Joseph Musukuma Amshambulia LOWASSA........Asema Alijisaidia Hadharani Pale Chato. Tazama Video hii

Joseph Msukuma
MWENYEKITI wa CCM mkoa wa Geita, Joseph Msukuma amemvaa mgombea wa urais kupitia Chadema, Edward Lowassa na wengine waliohamia Ukawa akisema wanashukuru chama kimetua mzigo.

Msukuma, ambaye anaaminika kuwa swahiba wa Lowassa wakati wa mchakato wa kura ya maoni kwenye CCM, aliuambia mkutano jana kwamba hakuna anayefahamu siri za Lowassa.

“Nataka nimwambie ndugu yangu, rafiki yangu Lowassa, huu ni muziki mkubwa,” alisema Msukuma kwenye mkutano wa kampeni wa mgombea wa urais wa CCM, Dk John Magufuli uliofanyika jana mjini Chato, mkoani Geita.

Msukuma ambaye aliponda waliohama CCM baada ya kura za maoni kwa kutaja majina ya baadhi, akiwalinganisha na bendera inayofuata upepo na kusisitiza kuwa wenye akili hawahami.

“Tumeshukuru sana CCM tumetua mizigo…”, alisema Msukuma ambaye ni mgombea ubunge, Jimbo la Geita Vijijini akiwataja Lawrence Masha, Msindai, Mngeja akisema wamehamia Ukawa si kwa mapenzi mema isipokuwa, ni kutokana na kukosa ushindi kwenye kura za maoni.

“Tuna hasara gani Masha akihama CCM?” alihoji umati ambao uliitikia kwa kusema hakuna hasara.

Msukuma ambaye alikuwa miongoni mwa viongozi wa CCM waliohudhuria mkutano wa Lowassa uliofanyika Arusha wakati wa mchakato wa kura za maoni, akisifia mkutano wa jana wa Magufuli, alisema, “Toka niwe mwenyekiti sijawahi kuona watu wengi kama hawa. Hata nilipoteremka Arusha na chopa, haikuwa hivi.”

Alieleza kushangazwa na baadhi ya picha zilizooneshwa kuwa ni za mkutano wa Lowassa mjini Chato na kusema mandhari iliyooneshwa, haikuwa ya uwanja huo wa stendi.

“Stendi ya Chato haina miembe wala lami,” alisema. Akiendelea kuponda waliohama, alisema, kama Dk Magufuli angekuwa anatoa rushwa, wasingehama.

“Hakuna hasara na wote waligombea wakashindwa,” alisema na kueleza kumfahamu Mngeja kwa kuwa walikuwa wakikaa kwenye helikopta moja.

“Tunaomba wachukue na wengine wenye tabia kama hizo. Wenye akili timamu tutabaki CCM...Mgombea wetu (Magufuli) anatosha. Na hapa ndiyo kwao…nimetembea na Lowassa gari moja, ndege moja, tunachagua rais na sio bora rais…,” alisema.

Alisisitiza, “Katika Kanda ya Ziwa, hakuna aliye na siri za Lowassa kama mimi…naomba waniweke kwenye mdahalo nitagharimia, niwapige kavu kavu. Watu wanaokwenda kule (Ukawa) zinatangulizwa hela. Nani anachukia hela?.”

Aliendelea kusema, “najua mengi ya kambi ile nilikwenda kufanya kazi. Hata wale wachungaji waliokwenda Dodoma, ni wachungaji feki walionunuliwa.”

Baada  ya  hapo, Msukuma  aliwauliza  maelfu  ya  wananchi  kuwa...." Mgombea  wa  UKAWA  alifanya  nini  pale  stendi?"......Wananchi  Wakamjibu...."Alijinyeaaaaa"

Msukuma akasema, "Sijasikia", Wananchi  wakajibu...."Alijinyeaaaa".

Akasema  tena, " Alijinyee......!!!". Wananchi  Wakamalizia..."aaaaaa" 

Zaidi, Tazama  video  hapo  chini  kumsikiliza
Tags

Post a Comment

18 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tutasikia mengi mwaka huu,MUNGU IBARIKI TANZANIA.

    ReplyDelete
  2. Siasa za majitaka hazitusaidii wananchi

    ReplyDelete
  3. WANASHINDWA MAPEMA NDIO MAANA WANALETA SIASA ZA MAJI TAKA.

    ReplyDelete
  4. mpuuzi mtupu badala yakuleza sera za maana umekaa jukwaani kuongea utumbo.Uchafu mtupu Ccm😂

    ReplyDelete
  5. aibu kwa taifa nonsense ,a leader like this guy give a speech like this is sign of poor education.,ni sawa na yule waziri alidai TANZANIA ni muungano wa visiwa vya Zanzibar na Zimbabwe,kiongozi wa taifa unaongea hivyo dunia inakusikiliza ,.

    ReplyDelete
  6. aibu kwa taifa nonsense ,a leader like this guy give a speech like this is sign of poor education.,ni sawa na yule waziri alidai TANZANIA ni muungano wa visiwa vya Zanzibar na Zimbabwe,kiongozi wa taifa unaongea hivyo dunia inakusikiliza ,.

    ReplyDelete
  7. Nchi Hii wamejaa Viongozi Wazee wasiojiendeleza. CCm Viongozi hawa Wamepataje Vyeo. Matusi yasioyo na hadhi. Yeye hana hadhi. Kajivua mpaka chupi yake mwenyewe kwa Mtindo huu. Viongozi wa CCM kama hawa ndio wanaomalza Kodi za Wananchi kwa upumbavu, ujinga, ubabe, dharau na nguvu. GAME CHANGER. Ukikubali kutawaliwa kiubabe na wajinga wasio na sera wasio na hadhi, adabu, ustaarabu. pigia CCM.
    IKULU SASA NI YA WAZALENDO. UKAWA IKIONGOZWA NA CHADEMA. KWA HERI CCMIZI.
    KARIBU PEOPLES POWER TANZANIA. THE PEOPLE HAVE SAID.
    HITORIA MPYA INAANDIKWA TANZANIA BAADA YA MIAKA HAMSINI NA TATU. INAANDIKWA NA WATU WAKAWAIDA. NAPENDA MAGEUZI. NAIPENDA CHADEMA. NAPENDA UKAWA. NAMPENDA LOWASA na MAMBO YAKE YOTE.
    NAPENDA MABADILIKO MAZURI, NAIPENDA NCHI YANGU TANZANIA.WAKATI NDIO HUU.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Tunachohitaji ni mabadiliko tu,miala 53, tunadanganywa kama watoto,peoples!!!!!! Power

      Delete
  8. Disgraceful. Bad Taste, Siasa chafu, Potufu, Hazina hadhi. Aibu, utaongozaje watu namna hii? Huna sera yeyote. Huna sfa yeyote ya Uongozi. Hivi CCM hamna viongozi wenye sifa? Akili timamu mavi matupu. BLAAA Blaa. Hivi umesoma? ni wewe Kajifunze kuongea badala ya Utumbo. Magufuli unaviongozi Mzigo. Raisi hawezi kuongoza kama Wabunge ni hawa wasio na akil. Si hela bali ni Elimu. Huna elimu. Wote wanaokushabikia jinga tupu. Raisi ni LOWASSA. Magufuli hapiti. Hizi Taa na Rami ni pesa za mali ya umma si za CCM. Akina mama mashangingi ndio wanaochekelea hapo. Mwenye akili angeficha Uso au kuondoka mkutanoni. Umekidharalisha chama chako au CCM hakuna hadhi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe Tanzania hakuna Raisi ila yupo Rais!
      Sasa kama wewe na wenzio mnamchagua lowasa awe Raisi wenu sisi watanzania tutamchagua Magufuri kuwa Rais wa Tanzania.
      Wewe baki na huyo raisi wako!

      Delete
    2. sheria moja wapo ya NEC mgombea haruhusiwi kutumia lugha ya asili( kabila lake) ila huyu kijana katumia lugha ya kisukuma, CCM mbona mnaishiwa sera, ccm inatosha mmeshatudanganya vya kutosha, tunataka mabadiliko, UKAWA juuuuuuuuuuuuu. vote for LOWASA

      Delete
  9. Namalizia kwa kusema hv, CCM MMEZUSHA YOTE MMEBAKIZA KUSEMA LOWASA AMEKUFA, HATA AKIFA TUTACHAGUA MAITI YAKE..... SEMENI LINGINE

    ReplyDelete
  10. kiongozi unaongea kampeni za matusi namna hii na kuna video nimeona mdada anaongea kumbe wewe kiongozi ndo umetengeneza trcu mko wapi kwa mtu kama huyu jamani.siasa gani hizi usiharibu demokrasi yetu kwa matusi yako

    ReplyDelete
  11. Kumbe kuna mtu alijinyeeeea!Ndio kwanza naiangalia hii vidio,du kama ni kweli alishikwa na tumbo la kuhara wakati muda wa kuhutubia ulishafika.Ila wasaidizi wake walitakiwa kuja na ile aliyovaa mke wa sugu siku ya kuzaliwa kwake ili kumsitiri.

    ReplyDelete
  12. KILA CHENYE MWANZO HUWA NA WISHO,CCM NDIO WAMEFIKA MWISHO, LAAANA NA USHIRIKINA ZINA WAANDAMA WAO NA VIZAZI VYAO.KUNA SABABU GANI KUDHALILISHA MTU KISA MADARAKA,TUTAONA MWISHO WENU,ETI HIYO NI KIONGOZI WA CCM NA MGOMBEA UBUNGE WA CCM KWELI WOOTE NI LAAANA TU.HAWA NDIO WATALETA MAENDELEO KWELI?

    ReplyDelete
  13. HARAFU HUYU BULEMBO AMEMALIZA HATA LA SABA?KWELI YAAANI SIJAJUA HUWA CCM WANAWAZA NINI,ETI NDIE MWENYEKITI WA KAMPENI NAMUONA NAE MSWAHILI TU NA MSHIRIKINA KAMA BOSSI WAKE.

    ReplyDelete
  14. kwani pampus zinakazi gani, tutamvisha mzee, na mchakato utaendelea ilimladi mabadiliko yatimie

    ReplyDelete
  15. Hapa ni mabadililko tu,miaka 53, tunadanganywa kama watoto,peoples!!!!! Power,mabadiliko,,,,,,,Lowassa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad