Wema Sepetu Amtangazia Kiama Tundu Lissu......Asema Siku Zake za Ubunge Zinahesabika

MSANII maarufu wa filamu nchini,Wema  Sepetu, amemtangazia kiama mbunge wa jimbo la Singida mashariki Tundu Lissu wa CHADEMA,kwamba siku zake za ubunge zinahesabika.

Wema miss Tanzania 2006, aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya safari yake ya kisiasa ambayo ameianzisha baada ya kushindwa kwenye uchaguzi ubunge viti maalum (CCM) mkoa wa Singida uliofanyika hivi karibuni.

Alisema matunda ya safari yake ya kisiasa yataanza kuonekana kuanzi oktoba mwaka huu baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu, kwani jimbo la Singida mashariki,litakuwa mikononi mwa CCM  chama tawala.

“Mimi nimerudi Singida kwa kazi maalum, nimekuja kushiriki upigaji kura za maoni CCM.Tumemchagua mgombea wetu Jonathan Njau…..tutahakikisha Njau anamgaragara Tundu Lissu”,alisema Wema kwa kujiamini.

Akifafanua,alisema hivi sasa maandalizi ya kuing’oa CHADEMA jimbo la Singida mashariki,yameanza na yanaendelea vizuri.

Wema alisema kazi ya kuing’oa CHADEMA mwaka huu, itafanywa kwa ushirikiano wa karibu na wana CCM wote na kuungwa mkono na kundi la wasanii maarufu kutoka jijini Dar-es-salaam.

Kwa upande wake katibu wa CCM wilaya ya Ikungi, Aluu Segamba,amesema Wema ameonyesha amekomaa kisiasa kwa kitendo chake cha kurudi Singida mapema,licha ya kuangushwa kwenye uchaguzi wa ubunge viti maalum CCM hivi karibuni.

“Tunaendeleaa kushuhudia wana CCM wengi wanaoangushwa kwenye chaguzi mbalimbali,huwa na chuki na chama na wangine wamefikia uamuzi wa kukihama chama. Lakini Wema ndio kwanza mapenzi yake kwa chama yameimarika na sasa anaelekeza nguvu zake kulikomboa jimbo la Singida mashariki kutoka CHADEMA na kulirudisha CCM”, alisema Segamba.

Post a Comment

9 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Actors wote wamekukonga sasa unatafuta wanasiasa.

    ReplyDelete
  2. huyu dada kanyaboya kweli!!! kwa upuuzi wake anataka anza ingilia mambo ya maana!! akae na ujinga wake huko! yeye ni nani? mpaka kutishia watu wakubwa mambo?

    ReplyDelete
  3. Kakimbia mji anajua Dai na Zari karibu watapata mtoto. Kaamua kuingia mitini ili asipatikane na watu wa magazeti. Hilooooooooo. Kaona mambo ya Nuh yamedunda baada ya Nuh kutomwacha Shilole. Ile tv ya in her shoes nayo mushkeli. Hahahahahah

    ReplyDelete
  4. Sasa ww na hao wasanii kutoka Dar ndio nutaenda kupiga kura huko ama vp mana sijakuelewa

    ReplyDelete
  5. WEMA WELL DONE NDUGU YANGU ..USIWA SIKILIZE WATU FANYA AKILI YAKO INAVYOKUTUMA. .HAWA WATU SASA WANATAKA UFANYEJE? UWE KAMA KINA LOWASA?

    ReplyDelete
  6. nyote haters wakizaa inamhusu nini? walipovuliana nguo walimuita?
    mxxxxx acheni watu waishi maisha yao

    ReplyDelete
  7. Analolote anatafuta kiki tu

    ReplyDelete
  8. dada bwege tu huyu, hana faida yoyote na taifa hili, akae huko na upuuzi wake

    ReplyDelete
  9. Kwani utaenda na agenda gani ya kisiasa? Kuwaambia a kina dada wa Singida wabadilishe wanaume km ww unavyofanya? Na ukimwi huu
    Nakutakia kila la heri lakini huo ni ndani

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad