Baada ya TWAWEZA kusema CCM inakubalika 66 %, haya ni maneno 15 ya Lowassa na 26 ya Zitto Kabwe

Kuelekea uchaguzi mkuu October 25 2015 matokeo ya utafiti wa taasisi ya TWAWEZA yametolewa September 22 2015 Tanzania na kuonyesha Watanzania mbalimbali wanamkubali nani zaidi ambapo CCM imepata 66%, CHADEMA ikipata 22%, C.U.F 1%,ACT 0%, NCCR 0%, UKAWA 3%.
Baada ya utafiti huu kutoka chumba cha habari kilipitia page za Twitter za Wagombea Urais na vyama vyao kutazama kama kuna walichoandika baada ya kupata haya matokeo.

Mgombea Urais Edward Lowassa ambaye yuko kwenye tiketi ya CHADEMA ameyaandika haya kwenye page yake halali ya Twitter

 ‘Watanzania tusipumbazwe na tafiti ambazo hatujashiriki, tushiriki kwa mafuriko Oktoba 25, majibu ya kweli tutayapata‘

Dr. Magufuli hakuwa ameandika chochote kuhusu utafiti huu huku tweet yake ya mwisho ikiwa inaeleza furaha yake kwa jinsi Wananchi wa Bukoba walivyojitokeza kumsikiliza.

Wananchi wa Bukoba nimefarijika pasipo na wasiwasi kwa namna mlivyojitokeza kwa wingi kukiunga Chama Cha Mapinduzi. 

Kwa upande wa ACT Wazalendo, kiongozi wake Zitto Kabwe aliandika kwenye Twitter ‘Chama chetu kinaamini kwenye tafiti haijalishi zina matokeo mazuri au mabaya kutuhusu, tumepokea matokeo haya kama changamoto… tutaongeza nguvu yetu kuhakikisha tunapata asilimia zaidi kwenye kura‘

Our party believe in research and accept results whether positive to us or not. Our trust in @Twaweza_NiSisi work is unshakable

January Makamba wa CCM kwenye sehemu ya Tweets zake aliandika kwamba hajashangazwa na matokeo ya utafiti wa TWAWEZA sababu imeendana na utafiti na CCM ambao ulitangazwa siku chache kabla.

I'm not surprised by Twaweza poll that gave @MagufuliJP a resounding 65% against Lowassa's 25%. It is consistent with our internal research.

Tags

Post a Comment

10 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. 25th October is coming, we will surprise them. Peopleeeeeeees

    ReplyDelete
  2. Hata 25/10/15 itakuwa hakuna tofauti,Magufuli ndio anaingia Ikulu,
    yote ni kwa sababu kwa muda mfupi sisi walala hoi tuliokuwa tunaipenda CHADEMA tumerudi CCM.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kuna watu katika hii dunia ambao ni mashabiki wasio na sababu ya kushabikia wala uwezo wa kupambanua uhalisia.

      Delete
  3. WAULIZE NIGERIA TAFITI ZILIKUWAJEEEE? OCT 25

    ReplyDelete
  4. Magufuli atashinda,nasema kweli,kweli kabisaaaaa.
    Lowasa anatudanganya,anajichanganya sana,haendi kimahesabu.
    Anawaza ni namna gani ataingia Ikulu aweze kulipa hela alizopoteza kununua urais.
    SIDANGANYIKI! NIMESHTUKA.HAPA KAZI TUUUUUUUUUUUUUUUUU

    ReplyDelete
  5. KWANGU NAONA NI KICHEKESHO.. UONGO MTUPU. SISIEM ONENI AIBU BASI KHA!!!

    ReplyDelete
  6. Hapo Zito ndio kaongea la maana, lakini sio huyo 'wakujinyea".....yaani utafiti tu mnapanick kiasi hicho, je hayo matokeo yakisomeka hivyo........ sipati picha...ndio maana mnaogopewa, wazee wa fujo

    ReplyDelete
  7. Maguful anashinda kwa ushindi wa ktosha sana sababu babu wa monduli anazid kpoteza dila kila siku anaelekea kuwa mwenye ukiwa tena sio ukawa wana CCM msidanganyike na hyo aliye poteza kmbkmb zaid babu wa miaka 90 ngd Ally H Mwinyi "swali kwa watanzania wote, kama mtu anamsahau mke wake kwa jina na ni moja tu kwake je sisi watanzania zaid ya milion 40 atatukumbka na matatzo yetu yalivo mengi? jama tuwe macho hizi ni ck za mwisho ili tcje juta baadae yangu ni hayo mchana mwema CCM oyeeeeee!!!!!!!!

    ReplyDelete
  8. MABADILIKO TU,, ANAYEKERWA AKARAMBE MARIMAU

    ReplyDelete
  9. Wengi watanzania bado hawaelewi jinsi com inavyotumika n.a. mataifa mkubwa. Sis so Libya.z tanzania so Iraqi Tanzania s io Misri. Male pongezi Kikwete mliyemwokota n.a. mnazidi kimlaghai awauzie zaidi Tanzania.mmweka kinyumba kama mlivyomweka Amin. Hana mbele wala nyuma. Watanzania wanakwenda kugumu kupitia udini ambapo yeye kama mwislamu anagombanisha watu kidini. Wala hakemei. Wala hajavunja bunge la Mawaziri. Kikwete ni adui mkuu wa Watanzania inabidi aogopwe. Hana inteligensi. Anapata vizawadi vya toka kwa mabepari waliomchumbia. Aibu kwa raisi wetu kutokuona haya. Gereza lo msubiti yeye na familia yake na mawaziri anaokula nao vibaraka wa waxungu. If I a mini alikuwa Malaya. Ijui mzee ataitwa nani.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad