Mnyika Aongea na Waandishi Ngome kuu ya UKAWA, Awajibu NEC Kuhusu Mazingira ya Wizi wa Kura 25 Oct


Mnyika:Katika Magazeti Yenu Jana mlimnukuu M/kiti wa TUME akijibu tuhuma za UKAWA juu ya mazingira ya wizi wa Kura

Mnyika: Jaji Lubuva Jana amejibu kwa wepesi tuhuma za wizi wa kura

Mnyika: Lubuva anasema ukishapiga kura rudi Nyumbani. Nawaomba vijana na wapiga kura wengine waipuuze kauli ya Jaji Lubuva!

Mnyika: Jaji Lubuva amedai yupo tayari kuziba mianya ya wizi wa kura.Nitataja mianya hiyo ili Jaji Lubuva ajibu masuala haya!

Mnyika: Matokeo ya Rais kubandikwa kituoni sio jambo jipya. Ni suala la kisheria. Nawaomba watu wasome sheria ya Uchaguzi

Mnyika: Masanduku ya kura kupelekwa kituo cha majumuisho sio jambo Jipya.

Mnyika:Lubuva anasema matokeo yatascaniwa jimboni.Hili sio jambo jipya. Mwaka 2010 matokeo yaliyoscaniwa yalikuwa tofauti na karatasi halisi

Mnyika: Jaji Lubuva aseme hadharani, ni lini wataalamu wetu wa IT wakakague na kuhakiki mfumo wa kutuma matokeo ili kuepuka goli la mkono

Mnyika: mfumo wa kujumlisha kura mwaka 2010 ulikuwa na mapungufu makubwa yaliyopelekea uchakachuaji wa kura!

Mnyika: Jaji Lubuva amesema uhakiki umefungwa, kuna jambo kubwa limejificha.Kama hakuna uhakiki daftari limeshakuwa la kudumu!

Mnyika: Mpaka tunavyozungumza hatujakabidhiwa daftari la kudumu la wapiga kura, Takwimu zinazotolewa idadi ya wapiga kura haziaminiki!

Mnyika: Tume iseme ni kwa nini mpaka sasa hawajatoa nakala za "soft copies" kwa vyama vya siasa ili wazihakiki?Hapa bao la mkono limejificha

Mnyika: UKAWA na vyama vingine Lazima viende kuhakiki Database ya Tume Makao makuu. Kwanini Lubuva hataki sisi tuende kuhakiki?

Mnyika: Jaji Lubuva anasema ipo kamati ya IT, muulizeni hiyo kamati ya IT ya vyama vya siasa inaundwa na nani?

Mnyika: Majeshi kuandikisha namba za askari, IGP alikiri jeshi kufanya hivyo kwa baadhi ya mikoa, kuna kitu kimejificha!

Mnyika:IGP alikiri suala hili limefanyika, msemaji wa TPDF alikanusha, kauli zao zilikinzana.Tume iseme ni kwanini majeshi yaliandika namba?

Mnyika: Suala la kuhamisha watumishi wa Tume, limeamia kwa wakurugenzi baada ya Rais, kuteua mkurugenzi Mpya!

Maswali: David Radio5: Wapiga kura wa Mara ya kwanza, na wasiojua utaratibu je wanabakia wapi baada ya kupiga kura?

Mnyika: Wapiga kura, wawe makini kuhakikisha wanapiga kura Siku ya tarehe 25 Oktoba!

Mnyika: Daftari la kudumu halitolewi kwa wakati ili kuruhusu goli la mkono!

Mnyika: wapiga kura wajielekeze kuangalia majina ndani ya daftari la wapiga kura na sio orodha ya wapiga kura inayobandikwa nje ya kituo!

Mnyika: Orodha ya wapiga kura inayobandikwa nje ya kituo inaandaliwa na manispaa, na daftari analopewa wakala limeandaliwa na Tume

Mnyika: Tume itoe Daftari la kudumu la wapiga kura, Jaji Lubuva amesema atalitoa daftari Siku 4 kabla ya Uchaguzi, hapa amejichanganya!

Mnyika:Hatua ya pili ni kutoa 'permanent voter register' hili ilipaswa kutolewa mapema

Mnyika: Kuna madaftari mawili, provisional voter register, hili tulitakiwa kupewa kabla ya uhakiki wa wapiga kura, hili hatujapewa!

Mnyika: Rai yangu kwa wana UKAWA, wasikate tamaa kufuatia matamko ya mawaziri mbalimbali

Mnyika:Juu ya matumizi ya vyombo vya Serikali kujihusishanaUchaguzi, linaongozwa naraisi,Bunge limevunjwa ila baraza la mawaziri linaendelea

Mnyika: Iundwe kamati ya pamoja ya vyama vya siasa ya IT ikakague Daftari na kuliboresha ili kuzuia goli la mkono!

Mnyika: Swali la1: Tulianza kusema haya mambo mapema, waliamua kufumba masikio na macho!

Maswali:Fred kutoka Mtanzania: Kisheria mnatakiwa mpate soft copy ya Daftari baada ya Muda gani?

Maswali: Francis kutoka ATN: suala la uhakiki wa BVR hamuoni Siku zimebaki chache na kwanini msingeliibua suala hili mapema?

Mnyika: Tume iliwahi kukiri kuwa haiko huru mbele ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba, WaTZ wasikubali faster faster hii.

Mnyika: Wanapeleka huu mchakato faster faster, rai yangu tusisubiri tarehe 25 Oktoba, tuanze sasa kudhibiti goli la mkono!

Mnyika: Ndani ya nchi tunao watazamaji wasisubiri mpaka Uchaguzi uishe, waende Tume kutazama mfumo huu wa ujumlishaji wa kura

Mnyika: Nawaomba 'Waangalizi wa Uchaguzi' watoe ripoti zao mapema juu ya haya masuala!

Mnyika: Tume ya Uchaguzi sio Mali ya watu binafsi, ni tume ya Taifa letu.

Mnyika: Kijana ukishaona matokeo yamebandikwa, piga picha matokeo hayo na uyatume kwenye WhatsApp!

Mnyika: Kama kuna MTU ataniita mchochezi kwa kusema 'first time voters' wakae mita 200 kusubiria matokeo basi atangulie mahakamani,

Mnyika: First time voters, kukaa ndani ni kosa kisheria, kukaa nje si kosa kisheria, kisheria wanakaa mita 200!

Maswali: David Radio5: UKAWA mtafanya nini endapo tume haitafanya mnayosisitiza wafanye?

Mnyika: Nasisitiza BVR ni Bomu la kufungwa bao la mkono, yote tuliyosema yazingatiwe na wahusika!

Maswali: Prosper - The Guardian: Mnataka wataalamu wa IT wakakague daftari pekee, vipi kuhusu ukaguzi wa idadi ya kura zilizopigwa?

Mnyika: Kama Tume haitasikiliza haya tunayosema wanajitengenezea mazingira ya kupelekwa ICC!

Mnyika: Local monitors wa Uchaguzi wapo wachache, wanasubiria matokeo majimboni, kila mpiga kura lazim awe monitor!

Mnyika: Nje ya kituo cha kupiga kura sisi wapenda Amani, tutawalinda mawakala wetu, wasirubiniwe kupokea hongo ndani ya vituo vya Uchaguzi!

Mnyika: Marando alisema atatangaza matokeo, sasa kwa sababu anaumwa yupo hospitali Mimi Mnyika nitayatangaza.

Post a Comment

11 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Bao la mkono lipo Na ndo maana CCM wana jeuri
    Watanzania msitoke kwenye vituo ya kura
    Tutatoa vyakula bure kwa kila mpiga kura

    ReplyDelete
  2. NILIMSIKILIZA SANA JAJI MSTAAFU DAMIAN LUBUVA WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI AKIELEZEA NA PIA AKIJIBU MASUALI YANAYOHUSU DUKU DUKU LA WAPIGA KURA WA TANZANIA, KWAMBA TUME NI TARISHI WA CCM.KISHA TENA NIMEMSOMA MHESHIMIWA MNYIKA NA KUMUELEWA VIZURI SANA.NI HIVI,KWANZA YALE YOTE ALIYOYATAMKA JAJI LUBUVA YAMEJAA UONGO NA HILA ZA`WAZI ZA KUKIBEBA CHAMA-DOLA,CHAMA TAWALA CHA CCM. KWA TAARIFA YENU WANANCHI KUANZIA TAREHE 22 SEPTEMBA 2015 TUME ILIWAPOKEA WATAALAMU WANNE[4] WA INFORMATION TECHNOWLEDGE -IT-KUTOKA CCM MAKAO MAKUU.HII NI SIRI KUBWA NA WANACHOKIFANYA WAHUNI WALE WA CCM HIVI SASA PALE TUME NI KUUANDAA MFUMO-WIZI WA BALLOT SOFT-WARE,SOFT COPIES,KUIBADILI DATA BASE TA TUME NA KUIWEKA KIVINGINEVYO BVR.LENGO LA WAHUNI HAWA WA IT KUTOKA CCM NI KUHAKIKISHA ANGALAU WANAKOKOTOA KURA'HEWA' ZA WIZI MILLION SITA i.e 6,000,000. TATIZO KUBWA NI KWAMBA JAJI LUBUVA AMEELEMEWA NA CCM NA HATAKI KUKIRI HADHARANI KUWA AMEELEMEWA. TATIZO LAKE LA PILI NI KWAMBA MASUALA HAYA YA CYBER PIRATING NA MFUMO MZIMA WA KIWIZI WA KUPITIA MITANNDAO YAANI IT LUBUVA NI MBUMBUMBU,MBUMBUMBU KABISAA NA WALA HANA UNAFUU HATA KIDOGO KWA HILO.INATAKIWA KWA SASA,TENA HARAKA AWAKARIBISHE WATAALAMU WALIOBOBEA WA IT KUTOKA VYAMA VYOTE VINAVYOSHIRIKI UCHAGUZI HUU ILI WAISAIDIE TUME KUJIWEKA SAWA NA HURU ZAIDI.NA TATU HARAMU HII KUBWA SANA YA CCM YA MATUMIZI MACHAFU YA FEDHA NYINGI SANA KUHARAMISHA WATU NA TAASISI MBALI-MBALI ILI MRADI WAJINUSURU NA JANGA KUBWA LINALOWASUBIRI LA ANGUKO TOKA CHAMA TAWALA HADI CHAMA CHA UPINZANI LIMEKWISHA MKUMBA JAJI LUBUVA.TUNA SHAKA KUU NA USAFI WAKE.CCM IMEENDELEA NA WIMBI LA KUTISHA KABISA LA MANUNUZI-WATU.MWISHO NINASEMA HIVI: KWA HALI HII YA SASA TA TABIA CHAFU YA CCM NI DHAHIRI KWAMBA MACHAFUKO MAKUBWA SANA YA NCHI HAYAEPUKIKI IWAPO HAKI HAITATENDEKA KWA SABABU HAWA WAPIGA KURA WATANZANIA WA LEO TAYARI WAMEKWISHA JIHAKIKISHIA MSHINDI HALALI KWA SABABU WAMEMCHAGUA,WANAONA,WANASHUHUDIA WA KURA YA URAIS NI MHESHIMIWA EDWARD NGOYAI LOWASSA.NO SHORT OF THIS NAKED- TRUE FACT.JAJI LUBUVA MZEE WANGU:NAKUOMBA SANA USOME WARAKA WANGU.NAKUOMBA.NI NYINYI TUME MTAKAOLINUSURU TAIFA LETU.WABILLAHU TAWFIQ.

    ReplyDelete
  3. Huyu dogo anaumwa ugonjwa wa mifuzhobia!

    ReplyDelete
  4. hakuna wa kushindana na Mungu, hatawafanyaje kama Mungu akipenda Lowassa kuwa Rais atakuwa tu! hata waibaje!

    ReplyDelete
  5. Chadema hatuwashangai, hata mfanyiwe nini hamtakaa mridhike.
    Jiandaeni kuandamana jkama kawaida yenu, kisha muende mahakamani mtachagua kama ni ICC au the Hague......TUMEWACHOKA

    ReplyDelete
  6. Mbona mnaliogopa sana hilo goli la mkono, haya basi tumebadilisha litakuwa 'bao la kisigino' ..........

    ReplyDelete
  7. Hivi jamani, pamoja na waangalizi wooooote kutoka mataifa mbalimbali waliopo kushuhudia uchaguzi, bado tu cdm mnalalamika?? 'Mnawahemsha' watoto wa watu wapigwe, nyie mkistarehe na familia zenu, kama mlivyowafanya Arusha, mliwatanguliza mbele, nyie mkajificha........na nyie 'wafurukutwa' msikubali kufanywa chambo, watangulie viongozi mbele nanyi mfuate.....litakalokupata utahangaika na familia yako, humwoni Mnyika, Mbowe wala Lowasa kukusaidia.....MTAJIJU

    ReplyDelete
  8. Mnyika, watanzania wa leo wana akili hawahitaji akili za kushikiwa! ACHENI kutengeneza MAZINGIRA na HOJA za kuja KUHALALISHA vurugu...........nyinyi wakati huo mmekaa mbaliiii mnataka kuwatumia WANANCHI kama ngazi kufikia MALENGO na kutimiza UCHU wenu!?

    Unachojaribu kutengeza sasa hivi ni picha kuwa LAZIMA tu CCM ishindwe na ikishinda hata kihalali basi ni BAO la mkono!?, siasa gani hizo brother, kwani ni LAZIMA TU HATA IKIBIDI WATU WAFE ni LAZIMA LOWASSA awe RAIS1???

    Si muwaache wananchi WAAMUE?

    ReplyDelete
  9. si muache wananchi waamue unamwambia nani?jee unaweza ukawaambia hawa fedhuli ccm wakakuelewa.wamekwisha kwambia mara nyingi tena kwa kutamba kwamba hawako tatari kuiachia ikulu.na kama ni suala la kuachia wananchi waamue basi ni hivi:wingi wa kura za kihalali ndio utakaokubaliwa na wananchi kinyume cha hapo UAMUZI UTAHAMIA MIKONONI MWA WAPIGA KURA NA SI DOLA TENA.NYIE CCM NI WA SIKIO LA KUFA,SIKU YA KUPIGA KURA TUTAWACHINJA KIULAINI KAMA KUKU WA KIZUNGU. ccm mtakumbukwa zaidi kwa maovu na mabaya mengi mliyoifanyia tanzania na watanzania wenyewe na kamwe hamtaikwepa hukumu hiyo,waallah sisi na nyinyi.

    ReplyDelete
  10. Mnyika kama unataka kujua mambo ya jeshi ni vema ukajiunga nalo ili ujue zaidi na sio kumuuliza lubuva, wananchi watapiga kura tena kwa mtu wanaempenda na sio kuwalazimisha, hata wawe wagombea 100 lkn mshindi ni mmoja

    ReplyDelete
  11. Mnyika kama unataka kujua mambo ya jeshi ni vema ukajiunga nalo ili ujue zaidi na sio kumuuliza lubuva, wananchi watapiga kura tena kwa mtu wanaempenda na sio kuwalazimisha, hata wawe wagombea 100 lkn mshindi ni mmoja

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad