Mtoto wa Miaka (4) Amekufa Kwa Kuteketea kwa Moto Wakati Baba yake Akimimina Petrol

Nyumba yenye familia ya watoto watatu ya Mbala Jijini Dar es Salaam, jana majira ya saa mbili usiku iliteketea kwa moto baada ya Baba mzazi wa familia hiyo kufungua petrol iliyokuwa ndani kwake na kupelekea nyumba kuwaka moto na kusababisha kifo cha mtoto mdogo wa miaka minne (4).


Baba na mtoto wake waliteketea kwa moto (Baba aliokolewa) ambapo wakati huo Baba na mwanae huyo walikuwa ndani huku mke wake aliyetambuliwa kwa jina la Catherine Abiria, akiwa na watoto wengine wawili nje.



Mashuhuda wa tukio wanasema katika hatua za kumimina petrol hiyo kwa bahati mbaya ndipo palipotokea mlipuko ambao ulipelekea kifo cha huyo mtoto ambaye alizikwa jana hiyo hiyo kutokana na kuungua vibaya.



Baba wa familia ameumia vibaya amelazwa katika Hospitali ya Tumbi na hali yake inaelezwa kuwa ni mbaya sana.



Funzo; Tuepuke kuweka vimiminika vinavyoweza kusababisha ajali kama hizi na kuwapoteza wapendwa wetu.
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad