CCM Wamekosea Kutumia Neno na Logo ya M4C Kumnadi Magufuli

Tangu jana kumekuwepo na mijadala sehemu mbalimbali kuhusiana na matumizi ya logo ya M4C kwa chama cha Mzpinduzi (CCM). Wengine wakisema ni sawa lakini wengine wakisema si sawa.

Sikutaka kulizungumzia hili lakini naona kuna upotoshaji (wa makusudi) unaoendelea, hivyo nimeona nitumie uzoefu wangu ktk taaluma ya Mahusiano (Public Relations) na uelewa mdogo wa Sheria nilionao kutoa ufafanuzi juu ya jambo hili.

Lakini kabla sijaendelea nimpongeze sana mwanasheria wa CHADEMA John Mallya kwa kutoa msimamo wa Chama kuwa wataifikisha CCM mahakamani kwa kitendo cha kurudufu nembo yao.

Kwa uelewa wangu kinacholalamikiwa si logo tu, kinacholalamikiwa ni kitendo cha CCM kutumia nembo ya utambulisho ya chama kingine (Corporate Identity) ya CHADEMA, while are two oponent parties.

Muaasisi wa Taaluma ya Public Relations, Arthur Page alisema ili kutengeneza utambulisho wako kwa jamii (Corporate Identity) unahitaji kuwa alama zitakazokutambulisha.

Alama hizo ni pamoja na Nembo (Logo), Jina (brand name), Rangi (corporate colour), Mundo wa maandishi (designing) kama ilivyo Cocacola, etc.

Vyote hivi ndio vinatengeneza kinachoitwa utambulisho wa kampuni/shirika/asasi/chama etc.

Nembo ya M4C ni Corporate Identity ya Chama cha Demokrasia na maendeleo na imesajiliwa hivyo. Kwa hiyo CCM au chama kingine kutumia nembo hiyo bila ridhaa au makubaliano maalumu na CHADEMA ni kosa kisheria (Criminal Fraud).

KWANINI CCM WAMEKOSEA.

Sheria zinazolinda haki miliki Tanzania (The copyright and neighbouring Act, ya mwaka 1999 na The Trade and Service marks Act, ya mwaka 1986) pamoja na Sheria za kimataifa zinazolinda haki miliki zinataka kuwe na utouti wa utambulisho kati ya asasi moja na nyingine, bidhaa moja na nyingine, shirika moja na jingine etc.

Utofauti huo unakuwa kwenye maeneo mengi lakini kwa uchache ni kama ifuatavyo;

1. Jina/Brand name.
Jina moja haliwezi kutumiwa na asasi mbili tofauti zinazofanya kazi za kufanana. Kwa mfano Kampuni ya bia ya TBL ikizindua kinywaji kiitwacho "Burudani" kampuni ya Serengeti haipaswi kuanzisha kinywaji chenye jina kama hilo. Sheria inazuia ili kutowachanganya wateja na kulinda haki ya mwanzilishi wa hiyo "brand name".

Kwa hiyo kitendo cha CHADEMA kusajili nembo ya M4C kama "operation brand name" yake kinazuia chama kingine cha siasa kutumia jina hilo. Kwa hiyo CCM kutumia M4C ni kosa kisheria.

2. Muundo/Designing.
Muundo wa maandishi una hati miliki kisheria. Kwa mfano muundo wa neno Cocacola ulivyo ni tofauti na muundo wa neno Pepsi. Cocacola wanaandika kwa kucharaza. Hiyo ni designing yao. Pepsi hawaruhusiwi kuiga muundo huo unless kuwe na makubaliano maalumu na Cocacola.

Sasa CCM kwa ujinga wa kiwango cha "PhD" wameiga muundo wa neno M4C. Bora hata wangeandika kwa muundo mwingine, kwa mfano M-FOR-C, au m4c au namna nyingine itakayotofautisha brand name yao na ya CHADEMA. Lakini wamecopy na kupaste. Hapa haihitaji degree ya sheria kujua kuwa CCM wamekosea.

3. Rangi/Corporate colour.
Unaposajili bidhaa yako au kampuni yako ni vizuri kusajili na rangi yako ya utambulisho.

Kwa mfano hati ya usajili ya Chama cha mapinduzi inatambua rangi za kijani na njano kama rangi zao za utambulisho (corporate colour). Chadema rangi zao ni Blue, nyekundu, nyeupe na nyeusi.

Ukisajili rangi yako ya utambulisho ni kosa kisheria kutumia rangi ya mshindani wako hasa kwenye ulimwengu wa leo wa ushindani wa kimasoko wa "Oligopoly Marketing"

Simba hawaruhusiwi kuvaa jezi za Njano kwa sababu sio rangi yao ya utambulisho, vivyo hivyo Yanga kuvaa nyekundu.

Japo Sheria inatoa ruhusa kubadili rangi ikiwa unaona kuna haja ya kufanya hivyo. Yani ukiona "clients" wako au "audience" wako hawaridhiki na rangi yako unaweza kubadili kwa kufuata taratibu za kisheria. Na si rangi tu bali hata logo au muundo (design).

Ndio maana Vodacom ilianza na rangi ya Blue na nyeupe, lakini wakachange na sasa wanatumia nyekundu na nyeupe. Sheria inaruhusu kubadilisha.

Lakini CCM hawakufanya hivyo. Bado hati yao ya usajili inaonesha rangi zao za utambulisho ni Kijani na Njano, lakini leo wamekurupuka kutengeneza logo ya M4C kwa rangi ambazo si zao. CCM hawana utambulisho wa rangi nyekundu, blue, nyeupe wala nyeusi. Wamezitoa wapi?

Haihitaji elimu ya sheria kujua hawa watu wamekurupuka. Yani baba Njano, mama Kijani halafu mnazaa mtoto mwekundu au mweupe.. haya ni maajabu ya 8 ya dunia.

Haiwezekani baba awe Punda, mama awe Nyumbu halafu mnazaa mtoto Twiga?? Hakuna "cross genetics" ya aina hiyo. CCM u have proved failure.

Nisiwachoshe sana lakini kwa kifupi CCM wamekurupuka mno. Ni kukosa umakini kwa kiwango kikubwa. CCM ina wataalamu wa Sheria, ina wataalamu wa PR and Marketing, ina wataalamu wa Communication, kwanini wanafanya "Technical Mistake" ya kitoto namna hii? Hizi ndio akili za kushauriwa na kina Lusinde (standard seven) na kupuuza wataalamu. Poor u.!

Malisa GJ.
Tags

Post a Comment

7 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Usitake kutuchanganya na ukereketwa wako hapo hakuna makosa yoyote kama ulivyoelezea nembo ya Chadema ni moja iliyokuwa na alama ya V Magufuli hakutumia Movement for Change amesema Magufuli for Change haina matiki yoyote itakayosababisha mkose kura hamkubaliki hamkubaliki ni mbaazi ikosapo maua husingizia jua yaani roho wasiwasi kila kitu chenu kwa uroho wa madaraka subirini October 25 msiwe na jaziba

    ReplyDelete
    Replies
    1. ukiona hivyo ujue sisiem maji yamewafika shingoni wanatapatapa!!!!!

      Delete
    2. kwanini wasibuni ya kwao??????

      Delete
    3. MAGUFULI ALIONGEA KWA UTANI TU SASA KWANINI NDUGU MNAPANIKI MBONA TAYARI USHINDI NI WA UKAWA HATA MTABIRI ALISHASEMA HAPA TATIZO LIKO WAPI

      Delete
  2. wamekosea tu hata uwatetee vipi ina maana hawakuona kama wamekopy na kupaste!!? yaani wanashangaza kwa kweli au ndio kujifanya chama dume kwamba lolote watakalo wanafanya!!? waache ukandamizaji kwenye kila kitu lo!!!

    ReplyDelete
  3. wakopi wapesti ukawa hamna nyimbo raisi hana sera wa nini bora jeshi lishike nchii

    ReplyDelete
  4. mfamaji haachi kutapatapa jamani mara ccm wametufanyia hivi inamaana hakuna vyam vingine vya upinzan mpo nyie tu nyie ukawa sijui ukiwa ndo manamasikio mengi kuliko vyama vingine mkafie mbele tena octt 25 baada yahapo najua mtazungumza mengi zaidi ya haya tumewacho kila kitu mna lalamika kama mna uhakika wakushinda kwa nini mlalamike mfyuuuuuuuuuuuuu kwendeni zenu huko magufuli ikulu ni yako baba acha watapetape oct 25 tunawasubiri

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad