NEC: Matokeo Ya kura za Urais Yatabandikwa Vituoni Ili Kuondoa Malalamiko Ya Kura Kuibiwa

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imesema kuanzia sasa itaanza kubandika matokeo ya kura za urais kwenye vituo vya kupigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu ili kuongeza uwazi na kupunguza malalamiko ya wizi wa kura.

Mpango huo umeelezwa na Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji mstaafu Damian Lubuva alipozungumza na viongozi wa dini jijini Dar es Salaam ambao walimueleza hoja hiyo kuwa moja ya vigezo vitakavyokamilisha mchakato huo kwa amani na utulivu na kuwaridhisha wagombea na wafuasi wa vyama.

Alisema licha ya kubandikwa vituoni, utangazaji wa matokeo utafanyika kama kawaida katika kila ngazi, udiwani kwenye kata, ubunge wilayani na urais Tume makao makuu.

Jaji Lubuva aliwahi kunukuliwa siku za nyuma akisema kuwa “hakuna haja ya kuwa na shaka wala kuandaa vijana wa kulinda vituo. Hakutakuwa na nafasi hiyo kwa sababu kura zote zitahesabiwa na kubandikwa huko.

“Kila mtu atajua diwani gani kapata kura ngapi, na mbunge na hata rais aliyemchagua. Itakuwa tofauti na zamani ambapo zilikuwa zinasafirishwa na kuhesabiwa wilayani ambako watu wengine walidhani yanabadilishwa,” alisema.
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. 'WATU WENGINE WALIDHANI YAMEBADIRISHWA' HII NI SEHEMU YA KAULI YAKO MHESHIMIWA JAJI MSTAAFU DAMIAN LUBUVA MWENYEKITI WA TUME YA TAIFA YA UCHAGUZI WAKATI UKITANGAZA KUWA MWAKA HUU MATOKEO YA KURA YATABANDIKWA VITUONI YAANI DIWANI,MBUNGE NA RAIS.HII NI SAWA KIINGEREZA TUNASEMA LONG OVERDUE.YAANI BAADA YA WIZI WA KURA NA MADHARA MENGI YA MIAKA MINGI.NIMEKUNUKUU KAULI YAKO JAJI KWA MAANA MOJA KUBWA.UMEITAMKA KANA KWAMBA WEWE NI KIONGOZI WA CCM NA IMEAMULIWA HIVYO KI-SHINGO UPANDE,KWAMBA HUKUPENDA LAKINI UFANYEJE,NA UNATIMIZA HILO ILI TUU KUONDOA MALALAMIKO.HII SIYO SAWA NA NI KOSA KUBWA LA KAULI,WANAKUANDIKIA USOME AU UNAANDIKA MWENYEWE? HOFU YA KWELI YA WIZI WA KURA KWA MWAKA HUU 2015 NI KUBWA KULIKO WAKATI WOWOTE.HII NI KWA SABABU CCM KWA ASILIMIA MIA MOJA [100] WAMESHABAINI KUWA WATASHINDWA,TENA WATADONDOKA VIBAYA MNO. TUME INAPASWA KULIPA SOMO HILI KIPAUMBELE KIKUBWA.WAMEISHA SEMA CCM TENA MARA KADHAA KUWA HAWATAKUBALI KUIACHIA IKULU,NA,SI WEWE,SI MKURUGENNZI WA TUME MMEWAHI KULITOLEA KAULI TAMKO HILI LA KUCHOCHEA UVUNJIFU WA AMANI LINNALOENDELEA KUTAMKWA NA VIONGOZI WA CCM.HII NI DALILI YA HATARI NA,DHIHIRISHO KUWA TUME YA TAIFA Y A UCHAGUZI INAWAOGOPA NA KUWASAIDIA CCM.USHINDI WA LOWASSA UPO WAZI MNO KWA SABABU NI LAND-SLIDE.RAIA TUPO MACHO A TO Z.

    ReplyDelete
  2. jaji Lubuva,asante kwakutattua tatizo moja kubwa kati ya mengi yanayowasumbua wapiga kura.
    Hakikisheni hilo namlitekeleze.
    La pili Mbona bado watu wengi wanamatatizo na vikatio vyao.wanahakiki taarifa wanaonekana hawapo.hamtoi taarifa yoyote mahali pakuhakiki .hili pia tatueni siku zinahesabika.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad