Wema Sepetu Awavua Nguo Nuh Na Shilole..Baada ya Wao Kudai Sauti ya Nuhu Akimtongoza Wema si ya Nuhu Bali Wema Ametengeneza Kuwagombanisha

Lile sakata la mrembo Wema Sepetu kutakwa kimapenzi na mpenzi wa msanii mwenzake, Zuwena Mohamed ‘Shilole’, Nuh Mziwanda limeendelea kushika kasi ambapo Wema ameibuka na kuwavua nguo kwa kuwatolea maneno ya shombo.

Wema alitoa maneno hayo hivi karibuni baada ya Shilole na Nuh kumgeuka na kusema kwamba aliwachezea mchezo mchafu ili kuwagombanisha kwa sababu anawaona wanapendana hivyo alimtafuta mtu ambaye anaendana na sauti ya Nuh ili tu amharibie.

“Sijui kwa nini Wema kanifanyia hivi najua anataka tu kunigombanisha na mpenzi wangu kwa sababu hata ukisikiliza hiyo rekodi utasikia sauti ya Mirror akizungumza, hapo ndiyo ujue kuna mchezo mchafu sana na kwa hilo amefanikiwa lakini sisi huku mapenzi yetu yanaendelea,” alisema Nuh.

Kutokana na maneno hayo Wema alicharuka na kusema kwamba hawezi kutoa rekodi ya uongo na kumsingizia Nuh kwani ni mpuuzi na hawezi kujilinganisha naye kutokana na kwamba ni staa mkubwa.

“Nuh alinipigia na kunitaka kimapenzi ndipo nikaamua kumrekodi na hiyo ni sauti yake haijatengenezwa kama wao wanavyodai, kwanza nawashangaa hivi ningetengeneza sauti feki ili iweje, Nuh na Shilole siyo levo yangu ni wasanii wachanga sana, mimi ni staa mkubwa Tanzania na hakuna wa kulinganishwa na mimi labda nje ya Bongo.

"Nitafute kiki kwa kina Shilole  na Nuh kweli? Si bora nitengeneze kiki kwa kina Davido na wasanii wengine wakubwa duniani, hao si levo yangu jamani,” alisema Wema kwa sauti ya hasira.

Kabla ya kupatana, Nuh na Shilole waligombana hivi karibuni katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni baada ya mrembo huyo kupokea sauti hiyo iliyosikika Nuh akimtongoza Wema.

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Wema sio mstaarabu hata kidogo. Kurekodi mazungumzo binafsi na kuyarusha ktk vyombo vya habari bila ridhaa ya upande wa pili ni dalili za kukosa busara. Kwa mtindo huo anaweza kukosa hata mambo ya msingi kutokana na watu kuogopa kurekodiwa endapo watampigia simu.

    ReplyDelete
  2. Acheni maneno ya fitina kuzeni itikadi ya heshima katika usanii

    ReplyDelete
  3. ingekuwa wewe Anony. 6.13 PM. ungeaa kimya halafu wakaanza kukukashifu unatembea na mabwana za watu sio. wacha kuropoka kama umekunywa uji wa moto.

    ReplyDelete
  4. wema ni mpumbavu halafu ni malaya ndio maana anayafanya hao fuck of wema!

    ReplyDelete
  5. Kumbe vichwa vibovu vipo vingi km anonymous 8:13 PM. Kuna namna nyingi za kusolve tatizo km hilo. Ninazidi kuthibitisha kuwa sio kila mwenye kipara ana busara nyingi.

    ReplyDelete
  6. Asingetoa hiyo record nuh angesema wema anamtogoza. Mumkome binti sepetu wakomeshe wote low level wanaokutokea

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad