MGOMBEA urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. John Magufuli anaendelea kukosoa Serikali ya CCM inayomaliza muda wake kwa kuiacha nchi katika dimbwi la umasikini.
Akiwa kwenye mkutano wa kampeni Uwanja wa Mkendo, wilayani Musoma, Mkoa wa Mara, amesema yapo mambo mengi hayapendi kwa sababu yanawaumiza wananchi na akichaguliwa kuwa rais atayabadilisha.
Ameutaja mradi wa maji uliopangwa kutekelezwa kupitia ziwa Victoria, aliosema kila siku unatajwa lakini hautekelezwi huku wananchi wa Mkoa wa Mara wakiendelea kupata shida ya maji.
Amesema haina maana kuwa na Waziri wa Maji wakati kunakuwa na mradi usiokwisha, akiwahakikishia wananchi kuwa atakapokuwa Rais, hawezi kushindwa kupata Sh. Bilioni 44 za kutekeleza mradi huo.
Dk. Magufuli ambaye amekuwa waziri katika serikali ya CCM kwa muda mrefu tangu alipoteuliwa kwa mara ya kwanza naibu waziri wa ujenzi mwaka 1995.
Kufufua viwanda vilivyo uliwa na watu kwa makusudi ambako kulikuwa na viwanda vingi ambavyo vimekufa mikononi mwa serikali ya CCM
“Naombeni kura zenu wananchi wa Musoma ili tuwatoe watu waovu kwani Serikali haitoki, watatoka watu wabaya ambao nitawatoa haraka sana,” amesema.
Magufuli azidi kuinanga CCM Kwa Kuicha Nchi Katika Dimbwi la Umaskini
2
September 13, 2015
Tags
MAGUFURI UKIPITA USHUKURU MAANA JK NDIO AMEWAANGUSHA CCM KWA KUTOKUA ANAWAFANYIA KWA VITENDO MAFISADI WAMEIBA SANA NA HAJAWAFANYA CHOCHOTE HATA MAFISADI WA ESCROW AMEWAACHA TU HAJAWAFANYA KITU WATU WAMEPIGA
ReplyDeleteKupita atapita NO DOUGHT,,,,,,,kikwete na lowasa washaiharibu nchi wakapumzike tu,,,,,,,CCM Mbovu sawaaa,,,,, Toeni Kashfa ya Magufuli kama mnayoooooo,,,,,,,mabadiliko tunayataka sana ila sio kwa mafisadi papa wanaijiita wasafi sasa hivi.
ReplyDelete