Lowassa jina Kubwa Kuliko Yeye Mwenyewe

Kimtazamo jina la Lowassa linatisha na kutetemesha. Kwa wapenzi wake, Lowassa anapendwa na kuabudiwa- na lolote analosema ni kama amri kwa wapenzi wake.

Lowassa ameweza kuwateka mpaka wasomi, watu ambao unategemea wanaweza kuchambua na kutathmini kinachotoka kwenye mdomo wake. Lakini kwa wale wasiomjua vizuri Lowassa, picha kwao kidogo ni tofauti.

Nina ndugu yangu kanitembelea kutoka Perth, Australia. Ni Mtanzania ambaye ameishi Australia kwa kipindi cha miaka 30. Yeye hamjui vizuri Lowassa ila alipokuja tu Tanzania amesikia mengi kumhusu. Kichwani kwake akajenga picha ya mwanasiasa nguli, kama Nyerere au Mandela vile (alivyoniambia). Kwa sifa za watanzania wanazompa, ndugu yangu akajua kweli Tanzania sasa imepata kiongozi anayependwa na anayekubalika.

Mawazo yake hayo yalikuwa hivo mpaka alipoamua kwenda kwenye campaign za Lowassa pale Kigamboni hiyo jana. Ndugu yangu huyu alishangazwa sana na Lowassa 'mwenyewe'. Alitegemea kukutana na kiongozi anayejua kuongea na watu wake na mwenye kumwaga sera za maana.

Ndugu yangu anasema 'nimeona watu wanamshangilia kama 'wehu'. Hata kwa maneno ambayo hayasikiki vizuri na wakati mwingine kwa maneno yasiyokuwa na msingi.

Anasema 'kama kweli Lowassa ni mwanasiasa...mbona hata kuongea hajui?' Mimi sikumjibu...ila katika tafakari zangu nikaona kweli picha ya Lowassa iliyojengwa haendani na yeye mwenyewe. Amewekwa juu sana kuliko anapostahili. Huwa najiuliza hivi huyu mtu anasujudiwa kwa kipi hasa au amepata 'zali la mentali'?

By Mugisher

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. asante,mtoa hoja kwamba lowassa jina kubwa kuliko yeye mwenyewe.unasema ulipoenda kumsikiliza kigamboni jumapili tarehe 20 septemba 2015 ulitegemea labda mtu huyu mashuhuri kuliko wote tanzania kwa leo labda awe pandikizi la mtu na au BEJEBEJE yaani muongeaji kupita kiasi,hachagui neno,anahamasisha maasi,anatisha,lakini aaah ukakuta ni mtu poa,makini,anaongea kidogo anawakuna wasikilizaji wake,wanalipuka kumshangilia,kuimba,kucheza,unajua kwa nini,kwa sababu yeye ndiye mkombozi wa wanyonge,malofa ambao ndio wengi tena wengi sana tanzania.wakati unavuka uliiona bahari, basi walikwisha ambiwa na mgombea wa ccm tena kwa ukali na kauli thabiti toka kinywani mwake bwana john pombe magufuli kwamba atakaye kuwa hana nauli apige mbizi,aogelee kuvuka maji yakimshinda basi awe chakula cha samaki..in contrary ulimsikia lowassa jana akiahidi kwamba akishinda uchaguzi wa octoba hii,basi usafiri wa kivuko utakuwa buree-free- .jee uliona kilichofuatia pale? kwa takriban dakika kumi nderemo,vifijo,kuimba hakuna maelewano ni vicheko juu ya vicheko.huyu ndiye lowassa wa tanzania na,tanzania ya lowassa.wasalimie canberra nakufahamu vizuri sana nilikuwa rubani wa qantas air miaka 15.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Amewaongopea kuwaambia kivuko kitakua ni bure, hata ulaya vivuko na madaraja watu wanalipia sembuse huku africa

      Delete
  2. Pilot mzalendo safi kabisaa

    ReplyDelete
  3. wewe kabwela ulitaka MHs Lowasa aongee nini? yeye siyo mpiga porojo kwamba oooh, nitakununulieni meli, ohh nitakupeni milioni 50 kila kijiji!! ahadi ambazo zinajulikana c za kweli!! Watanzania c Wadanganyika tena! na hatutaki porojo!

    ReplyDelete
    Replies
    1. Million 50 kwa kila kijiji inawezekana,Tz kuna hela nyingi sana zilikuwa zinaibiwa na mafisadi akiwemo huyo Lowasa.Swali ambalo ulitakiwa ujiulize ni je ahadi itatekelezeka?Chambua pumba tupa kule.GOD BLESS TANZANIA.

      Delete
    2. hizo milioni 50 unazoongelea zishaliwa, hela hamna kwahiyo haitawezekana kaka, kwahiyo kwanini utoe ahadi zisizokuwa za kweli wakati unajua!! nchi ishafilisika hii!

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad