Edward Lowassa Kuiteka tena Dar es Salaam LEO

MGOMBEA urais wa Chadema na anayeungwa mkono na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), Edward Lowassa anatarajia kuliteka tena Jiji la Dar es Salaam leo  katika mikutano mitatu.

Lowassa anarejea tena jijini Dar es Salaam mara baada ya kufanya mikutano kwenye majimbo ya Kawe na Kibamba Septemba 7 mwaka huu na kunadi wagombea wa majimbo hayo.

Lowassa alimnadi John Mnyika wa Kibamba na Halima Mdee wa Kawe kabla ya kuelekea visiwani Zanzibar katika uzinduzi wa Kampeni za Urais za Maalim Seif wa CUF.

Jijini Dar es Salaam leo Lowassa anatarajia kufanya mikutano yake katika Jimbo la Ukonga, Kigamboni na jimbo jipya la Mbagala ambapo maandalizi tayari yamekamilika.

Lowassa ataanzia Jimbo la Kigamboni saa 3:00 asubuhi, saa 6:00 mchana atakuwa katika Jimbo la Mbagala na atamalizia kwenye Jimbo la Ukonga saa 9:00 alasiri.

Sambamba na viongozi wengine Lowassa ataambatana na timu nzima ya kampeni ya UKAWA akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu, Fredrick Sumaye; aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Shinyanga, Hamis Mgeja; meneja wa kampeni John Mrema pamoja na mwenyekiti wa Chadema-Taifa, Freeman Mbowe.

Lowassa anaingia Dar es Salaam akiwa tayari amezunguka kwenye mikoa 15 ya Tanzania ikiwemo Dodoma, Geita, Kagera, Geita, Shinyanga na Iringa huku mikoa ya Lindi, Mtwara, Pwani, Arusha na mingeneyo ikiwa bado kufikiwa.

Post a Comment

3 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. GOD BLESS YOU. YOU WILL BE NEXT PRESIDENT OF TANZANIA

    ReplyDelete
  2. TULIKUWEPO LEO HII JUMAPILI TAREHE 20 SEPTEMBA 2015.TUKIANZIA KIGAMBONI.SHUGHULI ZILIANZA SAA TATU ENEO LA WAZI WANAPOPAITA MNADANI TUNGI.MHE.LOWASSA ALIWASILI SAA 8.ULE UMATI KAMA WA MBEYA,ARUSHA,AU BUKOBA MJINI JANA.VIMBWANGA KEDE KEDE.ALIYEBAKI NYUMBANI AWE LABDA MGONJWA.MAELFU,MAELFU,MAELFU.TUJE MBAGALA PALE UWANJA WA MIKUTANO ZAKHEM.UMATI MILLION MBILI KAMA PALE JANGWANI TAREHE 29 AUGUST 2015.MHE LOWASSA ALIFIKA SAA 11.ULE UMATI ULIMSHANGAZA MHE.SUMAYE KWA MSHANGAO AKAHOJI 'MI NAONA MHE.LOWASSA AKIKARIBISHWA BASI NA AFUNGE MKUTANO.HAKUNA TULICHOBAKIZA UKAWA IMECHUKUA DOLA TAREHE 25 OCTOBA 2015'.MHE.LOWASSA ALIPOSIMAMA AKAGEUKA KUWAANGALIA VIJANA WALIOUSHONA MNARA WA VODACOM UREFU MITA 200 NA BENDERA ZAO NA NYIMBO ZAO..JAMANI TUSIKIENI, KWA JINA LINALOSTAHILI UTUKUFU WOTE LA MWENYEZI MUNGU, MHESHIMIWA LOWASSA ANASHINDA UCHAGUZI MKUU 25 OCTOBA 2015 TENA KWA KISHINDO KWELI KWELI UTAFIKIRI UCHAGUZI WA CHAMA KIMOJA WA KURA ZA NDIO AU HAPANA.

    ReplyDelete
  3. na kwa ushuhuda huo sasa,tunashauri na kuomba tuanze sasa kuunda kamati mbali mbali za ushindi wa kishindo wa ukawa tukianzia vitongoji,kata,wilaya,sheha,mikoa na kamati kuu ya sherehe ya kitaifa ili ikifika ile siku ya sikukuu ya kuapishwa mheshimiwa lowassa sherehe zetu 'za karne' zifanyike kwa amani,utulivu,heshima na maelewano pasi na kusababisha maafa.tunaamini hata hivyo kuwa wapo watakaozimia kwa mishituko ya aidha ushindi au kushindwa,wapo watakaokimbizwa hospitali hawajiwezi na wapo watakaofunguliwa mafaili mirembe.kamati hizi ziombe ushirikiano wa mapema na polisi na hospitali mbali mbali.bila tahadhali hii kupewa umuhimu kwa sasa na leo hii basi tutegemee matatizo makubwa,mazito hususani kwa wale wana ccm walio wapinzani wakuu wa mabadiriko.athari kubwa sana zitawatokea-tuanze kuwaonea huruma,tuje tuwasaidie kuwapeleka hospitali.uchaguzi utakua umepita,na tutapaswa kurejea na umoja wetu ili tuijenge tanzania mpya ya lowassa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad