Wakati uvumi wa kujiuzulu cheo na kujivua uanachama wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk. Wilbroad Slaa, ukiwa umetawala kupitia mitandao ya kijamii na magazeti, taarifa zinadai kuwa sababu ya kuchukua hatua hiyo ni shinikizo kutoka kwa mkewe.
Taarifa zilizochapishwa na gazeti moja likimnukuu Dk. Slaa mwenyewe, zilisema ameachana na siasa na kujivua wadhifa wake na atabaki kufanya shughuli zingine.
Dk. Slaa amedaiwa hakubaliani na namna chama chake kilivyompokea Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa.
Lowassa aliyekuwa Mbunge wa Monduli alitangaza kuhamia Chadema, Julai 28, mwaka huu baada ya kutoridhishwa na mchakato wa CCM wa kumpata mgombea wa urais.
Habari za uhakika kutoka vyanzo vyetu vya habari ndani ya Chadema zinadai, Dk. Slaa alishiriki katika mchakato mzima wa kumpokea na kuridhia Lowassa, kusimamishwa kuwa mgombea urais kupitia Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa).
Hata hivyo, chanzo kingine cha habari kinadai kuwa mke wa Dk. Slaa, Josephine Mashumbusi, alitoa shinikizo kwa mumewe la kujiuzulu baada ya kuruhusu kusimamishwa mgombea mwingine (Lowassa).
"Josephine alikuwa na uhakika mume wake ndiye atakayesimama ugombea urais kwa upande wa Ukawa, hali ilivyobadilika, akakasirika na kumwambia mumewe ama yeye au Chadema," chanzo kilidokeza.
Kupitia ujumbe uliosambaa kwenye mitandao ya kijamii, unaoonyesha kutoka kwa Mashumbusi, aliandika "Ni kweli Frida na kwa hili Dk. Slaa amejivua wadhifa wake wa ukatibu mkuu na kuachana na siasa. Hamtamsikia tena kwani hawezi kupinga anachokiamini".
Hata hivyo, Dk. Slaa alipotafutwa kupitia simu yake ya mkononi kuthibitisha madai hayo, iliita mara moja na kuzimwa. Juhudi za kumpata ziligonga mwamba baada ya simu yake kutopatikana hali kadhalika simu ya Mashumbusi.
Wakizungumza na mtandao huu, baadhi ya wasomi walisema kama Dk. Slaa amejiuzulu nafasi yake na kujivua unachama atakuwa amejijengea heshima na uaminifu na kwamba Chadema kitapata pigo.
Mhadhiri wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Benson Bana, alisema kwa upande wake aliamini kitu kama hicho kitatokea kutokana na tukio hilo kuwa la haraka na kulifananisha sawa na mapinduzi ya ghafla ndani ya chama.
“Nafikiri kama kweli Dk. Slaa amejivua uanachama itakuwa ni jambo zito na pigo kwa Chadema, lakini ni uamuzi wa busara na kumjengea heshima kwa jamii,” alisema Dk. Bana.
Alisema kitendo cha Lowassa kuhamia chama hicho kwa haraka kilileta mashaka na mijadala kwa baadhi ya viongozi.
“Ninavyojua mimi ndani ya Chadema kuna watu wenye misimamo na wapo tayari kuilinda kwa nguvu zote, kujitoa kwake sawa na kutaka kusimamia kile anachokiamini na kukaa kwake kimya katika jambo hili lazima kutakuwa na mshindo mkuu,” alisisitiza.
Mhadhiri huyo alisema anaamini Slaa aliweza kukifufua chama hicho mwaka 2010 kwa kuweka misingi yake ya kukemea ufisadi, hivyo hawezi kurudi nyuma kwa kuivunja.
Dk. Kitlya Mkumbo kwa upande wake alisema anaheshimu maamuzi ya pande zote mbili kwani zinaonyesha demokrasia na ukomavu wa kisisa.
Alisema Dk. Slaa amechukua uamuzi sahihi wa kujiuzulu kwa sababu ni haki yake kikatiba na Chadema wamechukua hatua ya kumkaribisha Lowassa walikuwa na njia njema kukuza upinzani na kuiondoa CCM madarakani.
Kauli za Slaa Dhidi ya Lowassa
Septemba 15 mwaka 2007 katika viwanja vya Mwembe Yanga jijini Dar es Salaam, Dk. Slaa alimtaja Lowassa kuwa miongoni mwa mafisadi 11 waliochota fedha Benki kuu katika akaunti ya Epa.
Kauli hiyo alikuwa akiitamka kila mahali alipokwenda na kusisitiza kwamba Lowassa na viongozi wenzake wa CCM wamechafuka kwa ufisadi.
Akiwa katika kampeni ya urais mwaka 2010, Wilayani Monduli Dk. Slaa alimshambulia Lowassa, kwa kushindwa kudhibiti vitendo vya kifisadi vilivyotokea jimboni na serikalini.
Akizungumza katika mkutano uliofanyika katika viwanja vya Bomani, alisema binafsi hana ugomvi na Lowassa kwani ni mmoja wa viongozi aliofanya nao kazi kwa karibu na ni rafiki yake, lakini wanatofautiana katika masuala ya msingi yanayohusu maslahi ya Taifa.
Dr. Slaa kweli mtanzania halisi mwenye uchungu na nchi hii ulikuwa na nia ya kweli kuwakomboa watanzania lakini wahaini ktk Chadema wamekuvunjia dhamira yako uhaini wa wenye tamaa ya madaraka na pesa kwa tamaa yao kutwaa utawala kutoka mikononi mwa CCM wasahau imekuwa ni ndoto ya Alinacha wataishia kunawa mikono, walikuwa wanasema CCM imepasuka kwa kumuchukua Lowassa sasa wamejipasua wenyewe na wameipa nafuu CCM kwa kuwatulia zigo.
ReplyDeleteAnaonesha msimamo, aheshimiwe
ReplyDeleteKwa kweli Mbowe na Chadema wamemdhalilisha Dr. Slaa, ataiweka wapi sura yake? Aliahidi kumpeleka mahakamani Edo, leo anakuwa 'boss' wake wataishije, atamuangaliaje huyo "boss" wake? Atamuomba msamaha au? Na-huyo mzee wa 'visasi' atamfanyaje Slaa? Hakika Slaa yupo ktk wakati mgumu, uso umeumbwa na haya....NENDA MWALIMU!
ReplyDeletekwani mnaongelea nini?
ReplyDeleteSlaa kweliumeonyeshakua nimwanasiasa WA ahadi yakweli sio mbowe mwanasiasa WA tamaa ya pesa,mzewangu Silas msimamowako mithili ya Mandela Ni lulu kwatanzania yaleo,namedaniyaheshima yako yakesho daima kwa Tanzania na dunia kwaujumla,nanimwenyesiasa namsiamokama Wako ktk Tanzania yaleo? Dahkweli wewenimwanasiasa yawanyongekweli,usiekubalikuburuzwa kwa sababu ya pesa,hongra mzee,linda heshima,lulu yaleo nakesho.
ReplyDeleteHata kama mkewe ana mlazimisha kuacha siasa sio mbaya anasababu za kufanya hivyo kwani uchungu wanao wao jinsi gani walivyo pigwa virungu na polisi kutetea haki ya chadema, na pia Mbowe kamzalilisha sana Slaha mtu aliyeitwa Fisadi leo anaingia kwenye chama chako kisa uchu wa madaraka aoumzike tu siasa awaachie wafanya biashara wakina mbowe na ikulu hamuingii hata kwa kuloga CCM itawaburuza vibaya.
ReplyDeleteSwali la kumuuliza DR Slaa,amekubalije kuwa UKAWA yaani kuungana na vyama alivyowai kuvipinga alafu ajidai anamkataa Lowassa? N a hata kwako wewe unayeshabikia,unatakiwa ujiulize hivyo,Kuwa kama unamkataa Lowassa kupokelewa Chadema basi ungekataa na kuhoji kwanini waungane hao waliokuwa wanaonana maadui?
ReplyDeleteWewe ndo ujiulize ktk UKAWA yupo fisadi kutofautiana ki sera sio sababu ya kutokushirikiana kama kuna sababu za msingi for the country interest kweli rushwa na ufisadi utakwisha kwa wadanganyika kwa staili hii ya watu kama wewe
Delete