Ni Watoto na Ndugu wa Viongozi wa CCM tu Ndio Waliobaki Kuipigania Kufa na Kupona

Nimekuwa nikifuatilia mielekeo ya kisiasa ya viongozi wa CCM na watoto wao pamoja na watu wao wengine wa karibu kinasaba, na kushuhudia kuwa, ukiacha viongozi wenyewe wa CCM, kundi la pili ambalo linafanya kila kinachowezekana kujaribu kukinusuru chama hicho ni la watoto wa viongozi hao. Wapo watoto wengi wa viongozi wa CCM, hasa katika magroup ya WhatsApp na mitandao ya kijamii, wanapigana kufa na kupona kunusuru ulaji wa wazazi wao.

Kete yao kubwa ambayo wanaitumia kuonyesha umma kuwa upinzani haufai ni kuwa "Lowassa ni fisadi". Wengi wamejitoa ufahamu, wana uwezo mdogo wa "kureason" unaoambatana na kuchanganyikiwa, na hoja wanazojenga wakati wa malumbano ni za kushangaza mno!

Hutaamini majibu, ushindani na hoja zao pindi utakapokutana nao na kujaribu kuwaeleza kuwa tulipofika kuna haja ya mabadiliko!

Hoja zao zinatia hasira vibaya sana na kuashiria kuwa wao wana hatimiliki ya hatma ya Tanzania.

By LifeHacker/JF
Tags

Top Post Ad

Below Post Ad