CHADEMA Wadai Vijana Walioandamana Kumsisitiza Lowassa Amjibu Dr Slaa Walitumwa na CCM


Baada ya maandamano ya jana kumsisitizia mgombea urais kupitia CHADEMA 'Edward Lowassa' kujibu kauli za Dkt. Slaa alizotoa siku ya Jumanne, Katibu mkuu baraza la wazee taifa Bw. Roderick Lutembeka alifafanua zaidi suala hilo leo alipoitisha mkutano na Waandishi wa habari.
"Asante waandishi wa habari kwa kuitikia wito, jambo la msingi la kuwaita ni kutoa ufafanuzi kwa tukio la jana na kutoa tamko kama baraza la wazee kwa kukemea kitendo cha uvamizi katika ofisi ya CHADEMA makao makuu ambao walitumwa na Viongozi wa chama tawala CCM, viongozi wa chama tunakemea kwa kitendo cha kihuni na kihalamia kilichopangwa kupotosha amani na vijana waliodai wametumwa na viongozi ndani ya chama tawala kwa kupewa hela kuanzia sh 1000 hadi laki moja ili wavae sare za CHADEMA na kufanya maandamano kuelekea makao makuu ya chama eti kumshinikiza mgombea wa CHADEMA  ajibu hoja za Dkt. Slaa, vijana hao wakiwa kwenye sare za Chadema waliowatuma kuelekea makao makuu ya chama kufanya vurugu, tunashukuru kwa nia hiyo kwa viongozi wa CCM waliowatuma haikuweza kufanikiwa kutokana walinzi wa chama na majirani kuwathibiti waliokuwa maeneo ya ofisi, baadhi ya vijana walikamatwa na kuhojiwa na chama na  baadae kuthibitisha walipewa hela na kiongozi mmoja wa chama tawala jina tunalihifadhi ili wafanye maandamano hayo, chama kina ushahidi wa kina... Pamoja na kitendo hiki baraza la wazee tunaomba tume ya uchaguzi itoke hadharani na kukemea kitendo hiki cha aibu na kuashiria kuvunja amani kipindi hiki cha uchaguzi.
Tunawaomba wananchi wote kuwa tayari kutoa taarifa juu ya mipango yote miovu inayopangwa na watu kutaka kuvuruga amani na kutoa taarifa mapema." Roderick Lutembeka

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad