Magufuli Aigeuzia Kibao Taasisi ya Utafiti Iliyompa Ushindi wa Urais..Adai Amepunjwa Asilimia

Kahama. Mgombea urais wa CCM, Dk John Magufuli amesema waliofanya utafiti wamempunja asilimia kwani ana uhakika wa kushinda kwa asilimia 95 na si 65 kama zilivyotajwa kwa kuwa wananchi wanampenda, naye yuko tayari kufanya kazi ili kuwaletea maendeleo.

Akizungumza jana mjini Kahama, Dk Magufuli alisema: “Wapo wanaosema nimeshinda kwa asilimia 65, mimi ninasema nitashinda kwa asilimia 95, ninachoomba mjitokeze kwa wingi siku ya kupiga kura ili nitangazwe mshindi, ninawaahidi kwamba nitawatumikia na kujenga Tanzania mpya.”
Hivi karibuni, taasisi ya Twaweza ilitoa utafiti wake uliompa nafasi ushindi wa asilimia 65 huku mpinzani wake, Edward Lowassa akipata asilimia 25 na mgombea wa ACT –Wazalendo akipata asilimia 0.3.
Baadaye, taasisi ya Ipsos (Synovate) ilitoa utafiti wake ukionyesha kwamba alishinda kwa asilimia 62 huku Lowassa akipata asilimia 31 na Anna Mghwira akipata asilimia 0.3.


Post a Comment

5 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. :d ha ha ha ha acha nicheke miye niongeze uhai.....

    ReplyDelete
  2. ha ha ha ha ha !!!!!

    ReplyDelete
  3. Mta shangaaa nyie subiri muone kelele za kupanic,,,,, CCM ni ile ile,,

    ReplyDelete
  4. MWAKA HUU CCM HAMTAAMINI MACHO YENU KITAKACHO WATOKEA.JIFANYENI VIPOFU

    ReplyDelete
  5. Ukiona hadi Magu anapata upinzani mkubwa kiasi hiki pamoja na baadhi ya watu kuamini kuwa ana nafuu ukilinganisha na wengine katika chama chake inaonyesha wananchi wamechoka haswaa! Yeyote atakayeshinda mwaka huu aelewe kuwa wananchi wanataka maendeleo ya kweli wamechoka na hali ngumu ya maisha katika nchi ambayo imebarikiwa sana kila aina ya rasilimali

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad