CCM Waituhumu UKAWA Kumwagia Mikojo Ofisi zao Tanga........Wadai Lowassa Aliahirisha Mkutano Tanga Kwa Sababu Ya Matatizo Yake

Chama cha Mapinduzi kinasikitishwa na kitendo cha wafuasi wa vyama vinavyounda UKAWA kupiga mawe na kutupa chupa, baadhi zikiwa na mikojo, kwenye Ofisi ya CCM Mkoa wa Tanga jana, tarehe 28 Septemba 2015, kabla na baada ya mkutano wao wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Tangamano, Tanga Mjini.

Kama ilivyo kawaida yetu miaka yote, CCM iliazimia kufanya kampeni za amani, zinazoheshimu sheria za nchi na utu wa wapinzani wetu. Hadi sasa, tumeweza kuwadhibiti wapenzi, washabiki na wanachama wa CCM wasifanye vitendo vya ufunjifu wa amani.

Tukio la Tanga sio la kwanza. Tarehe 27 Septemba 2015 viongozi wa UKAWA waliwapanga vijana, katika eneo la stendi ya Uyole, mkoani Mbeya ili wasimamishe msafara wa Mgombea wa Urais wa CCM na kumfanyia vurugu na kumpigia kelele ili wananchi wasimsikie vizuri.
 
Ingawa Mgombea wetu alifanikiwa kukabiliana na hali hiyo, tunaamini kwamba huu sio ustaarabu. Washabiki wa CCM pia wana uwezo wa kupanga na kufanya mambo haya, tena kwa ufanisi mkubwa zaidi.

Lakini viongozi wa CCM wa ngazi zote wamekuwa wanawahimiza wasifanye mambo haya kwasababu CCM hatuamini kwamba hiyo ni njia sahihi ya kuomba ridhaa ya Watanzania kuliongoza taifa letu na pia, kwa kuwa sisi ndio tuliokabidhiwa na Watanzania nchi hii kuiongoza, tunafahamu dhamana yetu kubwa ya uongozi wa taifa na ulinzi wa amani ya Taifa letu.

Tunawasihi wenzetu wa UKAWA kwamba, katika kipindi hiki cha kampeni kilichobaki, tufanye kampeni kwa amani ili tumalize uchaguzi kwa amani na taifa liendelee kuwa na amani baada ya uchaguzi.

Wenzetu wa UKAWA wasitufikishe mahala ambapo washabiki wa CCM watashindwa kuvumilia kuona Chama chao na viongozi wao wanadhalilishwa.

Tukio la Tanga la Ofisi ya CCM Mkoa wa Tanga kupigwa mawe limewaudhi na kuwakera wana-CCM na wapenda amani wote wa Tanga.

Hata hivyo, tumewasihi wana-CCM wasilipize kisasi. Chama chetu kina dhamana ya uongozi wa nchi na ulinzi wa amani ya nchi yetu. Wenzetu dhamana hiyo hawana.
 
Chama chetu kina uhakika wa kushinda na kushika dola, wenzetu wana uhakika wa kushindwa na wamekwishakata tamaa.

Tunawapongeza wana-CCM kote nchini kwa utulivu waliouonyesha katika kipindi chote cha kampeni.

Tunawashukuru kwa kubaini na kutoyumbishwa na propaganda za wenzetu ikiwemo ya Tanga, kwamba mkutano wa Tanga uliahirishwa kwasababu watu walikuwa wengi.

Itakuwa ni mara ya kwanza katika historia kwamba mkutano wa kampeni unaahirishwa kwasababu ya wingi wa watu. Katika mikutano ya kampeni, ikiwemo ya CCM, na hata katika sherehe za kitaifa, baadhi ya watu huzidiwa nguvu na huhudumiwa na wahudumu wa huduma ya kwanza huku mikutano ikiendelea.

Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa wenzetu kutafuta kisingizio cha kutofanya mikutano ya kampeni. Mkutano wa kampeni ya UKAWA wa Geita pia waliuahirisha kwa kisingizio tofauti, kwamba jukwaa na vipaza sauti havikuandaliwa ingawa aliyetangaza kuahirisha alisimama jukwaani na akasikika na watu wote.

Mabadiliko wanayoyahubiri wenzetu yanaanza na kusema ukweli. Imefika mahali sasa wenzetu wa UKAWA wawaeleze ukweli Watanzania kuhusu mgombea wao kushindwa kuhutubia baadhi ya mikutano au kuhutubia kwa dakika 3 kuliko kuwahadaa kwa kutengeneza matukio na vioja ili kuficha mapungufu ya mgombea wao.

Tunarudia kuwataka viongozi wa UKAWA kuacha kupanga vurugu, kuharibu mali za CCM, na kutukana wana-CCM. Tunarudia kuwataka waache kauli zao za kuibiwa kura.
 
Kauli hizo ni za kukata tamaa na kuwandaa watu kufanya fujo. Tunadi sera zetu na wagombea wetu kwa amani ili tuwape Watanzania fursa ya kuchagua kwa amani ili taifa liendelee kuwa la amani, umoja, utulivu na mshikamano mara baada ya uchaguzi.

Imetolewa na:
January Makamba
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa
Mjumbe wa Kamati ya Kampeni ya CCM
29.09.2015

Tags

Post a Comment

15 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Na hapo ndio bado hawajashinda, wakipata ushinda si wata tu 'juma nyoso' wote, MUNGU TUEPUSHIE MBALI HILI BALAA

    ReplyDelete
  2. Hao UKAWA ni wavuta bangi, SUGU TYPE .......msitarajie ushindi, UWANJA WETU, MPIRA WETU, REFA WETU ..........mpooo

    ReplyDelete
  3. makamba hahahahaha poleeeeeeeee

    ReplyDelete
  4. Jamani kwa akili yangu Lowasa hawezi kuwa Raisi,
    Atamuongoza nani kwa kusema nini wakati kwenye kampeni tu anasaidiwa na kukumbushwa maneno ya kuongea?Ataweza kuwa amiri jeshi mkuu kwa kukagua jeshi letu sikivu na pendwa la TZ wakatI hata kusimama dakika 10 hawezi?Mwanajeshi hajapata kazi pasi kuwa na afya njema,naamini na Rais hivyohivyo,Inaingia akili kweli jamani huyu mzee wetu kushika nchi kwa hali aliyonayo?Ugonjwa ni mapenzi ya Mungu,lakini kuna sababu gani ya kumsimamisha mgonjwa wakati wenye afya njema wapo?Kwa hapo Mbowe na wenzako mlibugi sana kumuweka Lowasa awe mgombea Urais.Mstafute mchawi wala nini ccm itashinda PIGA,UA.Napenda mabadiliko lakini mmmmmh!Tukaneni tu lakini ukweli ndio huo.
    MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Funga domo lako Hilo hizo sh 10000
      Zinakubabaisha

      Delete
  5. We shakila huna lolote unataka kusema watu wore hao niwanywa viroba na kqma ndivyo chanzo ninani mpaka vijana wakae vijiweni na kunywa viroba serekali yako ya ccm haikuwaona nakuwadhibiti wakijua Sabah item gene sea Bomu wenyewe tafaksri ndio ufunguo dojo lako kenge wewe

    ReplyDelete
    Replies
    1. Asante kidoo
      Wote vimada wa CCM
      Wamezoea tangu kampeni na bungeni

      Delete
  6. NA CCM KWA MATUSI NA UDHALILISHA JEEEEEEEEEEE ?KWELI MKUKI KWA NGURUWE TULIE NA BADO.NA CHAMA CHENU CHA UKOO, ALIANZA BABU,AKAJA BABA,MTOTO,NA WAJUU SASA MUDA WENU UMEISHA MKATAFUTE KAZI ZINYINE.

    ReplyDelete
  7. NYAMBAFUUUUU, UONGO TU RED CROSS TUMESHUHUDIA KWENYE ITV WA KIKIRI HAWAJA PATA KUONA UMATI KM ULE,TUMESHUHUDIA WATU WALALA WAMEZIMIA HALAFU NYINYI CCM NI WAONGO BAHATI SIKU KUNA MITANDOA ULIPO TUPO,HADANGANYI MTU HAPA.TUNAJUA ROHO ZIMEWAUMA FULL MUSIC KUCHANGANYIKIWA POLE MAKAMBA.NA CCM YENU YA KURITHISHA.

    ReplyDelete
  8. CCM wenyewe wanatafuta sababu
    Mmetupa chupa wenyewe Kwani hatujui

    Tangu lini January kawa msemaji wa chama

    ReplyDelete
  9. Haiendi jimboni kwenye kampeni
    Hehe mna habari yeye ni waziri mdogo wizara ya mtandao
    Keshajua ccm wataiba kura anafanya Kazi na Watu WA IT waibe kura ole wenu hata sisi ni my IT tena tunajuwa kuhack na kuona Kila kitu ole wako January
    Tutaanika bbc, CCM, na alijazera

    ReplyDelete
    Replies
    1. hata uanike ulimwengu mzima haitakusaidia ccm itashinda tu

      Delete
  10. siku zote nilikua naamini kabisa kua January makamba ni Raisi wa TZ from 2025 lkn sasa anazikwa kisiasa bila ya yeye kuwa na Tafakuri. Kama Bunge la Katiba lilivyokua kaburi la Sita kisiasa, kamati kama hizi ndio zitammaliza mtu makini January Makamba.

    Usikubali kuhubirishwa Afya za watu kwa kua Afya ni miongoni mwa neema za Mungu. Yeye anaweza kuichukua wakati wowote. Wangapi wazima kama makongoro na Nape wanakufa wakati wagonjwa wanabaki????

    Ni vyema ukachunga ulimi wako kwa kua dhihaka hii ya kuhubiri afya ya Lowassa kila siku ina majibu kutoka kwa Mungu.............wacha tuone.

    ReplyDelete
    Replies
    1. mgojwa ni mgojwa tu akanye mbele ikulu haingii anaye jinyea ovyo

      Delete
  11. HATA MSEME VIPI UKAWA WANACHUKUA NCHI. LOWASA HATA AWEJE NDIO RAIS MTARAJIWA!!! PEOPLES POWER!!!!!

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad