Kauli ya NAPE Baada ya Wanachama Wengine 3,000 Kutoka Jimboni Kwake Mtama Kurudisha Kadi za CCM na Kujiunga na Chadema

KATIBU wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, amesema kadi za chama hicho alizokabidhiwa Mgombea wa urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Edward Lowassa akiwa Jimbo la Mtama si za kweli, bali mpango uliotengenezwa ili wajipatie umaarufu.

Nape alisema hayo wakati akizungunza na mwandishi mjini Morogoro juzi mara baada ya uzinduzi wa safari ya wasanii wanaounda kundi la NimEs’tuka Hapa kazi tu, linaloongozwa na Aunty Ezekiel na Vincent Kigosi ‘Ray’ uzinduzi uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Kiwanja cha Ndege Manispaa ya Morogoro.

Septemba 23, mwaka huu wakati wa mkutano wa kampeni za Mgombea wa urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chadema, Lowassa katika kundi la vyama vinne vinavyounda Ukawa ambapo pamoja na mambo mengine, ilidaiwa kadi 3,000 za cha CCM zilipokewa kutoka kwa wanachama na kuunga mkono Ukawa.

Kwa mujibu wa Nape, wakati kadi hizo zinapokelewa na Waziri Mkuu mstaafu aliyehamia Ukawa, Frederick Sumaye, yeye hakuwepo jimboni, bali alikuwa katika shughuli za kampeni za chama chake nje ya mkoa.

Kadi zote waliozipokea ilitokana na kutengeneza shoo, zote zilikuwa ni mpya hakuna hata moja ya zamani, kwa maana ni mpango mzima wa kutengeneza shoo na Sumaye ndiye alizipokea si mgombea wa urais wa Chadema,” alisema Nape na kuongeza: 
“Hii yote inamaanisha kuwa wananiogopa, binafsi sikuwepo...nilikuwa kwenye kampeni kwa wagombea wa chama changu .

Kuhusu uzinduzi huo, alisema wasanii hao ni miongoni mwa waliorejea CCM kutoka Ukawa, watazunguka nchi nzima na watapita kila kona ya Tanzania kuwaambia wananchi na vijana nini walichoona wakiwa Ukawa.

Naye Aunty Ezekiel akizungumza mbele ya umati wa wananchi waliokuwepo uwanjani hapo, alisema Ukawa hali si nzuri na kwamba alichambua mchele na pumba ndiyo maana ameamua kurudi CCM.
Alisema mgombea wa urais wa Ukawa, Lowassa amekuwa akihubiri kutaka mabadiliko bila kazi tofauti na mgombea wa urais wa CCM ambaye anahimiza kufanya kazi.
Naye Kigosi ‘Ray’ alisema ameamua kurudi CCM baada ya kuona kuna vitu ambavyo hawavipati kule Ukawa ambavyo vipo ndani ya CCM na alichokiona kikubwa ni siasa za hadaa tupu ‘magumashi.’
Tags

Post a Comment

20 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Tusuburi tarehe 25 October
    Tutajuwa Kama Bao la mkono au la

    ReplyDelete
  2. MUNGU IBARIKI TANZANIA,IBARIKI CCM,MBARIKI MAGUFULI.
    HAPA KAZI TUU!

    ReplyDelete
    Replies
    1. MUNGU TANZANIA UKAWA CHADEMA LOWASA. MABADILIKOOOO!!!!!!!

      Delete
    2. USHABIKI WA KISIASA USIO NA SABABU NI TATIZO LINALOIKABILI JAMII YA TANZANAIA WATU HAWAFIKIRI KABLA YA KUSEMA. WATU HAWAPIMI KAULI WATU WANAABUDU NA KUKUMBATIA CHAMA KAMA NDIYO MUNGU WAO.

      Delete
  3. hata wakimfufua MIchael Jackson kuja wapigia kampeni, sisi vijana hatubadiliki, kura ni LOWASSA tuu, hao wasanii njaa akina kigosi ndiye watatubadilisha?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hakuna bao la mkono,ni haki tu.
      CCM itashinda kwa kishindo,MSIANDAMANE.

      Delete
  4. Wewe peke yako mimi kijana team Magufuli hapa kazi tuuuuuu,,, lowasa hana mpya unataka mabadiliko mgombea hana mvuto hata wa speech,, ni shiidaaaa

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe ni kijana uchwaraaa!!

      Delete
    2. Ukikuta kijana anashabikia CCM mpaka leo chunguza sana utagundua kuwa ni aina ya watu wanaopenda hisani na makombo yanayodondoka kwenye meza za wanasiasa wala hawana sababu za msingi.

      Delete
  5. WASANII NJAA TU !!!

    ReplyDelete
  6. nape mimi nilitegemea kuwa rabda utakanusha kuwa hizo hazikuwa kadi halali za ccm jimboni mtama.maadam unaelekea kuzikubali kadi hizo kuwa ni halali za ccm ambazo idadi yaki imefikia alfu nne na mia nane[ 4800 ].ni nyingi,tena nyingi sana.nadhani kwa jimbo la mtama umekwishaanguka nape,ubunge na bunge ulisome magazetini.watu wa mtama hawakupedi kabisa laghai mkubwa wewe.sasa,kula hiyo jeuri yako.

    ReplyDelete
  7. Pipoooooozzzzz jamani oct 25 ifike tukawachinje safari hii hatudanganyikiiii tunataka mabadiliko lazima mshike adabu mwaka huu ili ikitokea mmerudi madarakani muwe na nidhamu.,pumbavuuuu

    ReplyDelete
  8. nape karibu kipatimu ujaribu yako kwenye kuvua samaki kwa nyavu ndogo,kwenye siasa umeaguka,umeangamia kabisaa dogo.ila kwa huo utipwatipwa wako yaania maungo ulegelege, nadhani tutakukabdhi kapu la kuchuuzia samaki.hapa kwetu tusingependa uendelee na tabia yako ya kula mirungi kupita kiasi,kwa sababu mkeo anasema ukipandisha handasi unalia kwa nguvu huku unaimba NAMPENDA LOWASSA MIMI NI MSHABIKI WAKE WA DAMU,LOWASSA OYEEEEE.sisi hapa wengine ni ma-ccm,watakudhuru.wana hasira hao,mashavu yao yamejaa kwikwi za hasira,kukojoa kila wakati,macho mekundu na kiila wakati wanajikuna sehemu zao za siri.

    ReplyDelete
  9. WEWE NAPE HUNA BAO.. GOLI LAKO LA MKONO IN NDOTO TU HATA WATU WAKO HAWAKUTAKI JIMBONI....UMEISHAKUWA LIMBUKENI, NDIO MAANA ULIKIMBIA

    ReplyDelete
  10. Kwanza hao wasanii hawajawahi kuwa UKAWA, hawana hata kadi ya chama chochote. Wanajinadi eti walikuwa ukawa tangia lini? walikuwa ukawa kwa maneno tu kwa sababu hawakuwa na kadi ya chama kimojawapo kinachounda Ukawa.

    ReplyDelete
  11. yaani,naona jumapili tarehe 25 octoba 2015[tumebakiza`siku 27 tuu] kama vile bado mwaka,nyumbani kwangu nimetengeneza box tatu mfano wa lile la kupigia kura,na karatasi tatu-tatu,yaani goli tatu bila] [3-0] kama anavyotuelekeza mpendwa wetu mheshimiwa EDWARD NGOYAI LOWASSA rais mtarajiwa wa awamu ya tano wa jamhuri ya muungano wa tanzania yaani mpe kura:rais:ukawa mbunge:ukawa na diwani:ukawa.yaani ni raha wee acha tuu.ninachokifanya mimi mke wangu,watoto wawili,tegemezi wawili tunapanga foleni kila mtu ana karatasi tatu toka sebuleni-sitting,kwenda chumba cha kupigia kura-dinnig- huku muziki mkali wa msaga sumu:NAMPENDA LOWASSA ukiendelea.anaingia pale dinning mtu mmoja mmoja anatumbukiza karatasi sanduku la urais,anatumbukiza karatasi sanduku la mbunge na anatumbukiza karatasi sanduku la diwani.baada ya hapo tunakusanya masanduku,tunaanza kuhesabu kura:lowassa 6:mbunge ukawa 6:diwani ukawa 6.kisha wananiomba nitangaze matokeo.mshindi wa urais:ukawa,mshindi wa ubunge:ukawa,na mshindi wa udiwani:ukawa. RAHA,RAHA,RAHA.

    ReplyDelete
  12. ccm mbele kwa mbele ...................hapa kazi tu matusi ukiwa

    ReplyDelete
  13. "Talk is cheap" Ni rahisi sana kusema mbele kwa mbele lakini kumbukeni hamtoweza kujificha nyuma ya uongo kwa muda mrefu wala Nape hataweza kukikimbia kivuli chake. Machozi ya watanzania waliokaangwa kwenye ufukara wa kutuwa yanawalilia wana CCM usiku na mchana mtapigwa butwaa sana kwa maaamuzi watakayo fanya . Hapo ndipo mtakapoanza kujua mlienda mbele kwa mbele mkikanyaga wanyonge na kuwaacha nyuma huku mkigawana kodi za walala hoi na kuuuza maliasili zetu nje.

    ReplyDelete
  14. NA NGOJA UKWAWA TUCHUKUE NCHI WASANII MTAENDA KULIMA NA KUJENGA MADARAJA MANA HATA HAMUONI WANANCHI TUNATAKA NINI! POLENI KWA KUPISHANA NA GARI LA MSHAHARA
    HAPO KWELI KAZI MTAFANYA FROM 1/10/2015...ATAWAAJIRI MAGUFULI

    ReplyDelete
  15. hapa kazi gani na wenzake walisema hivyo hivyo wala hawana walilolifanya tumechoka na washenzi hawa

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad