DK. Slaa Awavaa Maaskofu Waliojitokeza Kumjibu Kuhusu Kuhongwa Na Lowassa


Aliyekuwa Katibu mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA Dkt. Wilbroad Slaa amedai kusikitishwa na kitendo cha baadhi ya maaskofu kujitokeza kujibu hoja yake juu ya maaskofu kuhongwa bila kusikiliza hotuba yake.Akizungumza katika kipindi cha mahojiano maalam, Dkt. Slaa ambaye amesisitiza kauli yake aliyoitoa wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa baadhi ya maaskofu hao wamejibu hoja yake kwenye vyombo vya habari wakati akidai hawakusikiliza hotuba yake.
Ametumia muda huo kujibu baadhi ya hoja ambazo zimeibuliwa na wachambuzi wa masuala ya kisiasa, Wasomi na Wanasiasa kwa ujumla tangu atangaze kuachana na siasa.
Amesema kuwa amezungumza na kiongozi mmoja wa dini, ambaye amesema amekiri kutosikiliza hotuba yake licha ya kujibu hoja yake.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad