Uwezi Amini Kuwa Lowassa Sio Sababu ya Dk. Willibroad Slaa Kutoonekana Hadharani na Kwenye Vikao vya Chama..Sababu Hii Hapa

Wakati maelfu ya watu nchini wakiamini kutoonekana hadharani kwa Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Willibroad Slaa kunatokana na kuchukizwa na kitendo cha kukaribishwa kwa waziri mkuu aliyejiuzulu, Edward Lowassa , ukweli wa jambo hilo umeibuliwa.

Mjumbe mmoja wa Kamati Kuu (CC) ya chama hicho amesema, madai yanayotolewa na watu mitaani na katika mitandao ya kijamii yakisema Dk. Slaa amekasirishwa na kitendo hicho ni ya uongo.

“Kwa taarifa yako, Dk. Slaa ndiye aliyemtaka Lowassa ajiunge Chadema. Mbowe (Freeman, Mwenyekiti wa Taifa Chadema) hakumtaka kabisa huyu jamaa aje kwetu. Kwa sababu hakuona jinsi gani wangewaeleza wananchi juu yake, lakini mzee ndiye aliyeshawishi na vikao vya kumjadili vikaanza mfululizo. Ukiangalia picha za awali, Dk. Slaa yupo.

Kinachotokea kwa Dk. Slaa ni shinikizo kutoka familia yake. Kuna watu walikuwa na matumaini makubwa ya kufaidika endapo yeye angegombea tena na kushinda urais mwaka huu, hivyo wameamua kununa kwa sababu kilichotokea hakina masilahi kwa familia." alisema mjumbe huyo wa kamati kuu

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Ya kweli hayo? au unafurahisha genge?

    ReplyDelete
  2. Wacheni kutubabaisha sijui ya mjumbe mmoja wa kamati kuu CC kasema hivi madai yanayotolewa na watu mitaani na katika mitandao ya kijamii yakisema Dk. Slaa amekasirishwa na kitendo hicho ni ya uongo, Bana eee tunataka ukweli na kauli toka kwake mwenyewe Dr, Slaa hivi propoganda za enzi ya kibatali zimepitwa na wakati hivi hawa wana siasa wetu wanajifundishia wapi siasa, hawajui kuutumia uongo na wakati hawajui sasa hivi ni wakati wa mitandao wazi watu wameerevuka, mukikosolewa munakasirika munalazimisha hata kama ni uongo watu wakubali ndio kweli, mkombozi wa nchi hii bado hajazaliwa tupelekane hivyo hivyo bora salama.

    ReplyDelete
  3. October mtakubali tu,changes ni lazima na wizi kura msahau,miaka 50 ya uhuru hali inazidi kuwa mbaya halafu mnaleta mambo ya ccm hapa.

    ReplyDelete
  4. Mbona ccm mnakomalia sana mambo ya chadema?si mna makufuli nyie kwenu?sisi tuko poa nyie jiandaeni kufungasha vijana tumeamua.

    ReplyDelete
  5. ETI LOWASA MKOMBZI WA CHADEMA KIRUUUUUU MNAKUBALI KUMSALITU DR SLAA KWA UCHU WA KUINGIA IKULU MTAISIKIA WAITI HAUSI KWENYE DIGITALIIII AISEEEE

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad