MSANII maarufu wa filamu nchini,Wema Sepetu, amemtangazia kiama mbunge wa jimbo la Singida mashariki Tundu Lissu wa CHADEMA,kwamba siku zake za ubunge zinahesabika.
Wema miss Tanzania 2006, aliyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya safari yake ya kisiasa ambayo ameianzisha baada ya kushindwa kwenye uchaguzi ubunge viti maalum (CCM) mkoa wa Singida uliofanyika hivi karibuni.
Alisema matunda ya safari yake ya kisiasa yataanza kuonekana kuanzi oktoba mwaka huu baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu, kwani jimbo la Singida mashariki,litakuwa mikononi mwa CCM chama tawala.
“Mimi nimerudi Singida kwa kazi maalum, nimekuja kushiriki upigaji kura za maoni CCM.Tumemchagua mgombea wetu Jonathan Njau…..tutahakikisha Njau anamgaragara Tundu Lissu”,alisema Wema kwa kujiamini.
Akifafanua,alisema hivi sasa maandalizi ya kuing’oa CHADEMA jimbo la Singida mashariki,yameanza na yanaendelea vizuri.
Wema alisema kazi ya kuing’oa CHADEMA mwaka huu, itafanywa kwa ushirikiano wa karibu na wana CCM wote na kuungwa mkono na kundi la wasanii maarufu kutoka jijini Dar-es-salaam.
Kwa upande wake katibu wa CCM wilaya ya Ikungi, Aluu Segamba,amesema Wema ameonyesha amekomaa kisiasa kwa kitendo chake cha kurudi Singida mapema,licha ya kuangushwa kwenye uchaguzi wa ubunge viti maalum CCM hivi karibuni.
“Tunaendeleaa kushuhudia wana CCM wengi wanaoangushwa kwenye chaguzi mbalimbali,huwa na chuki na chama na wangine wamefikia uamuzi wa kukihama chama. Lakini Wema ndio kwanza mapenzi yake kwa chama yameimarika na sasa anaelekeza nguvu zake kulikomboa jimbo la Singida mashariki kutoka CHADEMA na kulirudisha CCM”, alisema Segamba.
Wema Sepetu Amtangazia Kiama Tundu Lissu......Asema Siku Zake za Ubunge Zinahesabika
9
August 06, 2015
Tags
Actors wote wamekukonga sasa unatafuta wanasiasa.
ReplyDeletehuyu dada kanyaboya kweli!!! kwa upuuzi wake anataka anza ingilia mambo ya maana!! akae na ujinga wake huko! yeye ni nani? mpaka kutishia watu wakubwa mambo?
ReplyDeleteKakimbia mji anajua Dai na Zari karibu watapata mtoto. Kaamua kuingia mitini ili asipatikane na watu wa magazeti. Hilooooooooo. Kaona mambo ya Nuh yamedunda baada ya Nuh kutomwacha Shilole. Ile tv ya in her shoes nayo mushkeli. Hahahahahah
ReplyDeleteSasa ww na hao wasanii kutoka Dar ndio nutaenda kupiga kura huko ama vp mana sijakuelewa
ReplyDeleteWEMA WELL DONE NDUGU YANGU ..USIWA SIKILIZE WATU FANYA AKILI YAKO INAVYOKUTUMA. .HAWA WATU SASA WANATAKA UFANYEJE? UWE KAMA KINA LOWASA?
ReplyDeletenyote haters wakizaa inamhusu nini? walipovuliana nguo walimuita?
ReplyDeletemxxxxx acheni watu waishi maisha yao
Analolote anatafuta kiki tu
ReplyDeletedada bwege tu huyu, hana faida yoyote na taifa hili, akae huko na upuuzi wake
ReplyDeleteKwani utaenda na agenda gani ya kisiasa? Kuwaambia a kina dada wa Singida wabadilishe wanaume km ww unavyofanya? Na ukimwi huu
ReplyDeleteNakutakia kila la heri lakini huo ni ndani