilipo.
    Hili jambo linanipa wacwac sn.

    ReplyDelete
  13. HUWEZI KUONGEA KWA JAZBA KAMA MKAPA, PAMOJA NA KWAMBA MKAPA KAKAA FOREIGN AFFAIRS BADO HAJAWEZA KUWA NA BUSARA! YOU CAN BE WELL EDUCATED; BUT YOU MAY LACK THE BASIC WISDOM AND SKILLS NEEDED TO LIVE IN A SOCIETAL CONTEXT!

    ReplyDelete
  14. Chadema bado sana wanaoshabikia huko asilimia kubwa nia Genge la wahuni tu
    hata hawajiulizi kwa nini mpaka sasa DR kimya Mafichoni
    kuna walaka ulitembea kuwa ataonekana Jangwani
    'mbona alitoa kauli ya kwamba si yeye kwa nini kawa kimya na anawaweka roho juu wanachama wake?

    huu ni mchezo hao akina mboe na wengine wajuaji kama mnyika na tundu Lisu wote kimya midomo imeshiba

    nawaambia mwisho wa chadema umefika kama mmekubali kununuliwa basi na chama ndiyo mwisho wake

    haiwezekani mtu mmemchafua kwa zaidi ya miaka 6 kisha mnakubali na kumpa madara makubwa ndani ya wiki moja kisha Mseme ni mtu safi

    hivi katiba ya chama chenu inasema mtu akija kama mwanachana anaweza kupewa ridhaa ya kuwa kiongozi ngazi ya uraisi kwa wiki moia?
    inaingia akilini kweli? je kama mamluki mnamwamini vipi?

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad