UVCCM Yamvaa Lowassa, Wasema Watamnyosha

Ndugu waandshi wa habari 
Assalama Alaykum 
Ndugu waandishi wa habari, 

Nchi yetu hivi sasa inapita katika hekaheka za kuelekea uchaguzi Mkuu. UVCCM tumewaita hii leo ili kuwapa taarifa yetu juu ya mwenendo wa kisiasa, suala la vijana na uchaguzi mkuu, mkakati wa UVCCM kuhakikisha wagombea wa Urais kupitia CCM kuhakikisha wanashinda kwa kishindo kikubwa na kuwapa idhari viongozi wa CHADEMA wajiandae kuwahakikishia watanzania kama Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa alihusika na vitendo vya ufisadi kama walivyodai au laa.

Aidha UVCCM tunampongeza kwa dhati mgombea wa CCM Dk John P. Magufuli kwa kuchukua fomu ya urais wa Jamhuri ya Muungano kwenye Ofisi za Tume ya Uchaguzi (NEC) akiambatana na mgombea mwenza wake Mhe, Samia Suluhu Hassan, 4 August 2015.

Pia Furaha yetu haijifichi na tunapenda kumhakikishia Dk Magufuli na Dk Shein tutabaki nao bega kwa bega ambapo pia hatutasita wala kurudi nyuma kufanya kila linalowezekana kuhakikisha wanapata ushindi wa kishindo cha ajabu kitakachowashangaza na kuwashtua wasaka vyeo na madaraka na wanaotumia gharama za fedha ili kupata uongozi.

UVCCM tunapenda kuwasihi vijana wenzetu wajiweke kando na wanasiasa wachovu waliochoka kifikra na kimwili ambao hawahimili mikiki ya siasa za kileo wanaopania kuwachochea vijana washiriki vurugu na fujo.

UVCCM tunawataka vijana wenzetu kutokubali kughilibiwa, kutumiwa na wanasiasa wachovu kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba mwaka huu. Badala yake sote kwa pamoja tutenge muda na wakati wetu kulinda amani, utulivu na umoja kitaifa kama sera ya CCM inavyosisitiza siku zote..
UVCCM tunachukua nafasi hii kuwakumbusha viongozi wa upinzani husasan CHADEMA kuyakumbuka matamshi walioyatoa na kuyasambaza nchi nzima miaka kadhaa iliopita sasa ni wakati wao kutoa majibu sahihi mbele ya wananchi.

Viongozi wa chama hicho kwa nyakati tofauti walitoa madai mazito dhidi ya mwanachama wao mpya Edward Lowasa na wengine kwa kuwatuhumu kuhusika na ufisadi wakati viongozi wa chama hicho wakihutubia kwenye majukwaa ya kisiasa.
Tunafikiri watatenda ungwana kuwathibitishia watanzania kama wao ni wakweli na si wanafiki wa kisiasa, wababaishaji na wazushi wasiofaa kusikilizwa.

Yale walioyasema, kuyaamini na kuyaeneza sasa ni wakati wao muafaka kuyafafanua, kusema ukweli na kama waliongopa kwa kutafuta umaarufu wa kisiasa wawatake radhi wananchi na wakiri wao ni wataalam wa kuzua na watamke kwa kukiri CCM si chama chenye makandokando ya ufisadi.

Wakati wakijiandaa kumkosha kila waliyemtuhumu katika kina kikubwa cha maji wajue kuwa bila ya kutoa ufafanuzi tope za madai ya ufisadi zitawachafua viongozi wa CHADEMA na kiongozi wanaembeba wakati huu wanapojaribu kutaka kuwashaulisha watanzania. Ni vyema viongozi hao wakatambua kuwa neno likishatamkwa ni vigumu kulirudisha mdomoni.

Ndugu waandishi wa habari.

Tokea kupitishwa na kutangazwa jina la Dk. John Magufuli, kuwa mgombea wa Urais, zama mpya imepambazuka mbele ya upeo wa macho ya watu . Ngurumo za kusafisha mafisadi zimeanza wa kasi kwenye vyama vya upinzani .Kasi hiyo na kusafishana ni hofu walionayo wapizani baada ya kuona ni vipi vyama hivyo vitashindana na mgombea urais wa CCM asiyekabiliwa na tuhuma,
asiyetiliwa shaka huku akiamainiwa na makundi ya vijana, wanawake, wazee, wasomii, wakulima na wafanyakazi kwa utendaji na uchapakazi wake mahiri.

UVCCM chini ya Chama Cha Mapinduzi tunaipongeza Kamati ya Madili, Kamati kuu, NEC na Mkutano Mkuu wa Taifa kwa kushiriki mchakato wa kuyapitisha majina ya wagombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Zanzibar.

Tunaona fahari kupata wagombea waadilifu, waaminifu, wachapakazi na waaminifu kwa CCM na Taifa letu wakipeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mkuu ujao Oktoba mwaka huu.

Tunavipongeza vikao hivyo kwa kupitisha wagombea ambao CCM haitapata kazi na gharama ya kuwanadi kwa wananchi wakati wa kuomba kura. Wagombea waliochaguliwa mikono yao ni misafi, hawatiliwi shaka na hawana uchovu zaidi ya kuwa na weledi, uzalendo na kuheshimu kwao misingi ya utawala bora.
Ndugu waandishi wa habari,

Tunampongeza na kuunga mkono kauli ya Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Jakaya Mrisho Kikwete aliyoitoa katika viwanja wa Ofisi ndogo ya Makao Makuu ya CCM Lumumba jijini Dar Es Salam kuwa "tumejiandaa kushinda na tutashinda, tuna uzoefu wa kutosha tunayo maarifa mwaka huu tutatapata ushindi mkubwa." Kauli hiyo imetupa nguvu na ari vijana wa CCM tukiamini CCM ni chama kikubwa kilichosheni hekma na mikakati mizito ya kulivusha taifa wakati wowote wa misukosuko ya pepo za kisiasa. Vijana wa CCM imetulazima kukumbuka historia ya pepo za misukosuko kabla na baada ya uhuru 1961 na Mapinduzi ya 1964.
Historia inaonyesha mwaka 1958 kiongozi wa juu katika TANU Zubeir Mtemvu alijitoa na kuanzisha chama cha ANC na TANU hikugawanyika, mwaka 1967 Waziri muandamizi katika serikali ya TANU Osca Kambona alijiondoa na TANU ilikuwa imara, Mwaka 1959 ASP iliwatimua kina Mohamed Shamte Hamad na kuenda kuanzisha chama cha ZPPP na ASP ilizidi kuwa imara na kujipanga hatmae 1964 ikafanya Mapinduzi.

Mwaka 1984 CCM inayotokana na TANU na ASP ilimvua madaraka aliyekuwa Rais wa Zanzibar Mzee Aboud Jumbe Mwinyi CCM haikutetereka, mwaka 1984 ilimfukuza Seif Shariff Hamad na wenziwe 6 CCM haikugawanyika, mwaka 2014 CCM ilimfukuza unachama waziri wake muandamizi (MNEC) Mansour Himid Yussuf CCM haikubabaika, 2015 CCM ilimfukuza unachama mkongwe wa siasa Hassan Nasoro Moyo bado hatujahamanika wala hatukujutia.

Hatuna la kupoteza wala kujutia kwa sababu ya kuondoka Lowasa ndani ya CCM, sisi vijana tunamini kuwa sasa LOWASA si agenda tena ndani ya CCM inayoweza kutusumbua CCM imefunga mjadala.
Vijana tunaendelea kujifunza na kuamini kuwa CCM iliyotokana na TANU na ASP imepita katika misukosuko mingi na imeweza kuhimili vishindo bila kugawanyika na harakati za ukombozi ziliendelea hadi wazee wetu wakitimiza malengo waliyoyakusudia.

Tunarejea tena hatuna cha kupoteza wala kujutia Lowasa kaondoka CCM aende tu na mjadala huo umefungwa tunaimani kubwa na umakini wa viongozi wetu CCM ndio ile ile, wembe ni ule ule, kinyozi ndio Yule Yule hakuna jipya Oktoba 25 kitaeleweka baada ya kumaliza kazi ya safari ya Magufuli na Shein Kuipatia ushindi CCM.
Kubwa tunawakumbusha wapizani wetu hatudharau adui UVCCM tumejipanga kulinda heshima ya Chama, tunasema mwaka huu Mlingoti Chuma, Bendera Chuma na upepo Chuma tunasonga mbele kwa uwezo wa MwenyeziMungu.

waandishi wa habari,
UVCCM tukiwa ni jeshi la msitari wa mbele la CCM tunataingaza rasmi vita ya mapambano ya hoja kwa hoja katika siasa na sasa tunasema Aluta kontinua. Mapambano yanaendelea dhidi ya mawakala wa ubeberu na ukabaila waliojipenyeza katika siasa za nchi yetu, Sisi UVCCM tunawaambia kamwe Ikulu ya Magogoni kule Dar es Salaam na ile ya Mnazi Mmoja hapa Zanzibar katu haitakuwa mahamia au machaka ya kujificha Mafisadi.

Asanteni kwa kunisikiliza.

Shaka Hamdu Shaka (MNEC)
Naibu Katibu Mkuu UVCCM (Tz) Zanzibar
6. Agost 2015

Post a Comment

20 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mnakazi Mbowe na CDM mmeingia choo cha kike bora msingemtibua Dr Slaa labda tungewaelewa

    ReplyDelete
  2. Nendeni kawaanyosheni baba zenu wezi wa ccm kwanza ndiyo mje kuongea na UKAWA, majangili watoto nyie,hiyo nchi inaamuliwa na vijina ambao tuko tayari.

    ReplyDelete
  3. Iwananchi, ogopeni kuichagua CCM. Hiki ni chama change majanga, chama cha mtu, cha cha madudu, chama cha majizi, chama cha mafisadi, chama cha maovu. Mungu alisema, ulituma dhambi utaokoka, wako waliotubu, na sisi tutawapokea, wataishi kama katika zetu zinavyosema. Inshaalah, nchi yetu it apana ukombozi wa pili toka kwa makaburu wa humu humu ndani.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe majanga kweli kweli yaani kama vile unasemea kutoka kaburini CCM chama cha mtu toka lini wakati UKAWA wanajionyesha wazi kabisa kimekua chama cha watu binafsi bila leseni wala ridhaa ya wananchi wamebaki kulana wao kwa wao kama samaki yale yale mliosema Edo fisadi na sasa ni msafi kabisa kuchukua nchi Mungu tunusuru kwa watu mafisadi na waoushabikia ufisadi

      Delete
  4. Wananchi, waogopeni ccm kama ukoma. Ccm ni ukimwi. Ni wangapi katika yetu hatjui kero za maji? Kero za umeme, Kero za foleni, Kero za uchaguzi mijimi, Kero za bandarini, Kero za madereva wa mabasi, Kero za hospitali, Kero za madawa, Kero za ardhi, Kero za ubinafsi (change na ufisadi na pesa ya mchicha ya mama wa UN), Kero ya reliable ya kati, Kero ya kufungiwa umeme majumbani, Kero ya tembo wetu kuuwawa, Kero ya wachina kujaa kariakoo wakauza mahindi kama experts, Kero ya wastaafu, Kero ya Mishahara ya mapolisi, Mishahara ya walimu.....NCHI HII INAHITAJI UKOMBOZI WA KWELI SASA. TUNATAKA MABADILIKO. MABADILIKO NJE YA CCM NI TOSHA, TOSHA KABISA..ONDOKENI MAGOGONI HARAKA SANA

    ReplyDelete
    Replies
    1. Utarudia sana hio sentensi ya ukoma na hivyo visababu vyako uchwara ili tumkabidhi nchi Fisadi huoni ndani tumeshawang'amua nini malengo UKAWA imeshakuwa UKIWA kwa hiyo subirini 25 Octoba mlie kilio cha mbwa mdomo wazi huku mnaimba aliselema

      Delete
  5. Wa Tanzania ogooeni UKAWA haina jipya wao kwa wao wanavurugana na wana jiuzulu, ,, majanga matupu, CCM mafisadi haya leo Lowasa msafi maana kahama CCM Ukawa hamjielewi mtaburuzwa sanaa

    ReplyDelete
  6. Alim son Shama..naomba contact sali (Email)..kuna kitu nataka nikutumie plz

    ReplyDelete
  7. Mtake mctake Magufuli ndie rais wa nchi hii, hv kweli utakua na akili gani wewe mtz uwe unapiga kelele eti Masai atakua rais... Nabaki nacheka tu tatizo watz wengi hawajitambui kabisa..wapo kishabiki tu.
    Wenzenu wana maslahi na hicho chama na ninyi je....!!? Poleni sn.

    ReplyDelete
  8. Nyie akina lemutuz,February makamba,Riz 1,mropokaji lusinde,naumpe nnauye na wengine wengi hiyo nchi siyo ya kisultani ya kukabidhiana madaraka lazima tuwaondoe baba zenu wezi ili tumuenzi mwalimu nyerere.

    ReplyDelete
  9. Nyie ni akina nani mtumie lugha kama hii kwa mtu mwingine ambaya anfuata democrasia ya nchi yetu? Au CCM ndio wao pekee yao wenye dhamana na nchi yetu? Ingekuwa ni police wanaofuata taratibu za kazi zao wangefuatilia hii statement "UVCCM Yamvaa Lowassa, Wasema Watamnyosha" - lakini kwetu......naona upuuzi na nyie wote ni WAPUUZI!!

    ReplyDelete
  10. CCM ni ukimwi, ni ukoma wanafikiri wana dhamana
    ya kuongoza tu? Naona ni kipindi Chao sasa cha kukaa pembeni kama KANU

    ReplyDelete
  11. October 25, 2015, tunachukua nchi kwenye mikono ya chama cha mafisadi (CCM), chama cha mihuni (ccm), chama cha matapila (ccm), chama cha makaburu (ccm) weusi, chama cha majambazi (ccm), chama cha mabinafsishaji, chama change magonjwa (ccm) sugu kama ukoma na ukimwi, chama cha mapapa (ccm), chama change majibu no (ccm). Angalieni KANU ilipofikia sada, someni Alamance za nyakati...wezi wa rasilimali zetu mnatapata pa sasa. Mpaka tumia a kina Nape, Kinana, Makonda na rasilimali zote za Taifa kuendelea kutukandamiza sisi wananchi tulip wengi? Mnataka wananchi wafanye shughuli zao kiujanjaujanja (BONGO).....TUOMBE MUNGU ARAB SPRING ISIFIKE KWETU....hope you know what I mean...wengi wapeni, la sivyo na nyie ccm pia mtakiona cha MTEMA kuni (kwa kuwa nyie mna vyombo vya dola ni halali yenu kumwambia mtanzania mwingine "watakiona cha mtema kuni" - i. An angry citizen

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wengi wape kina nani upo na nani jiulize kabla ya kuropoka usiunganishe mawazo yako duni kutaka kuamrisha watu wengine wewe kama nani tukufuate An angry citizen ushuzi unaijua nini maana ya arab spring walikuwa na demokrasi kama uliyonayo una bwabwajwa unavyotaka walikuwa na vyama huru vya upinzani kama vilivyoko Tanzania ukamchagua rais umtakae kama CCM cha mafisadi cha wahuni na uchafu wote ulioandika una haki ya kuwaadhibu ktk sanduku la kura na hakuna atakae kuhukumia hilo lilikuwepo ktk nchi za ARAB SPRING UNAZOZISEMA na KANU kwa akili yako ktk UKIWA kuna hata mmoja aliyebaki mwenye hekima akasukuma mageuzi kama ilivyokuwa kwa KANU badala ya Slaa na Lipumba kumwaga manyaga hao waliobaki ni ukoma kuliko ukoma huitakii mema Tanzania fikira zako zimejaa uzandiki na fitina

      Delete
  12. Week fikiria zako zimejaa uzandiki? Labda umeandika hivyo kwa sababu umefaidika na mfumo ulliopo. Wewe ndio unaropoka, nchi inaendeshwa kwa misaada tangu hujazaliwa wewe, na leo bado ndio mtaji mkubwa - mbona walipoahirisha kutoa misaada nchi iliyumba. Hilo. Ww unataka sehemu ya hiyo misaada uwapelekee familia yako? Kwani watanzania wengine hawana haki na nchi yetu? Nyie ccm ndio wenyewe wenye hati miliki ya kila kitu. Kama mmefikia mahali mnajibeza kuita watu majina, km, makapi, mtakiona, hiyo siyo jeuri? Nami nikitumia kauli chafu isiyokuwa ya kiistaarabu "Kwani mna tofauti gani na "Idiots" nyie basi" si ndio mwanzo wa kuingia mtaani? Basi ninakuambia, mwaka huu hamtaona chochote, asubuhi na mapema hemisheni vitu venu MAGOGONI haraka iwezekanvyo. Huelewi hata siasa za afrika, wala jirani zetu wa kenya, zambia, kwa hiyo kaa kimya, you Idiot

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ya nini kuandikia mate na wino upo usiwe na jazba subiri 25 October utafunga bakuli lako na mtanyooka saa ingine kusoma ujinga unatoa maneno kwa kuwaona wengine hawastahili kutoa maoni sio tatizo lako ni ukosefu wa dira siasa watu hawalumbani kwa jaziba na vitisho unakosa mengi na huitendei vizuri haki yako ya demokrasi vizuri eti hamisheni vitu vyenu magogoni ndo umeona la msingi bila kuwa na manufaa ya kuleta maendeleo ili mradi fisadi mliingize ikulu

      Delete
  13. Lol...sasa umekosa la kusema

    ReplyDelete
  14. Mate ni CCM. Huwezi kuendelea kutawala watu millioni arobaini kwa nepotism; kwa rushwa; kwa wizi wa meno ya tembo; kwa kuwaleta wachinna kuuza mahindi ya kukaanga na kuchoma kariakoo; kwa kuendelea kuendekeza wauza madawa ya kuelevya; kwa kufuatilia virushwa vidogo vidogo vya barabari (eti amekerwa na rushwa za askari wa barabarani) Ww kijana au bwana mdogo ulikuwa wapi wakati nchi hii inapata uhuru miaka 1960s? Je unakumbuka nyerere alipokea hii nchi ikiwa na reli ya kati? reli ya Moshi/Tanga? Ziko wapi hizo reli? Unakumbuka nyerere alifanya kazi mpaka tukapata viwanda vya wananchi wote (viwanda vya uma) vingi TUU? viko wapi saa hii? Niambie? Ww ni shabiki wa siasa au unapatiwa sehemu kidogo ya mgao? Labda ndio maana unaona shida kwamba Octoba 25 asubuhi na mapema ccm inaondoka madarakani! Hakuna njia tena! Hiyo ni lazima! Democrasy itawale tena nchi hii. Sheria zitumike sawa sawa kwa kila mwananchi! Si watu wa ccm wana sheria zao (au sheria za nchi haziwahusu - wanaendelea kumuuliza mwananchi wa KAWAIDA - UNANIJUA MM NANI? AU UNTAKIONA CHA MTEMA KUNI - HUU NI WENDA WAZIMU uliopindukia - HAKUNA NCHI YOYOTE DUNIANI AMBAPO SERIKALI INAWADHARAU WANANCHI WAKE KAMA SERIKALI YA CCM! Ondoa upuuzi wako hapa kwenye discussuon BOARD. kama huna la kuongea ww kaa kimya! Ondoa vitu vyako magogoni kuanzia saa mbili na nusu asubuhi ya October 25! Mungu ibariki TANZANIA, mungu ibariki wananchi wake wote! mungu mmbariki Edward Ngayai Lowassa, Raisi wetu anaesubiri KUAPISHWA!

    ReplyDelete
  15. HAWA UVCCM WANASEMA WATAMWADHIBU LOWASSA AMA KWA TAFSIRI NYINGINE WANATANGAZA HALI YA HATARI KWA MAMILIONI YA WATANZANIA TUNAOSUBIRI SERIKALI MPYA YA AWAMUYA TANO CHINI YA RAIS MPYA MPYA MHE.EDWARD NGOYAI LOWASSA.WAJIANDAE KWA HILO.

    ReplyDelete
  16. MAGUFULI ALIYEUZA NYUMBA ZA SERIKALI ZOOTE KATILI MSIMAMIZI WA BOMOA BOMOA BILA FIDIA ASIYE KUBALI NAULI MPYA FERI AOGELEE ADUI WA RAIA MASIKINI POMBE MDOMO WA CHURA CHAGUO LA MFUKONI LA MKAPA ANAANGUKA KIFO CHA MENDE NA NYINYI WAQAJIRIWA WA CCM UVCCM JIANDAENI KUTUJIBU MASWALI KUTOKANA NA JINAI YENU YA KUTISHIA MAISHA

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad