Ninatafakari hatima ya CCM kama Lowassa angekuwa ni mgombea Urais wa CCM

Kuna mengi sana yamesemwa kuhusu mchakato wa kumpata mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM uliofanikisha kumpata John Magufuli kuwa mgombea Urais.

Kwa kuangalia kwa nje kabla ya kumteua Magufuli, CCM ilikuwa inakabiliwa na hali yenye mashaka na hatari (awkward situation) kuhusu hatima ya Lowassa.

Kwa kuangalia kwa nje, maamuzi yoyote kuhusu Lowassa ndani ya CCM yalikuwa yanaiweka CCM katika wakati wa aina yake kwenye uchaguzi.

Kwa sasa ni zaidi ya mwezi mmoja tokea mchakato wa kumpata mgombea Urais ndani ya CCM umalizike. Katika muda huu majibu ya maswali mengi yameanza kupatikana.

Kwa sasa ninaweza kusema, kama mgombea wa Urais kwa tiketi ya CCM angekuwa ni Lowassa, CCM ingekuwa imeishashindwa kabla hata ya kuanza kampeni za Uchaguzi Mkuu.

Ndani ya mwezi mmoja akiwa CHADEMA, Lowassa ameonyesha udhaifu mkubwa pamoja na kusaidiwa na CHADEMA/UKAWA kulibeba/kulishusha zigo la ufisadi ambalo amelibeba kwa miaka mingi. CCM wasingeweza kuhimili hoja kutoka upinzani huku wakiwa wamebeba zigo lote la ufisadi na hasa ikichukuliwa hata uwezo wa Lowassa ni mdogo katika kuhimili jukwaa la kisiasa achilia mbali afya yake.

Lowassa akiwa mgombea wa CCM asingeweza kusema maamuzi ya kuendelea na mkataba wa Richmond yalitoka kwenye mamlaka ya juu ili kukabiliana na hoja za wapinzani. Wapinzani kama walivyo watu wengine wasingeamini haya maneno mepesi yasiyokuwa na chembe ya ukweli kiutendaji kwa Waziri Mkuu ambaye aliwahi kusema hawajakutana barabarani na Rais Kikwete.

Kuna wapinzani wengi tu wanaamini maneno ya Lowassa ni uwongo lakini kwa vile Mbowe na genge lake amewaletea Lowassa kama mgombea Urais, wanajikuta hawana njia nyingine zaidi ya kumkubali kama mgombea Urais. ndiyo maana kwa sasa kuna hoja ambazo wanadai wanamtumia tu Lowassa ili kushinda uchaguzi mkuu kwa sababu ana nyenzo fedha.

Kukatwa kwa Lowassa na Uthubutu wa kuihama CCM na kujiunga na CHADEMA kumefanya CCM wapumue na kulifanya zoezi la kumpata Rais wa Tanzania lichukue sura nyingine.

Wahenga walisema, Usilolifahamu ni kama...

Post a Comment

4 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. We kweli hovyo tens hovyo kweli ivi lowasa uwo ufisadi wake mmeujua Leo kama mnajua ni fisadi mnangoja nin kumshtaki acha ushenzi fara wewe angalia cha kuandika hapa

    ReplyDelete
    Replies
    1. wewe mimi sikutukani ila nakuambia .mimi kujuwa bwana mkubwa fisadi nilisikia kwa chadema .na sio leo nilisikia muda mrefu .na walituambia wao .mbona hawatokii na kuja kutuambia walitudanganya

      Delete
    2. Lowassa Atapita tu. Nyinyi CCM kuanzia raisi wenu anayetoka hajamkanusha Lowassa. Lowassa kamwambia Kikwete amri ilitoka kwake kama raisi kakaa kimya. Watu wa CCM bado mnalindana. mnamlinda Kikwete ambaye ni kiongozi wa ufisadi mkuu Tanzania. Ni yeye aliitwa Ikuru Marekani. Ni yeye aliyepewa majina hewa toka Marekani, Ni yeye aliyetoa kibali kupeleka Twiga magharibi kupitia Uraisi wake. Ni yeye aliyeipotosha Katiba. Ni yeye aliyewasafisha ESCROW, ni yeye aliyetoa amri pesa ya epa ilipwe toka Benki kuu, ni yeye aliyewaleta Wawekezaji na kuwapa ardhi ya serengeti na nyinginezo bure. Kwa nini, haelewi Maendeleo ya nchi nguzo kuu ni Wananchi wenyewe na si wawekezaji toka nje wenye maslahi tofauti na maslahi ya Watanzania. Nyere alisema Waangalie mabepari na makabaila. Aliwalinganisha urefu wa makucha yao na ya simba. KIkwete Kauleta ubepari nchini bila kuwa na Elimu mbadala ya kujua ubepari ni nini. Kawaleta makabaila wenye kujua udhaifu wake na kumwingilia kuitawala Tanzania. Amekuwa uso wa mabepari na makabaila unaohatarisha maendeleo , elimu, na usalama wa nchi hii. Huku kupigana mapanga hii hali si ya Watanzania. Huku kupiga mabomu hadharani kama unampiga nyani hii si mila ya Mtanzania wala Mwafrika. Hii imetokea baada ya kuikosa Elimu safi na kujua kwamba juhudi zetu za kazi zikiambatanishwa na elimu safi na juhudi za Watanzania Wenyewe. Si Wachina, si Wamarekani, si Waarabu, Si Wafaransa na si Waingereza wala Warusi. Hawa wote wanatafuta kujaza matumbo na mifuko yao kupitia uongozi mbovu na mfumo mbovu kisiasa. Kupitia maraisi watatu, Tanzania imeingiliwa kinyume na iko hatarini. Ni namna gani Tanzania itageuza kibao hiki. Haya mataifa yote yanachochea kipesa kuona kama Watanzania wameamka na mashujaa kuitwaa nchi yao. Wakishirikiana na Chama dora wako tayari kwa lolote kulinda maslahi yao.
      Piga kura yako mtanzania Ujikomboe kwa Kuikana CCM. weka shahada yako ya kupigia kura, nenda kimya kupigia sio CCM na ujirudishie heshima na hadhi yako na ya nchi. Mungu Wabariki Watanzania Wote popote Walipo Duniani. Dumisha Uhuru na Amani, lakini usiishie Hapo. Rudisha Mali ya Mtanzania na uweke mikononi mwa Watanzania Wenyewe na vizazi vyao Vjavyo. Naipenda Tanzania Yangu.
      Sitaiuza Wala sitawauza Watu wake hata kwa Matrilioni ya pesa. Watu ni mali ya Thamani kuliko kitu kingine chochote.

      Delete
    3. Thank you Udaku. We need you.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad