Walinzi wa CHADEMA Walioongoza Msafara wa Lowassa Jijini Mbeya Watakiwa Kujisalimisha Polisi Kwa Ajili ya Mahojiano

Mnamo Tarehe 14.08.2015 Mgombea Urais Kwa Tiketi Ya Chadema Alikuja Mkoa Wa Mbeya Akiwa Ameandamana Na Viongozi Wa Vyama Vya Cuf, Nccr – Mageuzi Na Nld Kwa Dhumuni La Kumtambulisha Na Kuomba Udhamini Wa Kupeperusha Bendera Ya Chadema Kwa Nafasi Ya Urais.

Katika Msafara Wake Kutoka Uwanja Wa Ndege [songwe] Kulionekana Gari Moja (pichani) Aina Ya Land Cruiser – Pick Up Yenye Rangi Nyeusi Na Ndani Yake Lilikuwa Limebeba Vijana Ambao Walikuwa Wamevaa Mavazi Meusi, Kofia – Bereti Nyeusi Na Miwani Nyeusi Na Mabuti.

Watu Hao Walikuwa Na Muonekano Kama Askari Na Shughuli  Waliyokuwa Wakifanya Ya Kuongoza Msafara, Ulinzi Na Kazi Nyingine Zifanyazo Na Jeshi La Polisi.
 
Kutokana Na Muonekano Wao Na Shughuli Walizokuwa Wakizifanya Ilikuwa Ikitafsirika Kuwa Ni Jeshi Lifanyazo Kazi Hizo Ambalo Halikuwa Likifahamika.

Kutokana Na Sintofahamu Hiyo Wananchi Wengi Walikuwa Wakihoji “hilo Ni Jeshi Gani” Sambamba Na Kutuma Picha Kwa Njia Ya Mtandao Wa Kijamii [whatsapp] Wakionyesha Wasiwasi Waliokuwa Nao Dhidi Ya Kikundi Hicho.

Kufuatia Hali Hiyo, Ofisi Ya Mkuu Wa Upelelezi Wa Makosa Ya Jinai Mkoa Wa Mbeya Ilifungua Jalada La Uchunguzi Ili Kuwapata Vijana Wale Kwa Lengo La Kuwahoji Na Kukamilisha Upelelezi Ili Jalada Lipelekwe Kwa Mwanasheria Wa Serikali Kwa Ufafanuzi Wa Kisheria.

Hii Ni Kutokana Na Kuibuka Kwa Makundi Ya Aina Hii Hasa Kwa Vyama Vikubwa Vya Siasa Hapa Nchini.

Katika Kufanya Ufuatiliaji Huo, Wapo Watu Wawili Walikamatwa Alfajiri Ya Leo Tarehe 18.08.2015 Kwa Mahojiano Na Baada Ya Maelezo Yao Kuchukuliwa Walipewa Dhamana.

Baadhi Ya Viongozi Wao Waliokuja Polisi Wameelezwa Kuhitajika Kwa Vijana Wale Waliokuwa Katika Gari Lile Ili Wahojiwe Na Kukamilisha Upelelezi Wa Jalada Hilo Mapema Ili Mwanasheria Wa Serikali Alitolee Mwongozo Wa Kisheria.
 
           Imesainiwa Na:
[ahmed Z. Msangi – Sacp]
Kamanda Wa Polisi Mkoa Wa Mbeya.

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. This is stupid. Nyie police msitumike kisiana! Mnajua tunakokwenda na tulikotoka. Hamjawahi kuwauliza watu wa ccm swali kama hili! Nyie ni vibaraka wa ccm

    ReplyDelete
  2. mnaacha kukamata majambazi mnaangaika na watu ambao hawana hatia,kweli mmeshikwa pabaya.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Acha hizo wewe ni mmojawapo wa hao magaidi,sasa tunakufatilia na chamoto utakiona!

      Delete
    2. mbona unatisha watu hivi jamaniiiii, ah....

      Delete
  3. Sasa tunakokwenda kubaya hawa Chadema ni mamuluki itakuwaje wawe na jeshi kabla ya kushika serikali wakishika serikali itakuwaje siwatafukuzisha kazi JWTZ mzima ili wanajeshi wao wapate ajira au nchi iwe na majeshi mawili tooba je wakishindwa uchaguzi tayari tumezalisha Boko haramu yakututafuna jamani wacheni masihara tujifunze na yanayotokea nchi zingine huyu Edo kama anautaka uraisi autafute kwa njia ya usalama sio kwa shari

    ReplyDelete
  4. KWA KOSA GANI ACHENI MAONEZI.KWA NGUO WALIZOVAA.JEE WAMEVAA UNIFORM ZA POLISI AMA JESHI?ACHENI MAONEZI.ILI KUJIOKOA NA FIMBO YA BAADAYE MUWE MNASEMA ALIYEWATUMA VINGINEVYO UKAWA IKICHUKUA DOLA MTAFIKISHWA MAHAKAMANI.NCHI YETU IMEENEA MAKAMPUNI YA ULINZI WANAOVAA UNIFORM AINA NYINGI MNO MNO.MSITUMIWE TUNAREKODI

    ReplyDelete
  5. Kweli wengi tulihoji kwa kuwa Majeshi ya TZ yanajulikana,MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  6. Mbona hapa tz kuna kampuni nyingi sana za ulinzi na zina hadi wanajeshi, polisi, mgambo sasa unafikiri hawawezi kuwa na mbinu kama za kipolisi!? kuna mjeshi mmoja hivi, kwanza alikua kijana, pili msomi, tatu alikua na cheo jeshini akafukuzwa kazi! baadae akaajiliwa na kampuni ya kk security, hivi mtu kama huyu hawezi kuwa anajua mbinu za ulinzi zaidi ya polisi wa kawaida! mh! haya yetu macho na masikio.....

    ReplyDelete
  7. Kamanda Msangi tunakusoma vizuri.wewe hutapelekwa icc ni mwepesi karatasi wewe ni Polisi na Magereza ya hapa hapa nyumbani,Tunarekodi kiiila ukandamizaji wako.Sisi na wewe sahani moja baada ya 25 Octoba labda ukimbie nchi

    ReplyDelete
  8. Hivi kamanda msangi una mke na au watoto?ipe thamani familia yako,soma nyakati.ni wazi baada ya 25 octoba hutokua kamanda tena lakini ni vizuri ukaishi wewe na famili yako kwa amani na utulivu uraiani badala ya kutumikishwa pasi na kutotumia busara zako.kumbuka muda wa dola tuliyonayo unakwisha na unakuja muda wa Dola mpya ya Mhe Edward Ngoyai Lowassa.Jipange Msangi wenzio waliogutuka wanatoa ushirikiano.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad