Nawaheshimu Mashabiki Wangu ndio Maana Sishiriki Kwenye Kampeni za Siasa- Joh Makini

Joh Makini
Joh Makini anawaheshimu mashabiki wake kiasi ambacho amekataa mamilioni ya fedha kushiriki kwenye kampeni za siasa zinazoendelea.

joh makini

Hitmaker huyo wa Nusu Nusu amesema ingawa wakiwa kama wasanii wana uhuru na haki ya kufanya hivyo, lakini wao kama Weusi wameona watawachanganya mashabiki wa wao.

Unajua sisi kama wasanii tunaheshimu sana audience yetu, hasa mimi kusema ukweli naheshimu sana audience yangu,” Joh aliiambia Clouds FM.

“Nina mashabiki kutoka vyama vyote, vile vile nina mashabiki kutoka dini zote, kwahiyo najaribu pia kuepuka kuwatenganisha, ingawa sio vibaya kwa mtu yoyote hata msanii kuonesha mimi na-support upande huu, ni haki ya kila mtanzania. Kusema kweli kwa wasanii sidhani kama wanakosea, kwa sababu wanakosea vipi?”

“Kwa sababu mimi kama msanii ni mfanyabiashara end of the day ukinilipa hela yangu, nije ni perfome nyumbani kwako sebuleni au kwenye kampeni yako, mimi nikija pale nitafanya yangu na mwisho wa siku hao wanaopiga kelele, hawajui kwamba hakuna mtu anaweza kukataa kufanya kazi yake akilipwa. Mwisho wa siku kama mtu ameenda kufanya show na amelipwa hela yake hiyo ni haki yake.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad