Mchezaji wa Yanga Canavaro Kuchukuliwa Hatua za Kinidhamu Baada ya Kupiga Picha na Jezi ya Yanga Kuonyesha Akimsupport Magufuli

Headlines za uchaguzi mkuu 2015 bado zinazidi kuchukua nafasi, tumekuwa tukiona watu maarufu kama wasanii wa filamu na Bongofleva wakionyesha hisia zao kwa wagombea wawapendao. Ila kwa wachezaji mpira wa miguu ni tofauti kidogo kulingana na sheria za vilabu vyao pamoja na mikataba yao.

Baada ya kuonekana kwa picha ya nahodha wa klabu ya Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Nadir Haroub Cannavaro akimsuport moja kati ya wagombea Urais wa mwaka 2015, kumekuwa na stori nyingi sana kuhusiana na sheria ya wachezaji kuonesha hisia zao kwa vyama wavipendavyo hususani wakiwa wamevaa jezi za vilabu vyao.

katibu mkuu wa Yanga Dk Jonas Tiboroha Kazungumza kuhusiana na Cannavaro kuvaa jezi za Yanga na kupiga picha akionyesha hisia zake kwa mgombea huyo.

Mimi nafikiri Cannavaro angekwenda akiwa amevaa nguo zake za kawaida na kuonyesha kumsuport Magufuli au mwingine isingekuwa na tatizo. Sisi tunachozungumzia ni yeye kuvaa jezi ya klabu na yenye nembo ya mdhamini wetu halafu unaonyesha kushabikia siasa, Cannavaro amekosea hivyo kama klabu tumekaa chini na tutaangalia hatua za kinidhamu zipi zichukuliwe
Tags

Post a Comment

8 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Alielimishwa/Walielimishwa juu ya hili?kama ndio achukuliwe hatua,vinginevyo asamehewe na kuonywa tu.

    ReplyDelete
  2. Mtaumia sana mwaka huu na kijiba cha moyo angeshabikia UKAWA ingehalalisha wala asingechunguzwa hii kampeni mtachukia kila mtu

    ReplyDelete
  3. Dr. J. Tiboroha hebu acha kumtishia mtoto wa watu nyau, YANGA YOTE pamoja na majengo yenu ni CCM, hebu mchukulie hatua tuone, kama hujapewa notice ya 'kuhama'......Manji anagombea udiwani CCM, Jerry alijaribu ubunge CCM na wengine wengi, wengi tu ni CCM, hilo jengo mmepewa na CCM, hizo rangi zenu za CCM........usituongopee bana, mumuwache Kanavaro ajinafasi.......CCM woyeeeee

    ReplyDelete
  4. Lakini hakija haribika kitu hapo, hao wadhamini wenywe Kilimanjaro ni CCM damu, lipi la ajabu hapo....... Tiboroha tuliza ball, tucheze ball

    ReplyDelete
  5. POLE SANA CANAVARO,NI MSHIKO HUO WA CCM,UNAJUA KAMA ILIVYOKUA KWA SHILOLE CCM WANATUMIA FEDHA NYINGI SANA SANA KUWAPONZA WATU MBALI MBALI HUSUSANI WASANII NA SASA WANAMICHEZO HII NI DHAMBI KUBWA.HEBU WEE ANGALIA PICHA YA CANAVARO MASKINI ALIIPIGA KWA HOFU,WOGA HAKUWA NA RAHA.UNAJUA PESA SIO KILA KITU KATIKA MAISHA,HESHIMA NA UTU MBELE.CCM MNATUMIA FEDHA NYINGI KWA KUWAHARAMISHA WASIO NA HATIA.CANAVARO NA CCM WAPI NA WAPI?LABDA UNGESEMA CANAVARO NA CUF.SASA PESA HARAMU ZA CCM ZIMEMDHALILISHA,ZINAMTOKEA PUANI,AIBU AIBU AJIANDAE NA ZOMEA ZOMEA KAYATAKA MWENYEWE LAKINI KWA NINI CCM?

    ReplyDelete
    Replies
    1. JAMANI UCHAGUZI WA MWAKA HUU NI AJABU KWELI KWANINI MNATANGULIZA FEDHA MBELE MTOTO WA WATU KAJISEMEA YA MOYONI MWAKE LEO HII KAPEWA PESA NA NANI? AU WEWE NDIO UMEMPA? YUPO NA AMANI ZAKE UNASEMA HANA AMANI UNAMSEMEA AU?

      Delete
    2. Kakuambia yeye ni CUF au kwa kuwa ni Mzanzibari unadhani wote ni wapenda CUF?kwa taarifa yako CCM Zenji ni zaidi ya hiyo CUF.
      CCM ni kambi popote

      Delete
  6. SAWA WEWE CCM JIFANYE KUMTETEA,LAKINI MWISHO WA SIKU AKIELEMEWA NA DHAMBI HII AMBAYO KWA SASA NI MZIGO KWAKE ATAPASUA JIPU.ACHENI HIZO CCM.NYINYI MWAKA HUU NI WA KUSHINDWA TUU WEZI WAKUBWA MNAFYATUA NA KUTAKATISHA PESA CHAFU KWA MABILLION KUTAKA KUJINUSURU,HAMNUSURIKI.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad