Mitambo ya Kuzalisha Umeme wa gesi Yawashwa.....Tatizo la Umeme Kukatika Kuisha LEO.

Mitambo ya Tanesco
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) limesema kazi ya kuunganisha mabomba ya gesi kutoka Kinyelezi I kwenda katika mitambo ya Ubungo I na II, jijini Dar es Salaam imekamilika.

Aidha, kazi ya kuwasha mashine 10 za mtambo wa Ubungo I imekamilika na  inategemewa tatizo la kukatika umeme litafikia tamati kuanzia leo.

Akizungumza na mtandao huu jijini Dar es Salaam jana, Ofisa Uhusiano wa Tanesco, Adrian Severin, alisema kazi ya kuwasha mitambo hiyo inahitaji umakini mkubwa  kutokana na mfumo unaotumika kuwa mpya.

Alisema kazi ya kuunganisha mabomba ya gesi imekamilika na tatizo lililokuwapo la kukatika umeme lilitokana na matengenezo ya mfumo mpya yaliyokuwa yakiendelea kwa ajili ya kuwashwa kwa mitambo hiyo mipya.

Aliwataka wananchi wawe na subira wakati kazi hiyo ikiendelea na hadi kufikia leo itakuwa imekamilika na umeme utapatikana kwa uhakika baada ya kuanza kuzalishwa kwa kutumia gesi kutoka Mtwara.

 “Kuanzia leo (jana) umeme umeanza kurudi kupatikana kwa uhakika katika mikoa mbalimbali pamoja na jiji la Dar es Salaam kutokana na mafundi kufanikiwa kwa kiasi kikubwa kuwasha genereta 10 za Ubungo I, hivyo mpaka kesho (leo) uzalishaji umeme utakuwa umeongezeka,” alisema na kuongeza:

“Watanzania wategemee umeme wa uhakika baada ya kuanza kuzalisha umeme wa gesi ya Mtwara kwani  kazi ya kuunganisha bomba la kusafirisha nishati hiyo imekamilika hivyo inatuhakikishia nchi kuwa na umeme wa uhakika hata kama mabwawa ya maji yanayotumiwa kuzalisha umeme yatakuwa yamekauka.”

Severin alisema gesi ya kutoka Mtwara inategemewa kuendesha mtambo wa Ubungo II wenye uwezo wa kuzalisha MW 105, mitambo ya Symbion MW 112 na Kinyerezi I, MW 150).

Alisema mtambo wa Ubungo I utaendelea kuzalisha umeme kwa kutumia gesi ya Songosongo na kwamba Ubungo II ndiyo utumia gesi ya Mtwara kwa kuwa inatosha kuendesha mitambo hiyo.

Severine alisema uzalishaji wa umeme kwa kutumia gesi utaisaidia serikali kuokoa takribani dola za Marekani bilioni moja kwa mwaka, ambazo zilikuwa zinatumiwa kununua mafuta mazito ya kuzalisha
Tags

Post a Comment

6 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. hapo itakua kuku, halafu munasema ooh chama cha mapinduzi hakijafanya lolote haya sasa umeme huo wa gesi kaleta nani baba zenu ? acheni kuchonga ngebe

    ReplyDelete
  2. Mbona hamtuonyeshi Picha kwenye magazeti wakati mitambo ya Richmond na dowans ilipokua inaingizwa ilikuwa inaonyeshwa?

    ReplyDelete
    Replies
    1. MITAMBO YA RICHMOND KAMUULIZE LOWASSA

      Delete
  3. WASIMAMIZI WAKUU WAHANDISI NA MAFUNDI MCHUNDO UKIACHA WAGENI NI VIJANA WATANZANIA WANACHAMA,WAKEREKETWA,WAPENDA MAGEUZI WANASUBIRI KWA HAMU KUBWA UKAWA KUSHIKA DOLA.HONGERENI VIJANA MHESHIMIWA LOWASSA ALISHASEMA GAS PRODUCTION NI SERA- KIPAUMBELE CHAKE,SUBIRINI MKAO WA MAENDELEO YENU FAMILI ZENU WANA KUSINI NA WATANZANIA WOTE KWA UJUMLA WETU.NINA AMINI NA NAWAONENI HAKUNA MWENYE SCARF YA KIJANI WOOOTE NYEUPE,NYEKUNDU,BLUU KIJANI MWACHIENI MWIGULU NCHEMBA MWENYE FAILI KIBAO TAKUKURU TUNAZOSUBILI KUZI -ACTIVATE BAADA YA UCHAGUZI MKUU OCTOBA 25,2015.

    ReplyDelete
  4. Sisiem itoe serikali imkabizi mtu mwingine ? Haya tutaona hayo maajabu

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad